Mimi ni muumini wa kanisa tajwa hapo juu, nimekuwa kiongozi wa jumuia kwa kipindi fulani, niliwahi kumfata paroko kishauriana naye mambo kadhaa, na pia kwenye vikao vya kamati tendaji ya kigango nilishauri kukiwa na msiba sadaka ikusanywe mara moja tu.
Kukusanya sadaka mara 2 ule utaratibu unawakwaza watu hata kama hawasemi kwakuwa si eneo la kuhoji bali mazishi pili hata ile sadaka inayokusanywa nilishauri wapewe wafiwa Mana kwa siku2-3 hawatazalisha iwasaidiye.
Kwanini mnachukuwa kuondoka nayo na kusema kuwa itasomewa misa ya marehemu kwani lazima muwasomee? Kusoma kwenyewe mnasema tu ktk misa hii tuungane na familia ya mr Kago anamuombea mr Blue Kago imeisha hiyo.
Nasisitiza suala la kuombea marehemu waachiwe wanafamilia wapange na watafanya misa kubwa maalum.
Aisee katubu ndugu. Kumbe ni kwaajili ya Misa mmh. Kuna kitu juu ya hizo misa za marehemu hukijui kabisa. Na umeleta huku ili watu watukane na kukufuru.
Kwanza hiyo sadaka ya pili huwa wanapata sh ngapi??
Na yote ni kutokana na ubinafsi wa wafiwa kujifikiria wao tuu, uchungu wao tuu kama ambavyo nawe umewa sapoti.. Badala ya kufikiria zaidi hali ya yule aliyeondoka, alikufaje? Alijiandaa, yupo wapi muda huo wakati watu watu wapo bize kulia lia na baadaye kugombea mirathi??
Misa hizo huwa zinasomwa misa 30 kwa siku 30 na lazima ishara kubwa itokee after that.. Kama ungeijua kwa imani maana yake aisee sijui ungeomba nawe maelfu ya misa Zisomwe kwaajili ya maelfu, kwa malaki, kama sio mamilioni ya Roho zinazoteseka mno baada ya kutelekezwa na jamaa zao waliojifanya kuwapenda sana walipokuwa hai lakini hawakuwakumbuka kuwaombea huruma ya Mungu baada ya kifo chao.
Fikiria juu ya mamilioni ya watu wasioamini juu ya huruma na rehema ya Mungu kwa marehemu, kutokana na mafundisho ya imani zao. Wote hao ni Wajibu wa Kanisa Katoliki kuwaombea hasa sisi waumini.
Kumbuka nia za kuwaombea Marehemu wanaoteseka toharani wasio na waombezi.
Ni watu wachache sana sana katika Dunia hii ngumu ambao wakifa wanaenda directly Mbinguni ni wachache mno.. Na ni watakatifu hasa na wanaokufa kishahidi kama kina Stephano..
Lakini wengi tunakufa tukiwa na mapungufu mengi mengi hata kama wengine walituona kama tuliishi kitakatifu lakini mioyo yetu kila mtu anaujua wake ulivyo, uvivu, uchoyo, tamaa, kiburi, majivuni, chuki, hasira, ulafi, uzembe, kutotimiza Wajibu, kutokuwa na huruma, ulevi, kutosaidia wenye uhitaji, kutofariji wafiwa na wenye huzuni na upweke, kutozika wafu, kijicho, ushabiki wa siasa tena chafu, kujiinua, kujiona mkamilifu, kudharau wengine, kubagua, undugunization, kutosalimia na kutowajulia hali watu, ndugu, rafiki, jirani. Umbea, usengenyaji, majungu, ubahili, kufurahia kushindwa au kuanguka kwa wengine, ujuaji, kupenda sifa badala ya kusifiwa Mungu, kusikiliza sauti mbaya iwe miziki, movie, tamthilia, vipindi, michezo, kunyima watu lifti, kutaka vizuri upate wewe tuu...
Utoaji mimba, ukosefu wa usafi wa moyo, kutovumilia mateso, manung'uniko, ulalamishi, kutosali kwa ibada na uchaji, kujifanya unaamini wakati imani yako ni haba, ku pretend ni mwema wakati sio
Na maelfu kwa maelfu ya dhambi... Kutumia vidhibiti mimba, kupandikiza watoto, malezi mabovu, kutochukua hatua
Je unadhani usipojitafiti na kujipekua ndani ya dhamiri yako utaiona mbingu??? Utaishia kuhukumu wengine tuu.
Hivyo ni lazima kuwaimbea msamaha na Huruma ya Mungu wote wanaokufa siku zote za maisha yetu maana na wao wamekufa wakiwa na mapungufu mengi kama ambavyo sisi tunayo.
Mwenyezi Mungu awahurumie, awasamehe, awatakase na kuwapokea katika utukufu wake huku wakisubiri hukumu ya mwisho ya wazima na wafu.