PostGE2025 Kanisa Katoliki limetoa maagizo ya tangazo la misa ya kuwaombea watu waliouawa 29 Oktoba 2025

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Kwanini una ROHO MBAYA SANA?Kweli katika hili la kuombea wafu nalo una leta siasa ?
kulikoni hapakuwepo ibada za wafu wa mv bukoba, mv liemba, ajali ya treni dodoma, ajali za ndege, na wafu wa ajali mbalimbali za barabarani, ajali za moto na hata wafu waliofia mahospitali kwa maradhi mbalimbali kama sio unafiki tu wa tec wa gentleman.

au hao sio wafu? :NoGodNo:
 
Waimba Samia must go Aleluyaaaaa
Wamejichokea kwasasa
Nasisi tunawatakiwa maombi yenye Amani Misa yao !

RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN anapendwa sana ndio

Siku wananchi wakitaka kufanya Maandamano ya kumuunga mkono ndio wangeelewa somo

Kwanini project ya Samia must go Aleluyaaaaa imeshindwaa

Wao wenye kumchukia ni Genge dogo sana
lkn wanajipa umuhimu
mkubwaaa kwa kelele mitandaoni!!!

Lau ingekuwa RAIS Dkt Samia Suluhu Hassan yupo kwenye kinyang'anyiro cha Uchaguzi wa 2030-2035

haaaa tungewapa ladha chungu ya Maandamano ya kumuunga mkono jiji zima lingezizima hili Watu wakose pakuweka mguu wake!!

Wale kondoo waliopotea wenye kuyumba yumba na kuimbishwa Samia must go Aleluyaaaaa

wangejifisha kwa aibu uvunguni kuogopa iyoo nyomii tu. ✍️
 
Mbona watu wanalishupalia kanakwamba Kanisa limekosea sana?. Ni kawaida ya kanisa hili kuwa na ibada hizi
 
Mikusanyiko yao watangulize Amani mbele
wasije kujichanganya na kuimbishwa tena Samia must go Aleluyaaaaa Samia must go Aleluyaaaaa🤠
mana viongozi wao wanawaona kama matoi sijui !!

Watakimbizana mitaani wasijue njia za kutokea kwenda kwao✍️
 
kulikoni hapakuwepo ibada za wafu wa mv bukoba, mv liemba, ajali ya treni dodoma, ajali za ndege, na wafu wa ajali mbalimbali za barabarani, ajali za moto na hata wafu waliofia mahospitali kwa maradhi mbalimbali kama sio unafiki tu wa tec wa gentleman.

au hao sio wafu? :NoGodNo:
Fanya tafiti, wakatoliki wanafanya misa za kumbukumbu za maafa kila mwaka, wana hadi tarehe maalum.
 
Mbona watu wanalishupalia kanakwamba Kanisa limekosea sana?. Ni kawaida ya kanisa hili kuwa na ibada hizi

Wapi wanajua wao ndio sehemu ya tatizo mpaka kutokea Mo29

wanazuga japo kufunika kombe kupoza waliopotelewa na wapendwa wao!

Walisakizwa kikondoo na kuimbishwa Samia must go Aleluyaaaaa Samia must go Aleluyaaaaa

Wakapokewa na Aleluyaaaaa chap :FeelsStrongJAM:☠️
 
Fanya tafiti, wakatoliki wanafanya misa za kumbukumbu za maafa kila mwaka, wana hadi tarehe maalum.
Gentleman,
mwaka huu wamefanya au hawajafanya? Na hufanyika lini ibada hiyo ya wafu kwenye tarehe hiyo maalumu?

na huu unaofanyika sasa sio unafiki?:1Head:
 
Misa nchi zima, Kanisa limeagiza Kesho watangaziwe kwenye jumuiya ndogo ndogo, jumapili tutangaze kanisani, na wiki yote inayofuata Itakuwa ya kutangaziana.

======

Mwadhama Kardinali,

Wahashamu Maaskofu Wakuu,

Wahashamu Maaskofu.

Bwana Awape Amani!

YAH: WITO WA KUADHIMISHA MISA TAKATIFU KWA NIA YA KUOMBEA MAREHEMU NA WAATHIRIKA WA MATUKIO YA UCHAGUZI MKUU SIKU YA TAREHE 29 ОКТОВА 2025​

Kwa moyo wa kichungaji na kwa kutambua wajibu wetu wa kuliongoza Taifa la Mungu katika ukweli, haki upendo na mwanga wa Injili. Kwa barua hii nawaalika kuadhimisha Misa Takatifu kwa ajili ya kuliombea Taifa letu la Tanzania na sisi wenyewe. Katika kutimiza mwaka. moja tangu uchaguzi wa mwaka jana, tunakumbuka baadhi ya watu wetu kuumizwa, kupotea na hata kuuawa. Hali hiyo ya maumivu na msiba bado ipo kati ya watu wetu.

