Kanisa Katoliki mje hapa, maana nimesema kwenye vikao hamfanyi

Kanisa Katoliki mje hapa, maana nimesema kwenye vikao hamfanyi

Hakuna anayejali

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2023
Posts
418
Reaction score
526
Mimi ni muumini wa kanisa tajwa hapo juu, nimekuwa kiongozi wa jumuia kwa kipindi fulani, niliwahi kumfata paroko kishauriana naye mambo kadhaa, na pia kwenye vikao vya kamati tendaji ya kigango nilishauri kukiwa na msiba sadaka ikusanywe mara moja tu.

Kukusanya sadaka mara 2 ule utaratibu unawakwaza watu hata kama hawasemi kwakuwa si eneo la kuhoji bali mazishi pili hata ile sadaka inayokusanywa nilishauri wapewe wafiwa Mana kwa siku2-3 hawatazalisha iwasaidiye.

Kwanini mnachukuwa kuondoka nayo na kusema kuwa itasomewa misa ya marehemu kwani lazima muwasomee? Kusoma kwenyewe mnasema tu ktk misa hii tuungane na familia ya mr Kago anamuombea mr Blue Kago imeisha hiyo.

Nasisitiza suala la kuombea marehemu waachiwe wanafamilia wapange na watafanya misa kubwa maalum.
 
kusoma kwenyewe mnasema tu ktk misa hii tuungane na familia ya mr Kago anamuombea mr Blue Kago imeisha hiyo.
Unataka wamwombeeje?

Nia za misa zote huwekwa wazi mwanzoni mwa adhimisho la Misa na wakati wa Konsekrasio (japo siyo kwa ulazima).

Kuhusu matumizi ya sadaka; ni utaratibu wa Kanisa Mahalia husika. Siyo universal. Halafu kwani wafiwa hamwapi rambirambi hadi wategemee sadaka?
 
Bado hujakua kiimani una imani haba halafu unajitamba wewe kiongozi wa Jumuiya nahisi wewe ndio wale utakua unawaambia unaowaongoza wasichange michango kisa anakula baba padre.

Sasa umeyaleta humu Paroko wako ndio yupo huku.nina mashaka unaweza kuwa hata sio Mromani wewe.

Vipi hiyo Sadaka mnatoa Milioni 50 nini umeshawahi changia mafuta ya gari la Baba Padri, umeshawahi nunua hata Ciborium moja, umeshawahi saidia hata mshumaa mmoja tu au kitambaa cha misa.

Nakushauri tumia hekima na omba hekima zaidi kama Selemani
 
Tuanzie kwanza kujua hiyo sadaka inakusanywa bei gani?kisha tuichanganue kwamba imetumika vipi kwa mifano tu lakini

Ili Padre afike hapo msibani alikuja na gari,gari si inatumia mafuta?wewe mleta mada unadhani zile sadaka huwa zinafika bei gani hata tuanze kukazia kuzidai?(kama kweli ni Mkatoliki) unaujua umuhimu wa marehemu kuombewa misa?unajua kwanini bila kujali imepatikana kiasi gani ni lazima sadaka hii iwe ni kwa ajili ya misa ya marehemu huyu tu?
 
Wanakosea sana,sadaka wagawane na wafiwa,btw mchungaji hula kondoo na kondoo hula nyasi[emoji28]
Wanakosea kwa kwa amri ya nani?

Hii sadaka huhesabiwa kama maalumu kwa ajili ya marehemu aliyezikwa sababu huchukuliwa kama ni sala za hadhira nzima iliyoshiriki ibada na inakuwa na kibali kwa Mungu maana imetokana na ibada ya marehemu husika iliyotolewa ktk altare ya ibada yake

Mkatoliki tu atalielewa vizuri hili
 
Skuiz kanisa langu katoliki kumekuwa na wapigaji wengi sana
Unaelewa katekisim Katoliki inasemaje kuhusu sadaka ya ibada ya marehemu?

Kwa hiyo unataka wewe uliye hai mwenye uwezo wa kutubu ukale haki ya mtu asiyekuwa na uwezo wa kutubu ambayo ataiwakilisha kwenye kiti cha enzi cha huyo aliyemuita kupitia usingizi wa milele?kufa wewe ufanyiwe ibada upewe sadaka yako mwenyewe!
 
Unaelewa katekisim Katoliki inasemaje kuhusu sadaka ya ibada ya marehemu?

Kwa hiyo unataka wewe uliye hai mwenye uwezo wa kutubu ukale haki ya mtu asiyekuwa na uwezo wa kutubu ambayo ataiwakilisha kwenye kiti cha enzi cha huyo aliyemuita kupitia usingizi wa milele?
Acheni uhuni kanisani
 
Siku hizi hakuna misaada kutoka Vatican..yani kuna ujenzi hapa parokiania kwetu bado nadaiwa parefu na deadline tayari..ila uzuri wa kanisani wala sina hofu nitatoa pindi nikipata..
 
Siku hizi hakuna misaada kutoka Vatican..yani kuna ujenzi hapa parokiania kwetu bado nadaiwa parefu na deadline tayari..ila uzuri wa kanisani wala sina hofu nitatoa pindi nikipata..
Jumapili nilikuona kanisani🤣
 
Back
Top Bottom