Ametueleza kuwa corona ipo na inaua. Sijajua sijui mtanzania gani hajui Kama corona ipo. Hata huku shamba tunajua.
Ametueleza Mapadri 25 na Watawa 60 wamekufa kwa corona ndani ya siku 60. Ninadhani ameisaidia Serikali kupata data ijapo sijajua Kama Mapadri wako juu ya sheria ya Takwimu. Ninadhani si sahihi kwake kama muumini anayesimamia haki. Ninadhani aisaidie serikali kupata majina na mahali walipofia hao ndugu ili serikali iweke kwenye kumbukumbu.
Kituko cha huyu Katibu kilichonifanya nihisi Kama anatumika kuleta taharuki ni pale kuonyesha kuwa wao wanajikinga. Lakini yupo kwenye camera hana Barakoa wala sanitizer. Lakini anatumia mike ambazo hata hajui zimetoka wapi. Nimejiuliza hivi yupo serious kwenye vita hii au naye anaigiza ili mradi tu wanaotoa misaada huko waseme kasema? Ninadhani ili kuonyesha u serious tungemuona yeye mwenyewe kavaa barakoa, Ana special mike n.k Lakini kwa mtiririko ninaona ni maigizo kutumia vifo kujinufaisha.
Na kuhusu kinga wanashindwa kututhibitishia kisayansi kuwa huko wanakopewa hizo chanjo vifo vimeisha au vimepungua? Kama bado wanakufa sisi chanjo inatusaidia nini? Uganda wapo lockdown toka mwaka jana wameokoa nini zaidi ya kujitengenezea umasikini?
Tuendelee kuchukua tahadhari za kujilinda na korona, tuache kutishishiana na kuleteana woga. Mungu atatuvusha hata Kama wachungaji wata surrender. Madam Rais alishasema hakuna lockdown Mapadri hawana uwezo wa kutu lockdown. Wakati wa kufa ukifika tutakufa, Lakini ha tutakufa kinyonge, tutakufa tungali tunapambana na kazi za kusaka mkate wa kila siku.
Huwezi kutufundisha kujikinga na corona wakati wewe mwenyewe umeshindwa kuonyesha demonstration kwenye press. Huna Barakoa, huna sanitizer na unatumia mike ambazo hujui zimetoka wapi, ni UHUNI.