Kanisa Katoliki lapoteza Mapadri 25 na Watawa 60 kwa tatizo la upumuaji ndani ya miezi miwili

Kanisa Katoliki lapoteza Mapadri 25 na Watawa 60 kwa tatizo la upumuaji ndani ya miezi miwili

Baada ya kutotangaza hawajafa?
Pamoja na kukuelewa..., ngoja nitumie muda mchache leo nawe hapa:

Unasema Marekani nako wamekufa..., unajua kwamba hata wao ugonjwa ulipoingia hawakuchukua tahadhari ipasavyo?

Unamkumbuka Trump? Unakumbuka yeye msimamo wake na kundi la watu wake hapo mwanzo kabla ya akili kuwaingia kichwani?

Unajua kwamba vingi vya vifo hivyo nusu million ni matokeo ya uzembe ule?

Nilishakupa mfano mzuri humu humu JF, lakini kama kawaida ya akili zenu hamtaki kujifunza chochote hata kama hamjui lolote: Nieleze China huko pamoja na wingi wao wa watu, ni watu wangapi walishakufa kutokana na corona huko? Huwezi kulijibu hili swali.

Na sio China tu, kuna nchi nyingi sana ambazo zimechukua tahadhari na kufuata taratibu zinazojulikana za kukabiliana na janga la magonjwa ya mlipuko kama huu, na wamefanikiwa kuokoa maisha ya raia zao kwa kiasi kikubwa.

Muda si mrefu, hata Rwanda na Uganda na Kenya watakuwa na matokeo ya juhudi walizofanya, huku sisi tukielekea upande tofauti.

Wewe na YEHODA, si kwa mapenzi yenu kwa mtu mnayempigania hapa. Juhudi hizi ni juu ya matumbo yenu kwa mshahara wa mauti ya waTanzania wenzenu.
 
Ningemwelewa huyo m-tec kama angetoa tamko la kufungwa kwa ibada zote kanisa katoliki tanzania; na kuhakikisha sheria, kanuni na taratibu wanafuata kivitendo na kuacha kupayukapayuka kwenye vyombo vya habari na mitandao ya jamii kushindana muumini wake hadharani !
So, ibada za madhehebu mengine zisifungwe kwasababu wao hawafi au?

Sent from my TECNO BC1 using JamiiForums mobile app
 
Kanisa limepoteza Imani hivyo wanavuna walichopanda.

Tunasahau hata wimbi la Kwanza hatukulishinda kwa nguvu zetu.

Petro alianza kuzama majini baada ya kupoteza imani.
Kweli kabisa...nawashangaa ata wizara ya Afya kuwapa watoto wetu dawa za minyoo,pepo punda na net za kuzuia mbu...Wakati wanajua fika sisi tunasali
 
Hivi tukiacha siasa kati ya nyungu na madawa ya mabeberu kipi ni bora zaidi.
 
Mambo mengine ni foolishness tupuu, sasa watu kufa kuna shida gani? Imeanza leo? Hilo tamko ni la kiibilisi
 
Hakupaswa kutoa hizi takwimu, siyo wajibu wake, amesababisha hofu na taharuki isiyo na sababu! Ashitakiwe kwa mujibu wa Sheria ya takwimu!! Yeye angetahadharisha tu! Hawa maaskofu na mapadri wakiheshimiwa wasidhani kuwa wako juu ya Sheria!!
Amesababisha hofu na taharuki ? mbona mna ovarrate sana hiyo kitu.
mtu akisema ukweli ni hoffu na taharuki. kqa taarifa yako tu ni habari ya kawaida.. hamna mtu ana hoffu wala taaruki.
acha kulazimishia watu mambo wasiyoyawaza
 
Kati ya hao Mapdre 25, mmoja Ni kaka yangu baba mmoja mama mmoja. Rest in Peace Our first Born.
Msg zako za Whasap nazisoma Sana naona kama upo hai brother![emoji24][emoji24]
Pole sana [emoji24]
 
Pamoja na kukuelewa..., ngoja nitumie muda mchache leo nawe hapa:

Unasema Marekani nako wamekufa..., unajua kwamba hata wao ugonjwa ulipoingia hawakuchukua tahadhari ipasavyo?