Katika mazingira haya, tunaitwa kusimama pamoja kama jumuiya ya waamini, tukimkabidhi Mwenyezi Mungu mwenye huruma Taifa letu, viongozi na watu wake. Tukiomba umoja, upendo, ukweli, mshikamano ambavyo ni matunda ya haki na amani. Kwa sauti ya upole, unyenyekevu, unyofu na majuto tuombe faraja kwa wanaolia, tumaini kwa waliokata tamaa, imani kwa wenye mahangaiko, haki na ukweli kwa waliopotea, busara kwa wasioelewa, uponyaji kwa wenye majeraha na upendo kwa wenye chuki. Pia huruma ya Mungu kwa wale waliotangulia mbele ya yake.

Tunaomba Misa Takatifu ziadhimishwe kwa nia hizo; walioumizwa, kupotea, kuuawa na kuliombea Taifa letu. Tunashauri Misa hiyo ifanyike katika Parokia, vituo vya sala na Taasisi za Kanisa kadiri iwezekanavyo siku ya Alhamisi 29 Oktoba 2026. Misa inaweza kufanyika asubuhi muda wa kawaida, au muda wowote unaofaa. Masomo ya siku au ya kuchagua yanaweza kutumika kwenye Misa hiyo.

Tukizidi kuliombea Taifa letu, naendelea kumshukuru Mungu kwa kila moja wenu kwa upendo, uelewa, ushirikiano na majitoleo yenu yasiyokoma.

Katika utumishi, upendo na ukweli,

+ Wolfgang Pisa, OFMCap

Askofu wa Lindi na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC)
View attachment 3697014
 
Attachments

  • aab1760f323876d9b25527ab3d5bda1e_1792904137725.mp4
    4.6 MB
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ipo macho sio MISA tu mkipenda zaidi njooni kitaaaa :worryStick:
 
Gentleman,
mwaka huu wamefanya au hawajafanya? Na hufanyika lini ibada hiyo ya wafu kwenye tarehe hiyo maalumu?

na huu unaofanyika sasa sio unafiki?:1Head:
Ni utaratibu wao kuwakumbuka na kuombea marehemu, sio hapa nchini tu, encyclopedia yao inaelekeza hivyo.

mimi sikatai ikiwa huo ni utaratibu wa kanisa katoliki,
hoja yangu ni kwamba, wafu wa ajali ya MV BUKOBA, wafu wa MV NYERERE, wafu wa ajali ya Treni dodoma, albino alieuawa na padre wa kikatoliki kwa sababu za kishirikina na wafu wengine hawana maana, ila hao wa october mwaka jana?

au hao hawana muombezi na hawana kiki za kisiasa wala hawaatract public symapathy?

mbona ni unafiki wa wazi kabisa gentleman? :NoGodNo:
 
Na ndo nikakujibu waliwakumbuka na wanaendelea kuwakumbuka, wana misa nadhani kila March na Mei 21, nimeuliza pia kwa mkatoliki mwingine anasema na October Kuna parokia wamekuwa na hizi misa za kuwakumbuka marehemu wa maafa. Hichi unachokitumia kama rejea ya kumbukumbu ya marehemu sio sahihi.
 
kwahiyo huo unafiki wa misa uliotangazwa na pisa ni wa parokia gani gentleman? :NoGodNo:
 
Pale Uganda Wafuasi wa kibweteere walikufa mia900 kwa kuchoma MOTO :FIRE: Kanisani na Mchungaji Joseph kibweteere mwenyewe
Joseph kibweteere kafungwaa maisha gerezani,

Kenya napo wafuasi wa Paul Makenzie kawaua njaaa kwa kuwaaminisha waumini wake wafuasi wake watapokewa na Aleluyaaaaa YESU mwenyewe na kwamba Aleluyaaaaa
anawasubili kwa
hamu kubwa:FeelsStrongJAM:☠️ Wafuasi wakajaaa wakafa kibwena kikondoo kondoo ☠️ Paul Makenzie yupo Mahakamani bado mana yupo na kesi nyingi ❗

Tanzania Kanisa letu la katoliki linabeba dhambi za Vifo vya Mo29

Wakisema kwani wao ndio wameuwa!!!!
Hata Mchungaji Joseph kibweteere kasema ivyo mimi sijauwa wamekufa kwa MOTO :FIRE:
Lkn Mahakamani wakaona chanzo ni wewe Mchungaji Joseph kibweteere
Kafungwaa maisha gerezani

