Kanisa Katoliki lapoteza Mapadri 25 na Watawa 60 kwa tatizo la upumuaji ndani ya miezi miwili

Mkuu hata kama ni kutetea unachokiamini,hebu basi wakati mwingine changanya hata na akili kidogo [emoji1787] [emoji1787]
Mkuu hata huko kwa wenzenu chanjo siyo lazima na kuna watu hawataki kuisikia.

Kwa hiyo nanyie hapa mkitaka vukeni hapo Kenya mchanjwe
 
Kwahiyo ile tuzo ya kumaliza corona aliyopewa Magufuli ni fake?
Sio fake tuzo ilitolewa na watu waamini maombi kuwa yana nguvu Wa Tanzania Assemblie of God Ni kanisa kubwa lina wachungaji wengi kuliko mapadre wa kanisa katoliki sababu kila mitaa mijini na vijiji kuna Kanisa la TAG lakini hawajazika mchungaji hata mmoja kwa Corona toka Corona ianze wanakufa mapadre na masista wenye imani haba ya uwezo wa Mungu kuwa aweza dhibiti Corona!!
 
... kwa takwimu zipi unaleta uharo wako hapa? Katoliki wameweka takwimu; TAG hawajatoa takwimu; serikali haitaki kutoa takwimu; huna facts acha kuongea upuuzi.
 
... huko mbali sana Mkuu; wavunjilie mbali mahospitali yote ili tuishi kwa maombi tu! Unakuta jitu linaongea utafikiri kichwani hamna kitu!
 
Kati ya hao Mapdre 25, mmoja Ni kaka yangu baba mmoja mama mmoja. Rest in Peace Our first Born.
Msg zako za Whasap nazisoma Sana naona kama upo hai brother![emoji24][emoji24]
Pole Sana kiongozi
 
Elimu yako ni ya kiwango gani? Aisee
 
“Mwamini Mungu, lakini mfunge vizuri Ngamia wako”-Mtume Muhammad S.A.W

Mungu huwa halipi maombi bali hulipa jitihada!Kupiga maombi ya nguvu wakati hakuna mipango wala hatua(Actions) sahihi,stahiki na madhubuti za kupambana na Corona ni kumkejeli Mungu.
 
Halafu anatokea Rais fulani mataputapu anasema Corona itaondoka kwa maombi!
 
Ukichimama nchale ukikaa nchale.
Ndio hii hapa.
Hadi meko akili imkae sawa
 
Maneno ya maaskofu, mapadre na walei wengine ndio yananiongoza, kwanza kamwe sitojifukiza kwa sababu kila binadamu mwili wake una kiwango chake cha kuhimili joto la nje ili liwe sawa na joto la ndani.

Viongozi wangu wamesisitiza nivae barakoa hii navaa kila siku, wamesema ninawe mikono kwa maji tiririka, wamesema niepuke mikusanyiko na nichukue tahadhari bila kuleta utani.

Sitojifukiza kwa kua hawajanishauri kujifukiza, Viongozi wangu wa dini wakisema kuna chanjo haraka sana nitachanjwa maana kila mmoja apambanie maisha yake na kwenye hili la corona kamwe sitowasikiliza wanasiasa.
 
Kanisa limepoteza Imani hivyo wanavuna walichopanda.

Tunasahau hata wimbi la Kwanza hatukulishinda kwa nguvu zetu.

Petro alianza kuzama majini baada ya kupoteza imani.
Huyo petro wenu yupi wa Waafrika au wa wazungu? Nyote mnaojifanya sijui petro,yesu'n.k mtakiona cha moto kwani Mwenyezi Mungu hajaribiwi.

Rudini kwenye mila zenu kwani kusali mlikopandikizwa na wazungu hakuna maana tena bali hata wao walikuwa wanaabudu miungu wao.

Badilikeni!!
 
Kanisa limepoteza Imani hivyo wanavuna walichopanda.

Tunasahau hata wimbi la Kwanza hatukulishinda kwa nguvu zetu.

Petro alianza kuzama majini baada ya kupoteza imani.
Hatukuvuka kwa imani tu. tulivuka kwa imani na matendo. imani bila matendo ni imani mfu. Kanisa halijapoteza iman,ila limeruhusu madhabahu kunajisiwa na wanasiasa.

Wanasiasa ni wataalam wa ku twist uwongo ukaonekana ukweli. kanisa lilikosea lilipomruhusu mwana siasa kupanda madhabahuni
 
Shetani akapewa nafasi ya kuwarubuni watu wa Mungu leo ni kilio na kusaga meno! Uongo ukatamalaki, taifa likahadaiwa - HAKUNA CORONA! Yamfaa mpotoshaji yule afungiwe jiwe la kusaga na kutupwa baharini sio kwa upotoshaji ule tena madhabahuni!

Mtakatifu Luka (mwinjili) alikuwa tabibu; huduma za kitabibu sio za jana wala juzi; zipo toka mwanzo wa uwepo wa mwanadamu. Ni huduma zilizo na kibali mbele za Mungu kama zilivyo huduma nyingine nyingi!

Leo hii wanatokea wachache miongoni mwetu kuzifanya zionekane si chochote si lolote ili kulinda heshima zao kwa kauli zao tata kwa gharama ya maisha ya wananchi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…