Unamkumbuka Trump? Unakumbuka yeye msimamo wake na kundi la watu wake hapo mwanzo kabla ya akili kuwaingia kichwani?

Unajua kwamba vingi vya vifo hivyo nusu million ni matokeo ya uzembe ule?

Nilishakupa mfano mzuri humu humu JF, lakini kama kawaida ya akili zenu hamtaki kujifunza chochote hata kama hamjui lolote: Nieleze China huko pamoja na wingi wao wa watu, ni watu wangapi walishakufa kutokana na corona huko? Huwezi kulijibu hili swali.

Na sio China tu, kuna nchi nyingi sana ambazo zimechukua tahadhari na kufuata taratibu zinazojulikana za kukabiliana na janga la magonjwa ya mlipuko kama huu, na wamefanikiwa kuokoa maisha ya raia zao kwa kiasi kikubwa.

Muda si mrefu, hata Rwanda na Uganda na Kenya watakuwa na matokeo ya juhudi walizofanya, huku sisi tukielekea upande tofauti.

Wewe na YEHODA, si kwa mapenzi yenu kwa mtu mnayempigania hapa. Juhudi hizi ni juu ya matumbo yenu kwa mshahara wa mauti ya waTanzania wenzenu.
Sasa hili povu lote mkuu ili nini?

Kwa maana hiyo nchi zote basi zinapaswa kulaumu viongozi wao maana kila nchi wamekufa kwa maelfu,!

Hivi sisi na Kenya na Uganda tuna tofauti gani?
 
Kanisa limepoteza Imani hivyo wanavuna walichopanda.

Tunasahau hata wimbi la Kwanza hatukulishinda kwa nguvu zetu.

Petro alianza kuzama majini baada ya kupoteza imani.
Kabisa, umeongea jambo la imani kubwa sana! Nakuunga mkono!

Lakini mimi naona twende mbali zaidi!

Mimi naona hata Hospitali zilizopo zigeuzwe nyumba za maombi, ndipo Mungu ataona imani yetu ni kubwa!

Kwa imani hiyo malaria nayo itatoweka, kansa itatoweka, kisukari pia kitatoweka, magonjwa ya moyo yote yataisha, na magonjwa yooote kabisa!

Hii itaokoa gharama nyingi, na itapelekea Wizara ya afya ivunjwe, na watendaji wake wote wahamie kwenye maombi, kuanzia Waziri, Katibu Mkuu, maRMO na maDMO n.k.

Tutaidhihirishia dunia kuwa kiongozi wetu ni mcha Mungu, ni mtu wa imani kubwa kuliko hata viongozi wa dini!
 
Hadi leo Vatican hakuna mtu aliyepoteza maisha tangu Corona ibishe hodi pale.
Takwimu zinaonyesha kuwa walikuwa na maambukizi ya watu 27 wakapona 15 na 12 bado hawajapona.
Wao walifunga ibada kabisa na kujifungia ndani na hata hivyo kuna mapadri kibao walikufa usitake kudanganya watu hapa
 
Mambo mengine ni foolishness tupuu, sasa watu kufa kuna shida gani? Imeanza leo? Hilo tamko ni la kiibilisi
Huyu Padri na wenzake, walipaswa kumfuata mtume Paulo kama alivyomfuta Kristo[1cor11:1 Kjv bible]; siyo kuacha kuoa au kuolewa tu ❗
Hizi ni nyakati za mwisho wa dunia na unabii unaendelea kutimia.
ASOMAYE NA AFAHAMU
⁉️
 
Vita ya Corona ni ngumu ila kama Tz watu wamejiachia sana,mwanzo kulikuwa na tahadhari kila mtu alikuwa mlinzi wa mwenzake ila tangu matamko yalipoanza kuwa maombi yameiondoa Covid ,kila mtu akaacha kufuata kanuni za kujikinga......daladala zinajaa.....kila kitu kipo kawaida tu......
 