Na Mchungaji Paul Makenzie nayeye juzi kasemaje mimi sijauwa wamekufa wenyewe kwa njaaa kwa hiyari yao 😳 Napo Mahakama wamemuona chanzo ni yeye wamemuhukumu kesi ya kwanza

Kanisa Kotoliki ni chanzo cha wimbo wa Samia must go Aleluyaaaaa chanzo cha kuhamisha watu wasiende kupiga kura kwenye Uchaguzi wa October 2025
Na wakasema watafanya migomo ya kukataa kwenda kupiga kura kwa njia mbali mbali

Leo kusema sisi hatukupiga risasi kuuwa mtu

Lkn watu waliopigwa risasi wamechochewa nanani kwenda kuvamia miundombinu mbali mbali Wachochezi ndio wanawajibika ktk hili

Kanisa Kotoliki wanapaswa kuomba radhi Watanzania
Matendo yake yameingiza Taifa kwenye Janga kubwa la kupoteza Watoto wetu ✍️
 
kwahiyo huo unafiki wa misa uliotangazwa na pisa ni wa parokia gani gentleman? :NoGodNo:
Kwanza acknowledge kuwa kusema marehemu wa majanga ya nyuma hawakumbukwi si sahihi ndo tuhamie kwenye hoja ya misa unayoiita unafiki. Reputation ya mjadala inajengwa na kukubali kukosea iwapo kuna makosa. Kama mjadala hauna usahihishaji wa makosa hakuna haja ya kuendelea kuuita mjadala.
 
Misa nchi zima, Kanisa limeagiza Kesho watangaziwe kwenye jumuiya ndogo ndogo, jumapili tutangaze kanisani, na wiki yote inayofuata Itakuwa ya kutangaziana.

======

Mwadhama Kardinali,

Wahashamu Maaskofu Wakuu,

Wahashamu Maaskofu.

Bwana Awape Amani!

YAH: WITO WA KUADHIMISHA MISA TAKATIFU KWA NIA YA KUOMBEA MAREHEMU NA WAATHIRIKA WA MATUKIO YA UCHAGUZI MKUU SIKU YA TAREHE 29 ОКТОВА 2025​

Kwa moyo wa kichungaji na kwa kutambua wajibu wetu wa kuliongoza Taifa la Mungu katika ukweli, haki upendo na mwanga wa Injili. Kwa barua hii nawaalika kuadhimisha Misa Takatifu kwa ajili ya kuliombea Taifa letu la Tanzania na sisi wenyewe. Katika kutimiza mwaka. moja tangu uchaguzi wa mwaka jana, tunakumbuka baadhi ya watu wetu kuumizwa, kupotea na hata kuuawa. Hali hiyo ya maumivu na msiba bado ipo kati ya watu wetu.

Katika mazingira haya, tunaitwa kusimama pamoja kama jumuiya ya waamini, tukimkabidhi Mwenyezi Mungu mwenye huruma Taifa letu, viongozi na watu wake. Tukiomba umoja, upendo, ukweli, mshikamano ambavyo ni matunda ya haki na amani. Kwa sauti ya upole, unyenyekevu, unyofu na majuto tuombe faraja kwa wanaolia, tumaini kwa waliokata tamaa, imani kwa wenye mahangaiko, haki na ukweli kwa waliopotea, busara kwa wasioelewa, uponyaji kwa wenye majeraha na upendo kwa wenye chuki. Pia huruma ya Mungu kwa wale waliotangulia mbele ya yake.

Tunaomba Misa Takatifu ziadhimishwe kwa nia hizo; walioumizwa, kupotea, kuuawa na kuliombea Taifa letu. Tunashauri Misa hiyo ifanyike katika Parokia, vituo vya sala na Taasisi za Kanisa kadiri iwezekanavyo siku ya Alhamisi 29 Oktoba 2026. Misa inaweza kufanyika asubuhi muda wa kawaida, au muda wowote unaofaa. Masomo ya siku au ya kuchagua yanaweza kutumika kwenye Misa hiyo.

Tukizidi kuliombea Taifa letu, naendelea kumshukuru Mungu kwa kila moja wenu kwa upendo, uelewa, ushirikiano na majitoleo yenu yasiyokoma.

Katika utumishi, upendo na ukweli,

+ Wolfgang Pisa, OFMCap

Askofu wa Lindi na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC)
View attachment 3697014
Huu uzi huwezi kuwaona chawa wa Serikali haramu.
 
Back
Top Bottom