Kanisa Katoliki mnazingua, michango imekuwa kero

Unachofeel ni kweli, umefeel kitakatifu sana

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Lengo la kwenda mbele Kwa asiye na sadaka siyo Kumshukuru Mungu, kwani Mungu yupo kule mbele? Lengo la kupita mstari Kwa mstari ninkuakikikisha Kila mtu anatoa, na kusema Kila mtu apite mbele ni kumfanya mtu aone aibu kupita bila kutoa sadaka
 
Wakatoriki siku hz wanashindana na lutheran, Pentecost kwa wingi wa michsngo,
Makanisa ya Afrika, wachungaji wake huduma pekee wana kupa, ni "kukuombea kwa Mungu" Na maneno ya faraja tu,
Hawakujengi kisaikolojia ili upambsne zaidi, uwe tajiri,
 
Kuna Uzi niliuanzisha hapa miaka kama Minne au Mitano iliyopita Kulalamikia hili hili na kusema kuwa ndiyo limechangia si tu Kusuasua Kwangu kwenda Kanisani au hata Kuhudhuria Jumuiya ( ambako nako huko muda mwingi Watu wanaacha Kusali wanaanza Kutetana na Kupigana Majungu ) na kuamua tu Kusali kipeke yangu peke yangu Nyumbani / Chumbani Kwangu.
 
mkuu njoo jumuiyani usijitenge
 
mkuu njoo jumuiyani usijitenge
Nipo Msituni huku Porini naitengenezea Jina na Sifa Tanzania yako / yetu huko Jumuiyani Kwako nitaenda muda gani? Ninachoweza ni kila Jumapili kuhudhuria Maombi Mjini Kampala kwakuwa kila Ijumaa huwa nakuwa huko Kwangu kwa ajili ya Kupumzika ( Refreshing ) na Jumapili nageuka kuja katika Kituo changu Tukuka cha Majukumu ya kuiletea Heshima Tanzania ndani ya Uganda lakini pia Kuisaidia Uganda kwa Kazi ambayo nawafanyia ambayo nimepewa Heshima Kubwa ambayo itabakia kuwa Historia katika Maisha yangu yote.
 
Umesema vema
 
Huku kwetu Paroko alianza kutupagia kiwango kila jumuiya, tukamuitikia tu. Ikifika ktk utekelezaji tunapeleka tulichokipata kata kama 70,000. Basi anakasirika

Akaanza kufoka na kututishia kwa maandiko. Tukamwambia yeye hana majukumu, pia asitupangie ktk utoaji. Maisha ya waamini n magumu sana. Wapo wanakula milo miwili tu. Yeye hajawahi kugawa hata mche wa sabuni kwa kaya maskini.

Sisi tumeamua kutoa sadaka, zaka na mavuno basi. Tena kila mmoja kuamua si kumpangia ktk utoaji.

Katika kikao cha halmashauri Paroko alipewa ukweli tu, ajue pia hali ya kiimani ya waamini wake kama anavyojua kaya zisizotoa michango.

Wakatoliki ifike wakati tauche unafiki wa kufukia makosa. Tuache yasemwe turekebishe. Jamaa amesema baadhi wanamwandama kwa maneno makali. Sio namna nzuri ya kutatua ama kutetea taasisi.
 
Jombaa hivi ukipiga mahesabu ya matumizi yako ya mwaka mzima na sadaka ulizo mtolea Mungu Mzani wako Unaelemea wapi?

Sasa Kama mzani wako unaelemea kwenye matumizi basi kwa Mungu wewe ni Mwizi Na huna faida kwenye Ufalme wa Mungu Mjomba.

Hivi kama Unaakili timamu Mungu Anakupa Uzima, anakulinda, anakupa BARAKA za kupata hiyo fedha unayo bwabwaja unapata uchungu kumtolea?

Jitafakarini sana kama sadaka zako kwa mwaka hazifiki 1M Na Unakipato kizuri jitafakari Na Utubu kwa Mungu Mjomba.
 
It's as simple as this. Unacho, toa "kadiri unavyoweza". Huna, huko kukosa ndiyo matoleo yako na Mungu anayapokea pia kwa sababu "anaona hadi moyoni mwako." Kwa hiyo, shida iko wapi, kwako au kwa kanisa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…