Ngungenge
JF-Expert Member
- Jun 11, 2016
- 2,914
- 3,386
Kwa heshima na unyenyekevu mkubwa, nitoe Rai kwa Kanisa Katoliki ambalo ni kanisa Mama na lenye mchango wa kipekee kwa hili Taifa tangu uhuru mpaka sasa.
Sisi waumini na wananchi kwa ujumla tunaona ufinyu wa nafasi yenu katika kuunga mkono serikali ya Rais Samia tofauti na serikali iliyopita. Je, ni kwa sababu Rais Magufuli alikuwa Mkristu? Je, ni sababu Rais Samia ni Muislamu.
Metendo yenu yawe sawa kwa watu wote na tusibague kwa kuwa huyu sio wa kwetu la hasha tutakua tunatenda dhambi.
Mama huyu mnyenyekevu sana na mwenye hofu ya Mungu na heshima kwa Viongozi wa dini na wazee, wakati wote amejiepusha na ubaguzi wa kidini na kutoa upendeleo sawa kwa madhehebu yote ya dini bila kubagua.
Katika Jambo lolote ameshirikisha madhehebu yote na kuwapa uzito sawa. Ni kweli suala la bandari linahitaji maboresho lakini sio kupinga moja kwa moja. Mathalani ishu ya ukomo wa mkatabaa ni muhimu na maeneo ya uwekezaji yanabaki mambo muhimu.
Tusisahau Rais Samia angeamua kusaini mkataba bila kuweka mkataba public je mngefanya nini. mikataba mingapi imesainiwa kimya kimya. Je kwanini huyu mama asipewe pongezi?
Huyu Mama ambaye Mungu amempa kibali mwacheni atawale kwa muda wake. Maumivu ya kanisa kwa Hayati Magufuli lazima tukubali ni mapenzi ya Mungu. Mungu ndio huamua awe hai hatakama wanadamu watahusika.
Ni nafasi yenu kurekebisha, hili Taifa linaaongozwa na Mkono wa Mungu.
AMEN