KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Pamoja na kukuelewa..., ngoja nitumie muda mchache leo nawe hapa:Baada ya kutotangaza hawajafa?
Unasema Marekani nako wamekufa..., unajua kwamba hata wao ugonjwa ulipoingia hawakuchukua tahadhari ipasavyo?
Unamkumbuka Trump? Unakumbuka yeye msimamo wake na kundi la watu wake hapo mwanzo kabla ya akili kuwaingia kichwani?
Unajua kwamba vingi vya vifo hivyo nusu million ni matokeo ya uzembe ule?
Nilishakupa mfano mzuri humu humu JF, lakini kama kawaida ya akili zenu hamtaki kujifunza chochote hata kama hamjui lolote: Nieleze China huko pamoja na wingi wao wa watu, ni watu wangapi walishakufa kutokana na corona huko? Huwezi kulijibu hili swali.
Na sio China tu, kuna nchi nyingi sana ambazo zimechukua tahadhari na kufuata taratibu zinazojulikana za kukabiliana na janga la magonjwa ya mlipuko kama huu, na wamefanikiwa kuokoa maisha ya raia zao kwa kiasi kikubwa.
Muda si mrefu, hata Rwanda na Uganda na Kenya watakuwa na matokeo ya juhudi walizofanya, huku sisi tukielekea upande tofauti.
Wewe na YEHODA, si kwa mapenzi yenu kwa mtu mnayempigania hapa. Juhudi hizi ni juu ya matumbo yenu kwa mshahara wa mauti ya waTanzania wenzenu.