Huyu Padri na wenzake, walipaswa kumfuata mtume Paulo kama alivyomfuta Kristo[1cor11:1 Kjv bible]; siyo kuacha kuoa au kuolewa tu [emoji779]
Hizi ni nyakati za mwisho wa dunia na unabii unaendelea kutimia.
ASOMAYE NA AFAHAMU
[emoji3480]
Fungua thread mpya kwa ajili ya mada hiyo tofauti
 
Ni ajabu kulaumiana kwa vifo vya watawa huku historia ya Rome 2020 ikijulikana. Kwangu mimi kila mtu anatakiwa kuchukua tahadhari, kula vizuri, mazoezi na kumwomba Mungu sana
Wacha uwongo.....kumwomba Mungu siyo tahadhari
 
Ni janga kubwa

Tatizo ni kuwa kuna huyu jamaa asiyetaka kufahamu kuwa tuna janga.

IMG_20210214_214251_251.jpg

Matokeo yake ndiyo huu mkururo wa matatizo unaotufuata.

Kukataa na kupotosha kuhusu chanjo ni moja tu.
 
Ni ajabu kulaumiana kwa vifo vya watawa huku historia ya Rome 2020 ikijulikana. Kwangu mimi kila mtu anatakiwa kuchukua tahadhari, kula vizuri, mazoezi na kumwomba Mungu sana

Lini tutakuwa objective na kuacha hii mambo ya kudanganyana kama watoto wadogo?

IMG_20210214_214251_251.jpg

Hivi serikali inajua kuwa tuna janga?
 
Povu lote hili ni kwa sababu tu padri kasema corona ipo na imeua watumishi wake kibao? Ama unachuki nyingine na padri wetu
Akuna cha povu hapa,huyu padre ni mwoga tu,kila siku wanatuubiria uzima wa milele,leo kafa mapadre 20 tu anatokwa na povu eti serikali ichukue atua, anataka hatua gani wakati corona aina dawa,huyu padre ni wakala wa shetani tu.
 
Kanisa limepoteza Imani hivyo wanavuna walichopanda.

Tunasahau hata wimbi la Kwanza hatukulishinda kwa nguvu zetu.

Petro alianza kuzama majini baada ya kupoteza imani.
Sasa kutahadharisha watu wajikinge na ugonjwa ndio imani imepotea hivi watu wengine kichwani kuna ubongo au mliwekewa kitu gani??
 
Padri nae anaogopa kusema kuwa wamekufa kwa Corona? Anasema changamoto ya upumuaji halafu mwisho anasema Corona ipo!
Ni kitu kile kile. Jina la kitaalamu wa huu ugonjwa ni Severe Acute Respiratory Syndrome
( SARS-CoV-2).

Kifupi ni Changamoto kubwa za kupumua zinazosabishwa na kirusi cha korona cha pili. Wako kama saba hivi.

WHO wakasema wananchi/ Dunia hawataelewa vizuri kwa hiyo tufupishe tuuite. Covid -19, au Corona ili iwe rahisi kueleweka.

Kwahiyo akisema changamoto za kupumua na baadaye akasema Corona ipo hajakosea.
 
Ni upumbavu wa hali ya juu kumtaka Mungu akulinde huku wewe hufanyi chochote.

Hutaki kufunga mlango, halafu unaamini hakuna jambazi atakayeingia, huo ni ukichaa.

Tuondoe ujinga, tuondoe woga, yaani unaona unapotezwa, halafu inabaki unasema tupotee tu kwa vile kiongozi anataka tupotee. Kuwa Rais haaanishi kuwa sahihi wakati wote, kuwa Rais haimaanishi kuwa na akili na ufahamu kuwazidi raia wote. Tusikubali kuwa mizoga inayoweza kusogezwa na kiumbe chochote kilicho hai.
 
Back
Top Bottom