Mkuu,Kanisa ni asasi ya kiraia inayohitaji ulinzi na huduma nyingine za kiraia kama polisi, maji, umeme, barabara, usajiri, misamaha ya Kodi, ardhi, nk. Waumini ni raia pia wanaishi kwenye jamii. Huduma zote hizi zinategemea wanasiasa ili zipatikane kanisani pia.
Kupiga marufuku wanasiasa kwenda kusema chochote kanisani bila kubagua anatoka chama gani ni vita nyingine kati ya kanisa na mamlaka.
Sijui nani ataumia kama ikiwa hivi.
Mkuu,
Unaelewa kuwa hao waliokupa hizo habari za nchi, rais, bunge, mahakama, serikali wameweka kitu kinaitwa "Separation of Church and State"?
Ushawahi kusikia hiyo habari?
Mambo yetu ya uongozi, nchi, mahakama, bunge, serikali, demokrasia, etc, tumeiga.Mkuu,naomba unifafanulie hapa nielewe,sijui shida kizungu au vip?
Unamanisha nini?
Hivyo vyote ulivyotaja hapo ni hisani au ni haki ya hizo taasisi? Pia kumbuka hizo huduma zote haukuna ya bureKanisa ni asasi ya kiraia inayohitaji ulinzi na huduma nyingine za kiraia kama polisi, maji, umeme, barabara, usajiri, misamaha ya Kodi, ardhi, nk. Waumini ni raia pia wanaishi kwenye jamii. Huduma zote hizi zinategemea wanasiasa ili zipatikane kanisani pia.
Kupiga marufuku wanasiasa kwenda kusema chochote kanisani bila kubagua anatoka chama gani ni vita nyingine kati ya kanisa na mamlaka.
Sijui nani ataumia kama ikiwa hivi.
UmenenaWalichelewa sana kufanya maamuzi hayo, matokeo mazoea!
Hata mikutano ya chama/serikali salamu iwe moja tu.....Jamhuri ya Muugano wa Tanzania...Kazi iendelee...
Haya mambo ya Tumsifu Yesu Kristo; Bwana Yesu Asifiwe; Mwanakondoo Ameshinda; Asalaam Alaykhum... tuyaache makanisani au misikitini.
Mini sio mtu duni. Mtu mwenye utimamu wa akili hasumbiliwi na vitu duni. Ukiona kitu duni kinamsumbua mtu ujue yule anaesumbuka ndiye duni zaidi.Nimesoma na kuona ni uchafu/takataka; ndiyo maana nikatumia haki yangu kuyasema hayo.
Wewe ni mtu duni sana, ningejuwa kungali maema, nisingejihangaisha kuoteza muda wangu na takataka.
Kulifuta kanisa kama RC ni kazi ngumu lakini ugumu wake utatokana na aina ya kosa na ukubwa wa kosa, vinginevyo ni rahisi sana kudili na mtu mmojammoja aliyekosea. Hata watu wa dini wanazo orodha ndefu sana za watu wa wa dini waliokatwa vichwa vyao na watawala. Unapotaka kujibizana na watawala maana yake unajiandaa kupambana na watu wanaolipwa na walioapa kumtii na kumlinda mtawala kwa gharama yoyote ile hata ikibidi wao kufa. Ni mwehu tu ambae hajui hili.Serikali inaweza kuwa ni set yenye subsets nyingi ikiwemo dini.
Mbona humu kuna watu wanatishia eti serikali inaweza hata kufuta kanisa kama vile hiyo serikali inaendeshwa na maroboti?
Serikali ikisha pitishwa na watu inamilikiwa na watu. Kama haikupitishwa na watu hicho ni kitu kingine.
Sikutegemea katazo la RC dhidi ya wana siasa ambao pia wanaweza kuwa ni waumini pia kuwatatiza baadhi ya watu kiasi hicho.
Baadae nini kilitokeaNdoto za alinacha hizo, RC itabakia kwakuwa ina watu wema wengi na wenye akili, hekima na busara na sio kwasabu ina watu wengi. Kwani hakuna nchi duniani ambazo hakuna RC au uisalamu? Unadhani Magufuli alipowaita wale jamaa wa RC kuwa wanawashwawashwa na walaka wao aliupata wapi huo ujasiri?
Huko misikitini wanasiasa wanaruhusiwa kusema lolote?Wapo kwenye ushindani ndio maana watu wanasema wana muonea rais kisa dini nyingine
Waliyomfanyia Kitima akafanyiwe balozi wa Marekani pale Oyster bay afu tuone kama hii nadhari Yako ina mashikoHakuna taasisi yoyote ile humu nchini ambayo ni serikali proof au serikali resistant, Itategemea na unyeti wa jambo lenyewe.
Vipi kuhusu kuomba kura kwenye nyumba za Ibada?Kama mlawiti yumo msikitini au kanisani atafuatwa humohumo na kama mwenye dalili za ugonjwa wa ebola yumo kwenye nyumba ya ibada anasali na watu wengine atakwenda kuchomolewa humohumo kwenye safu za wanaosali, hakuna mipaka kwa serikali kama kuna jambo muhimu la nchi.
Kitima ni mtanzania tena msomi. Amani tuliyonayo Sasa haitokani na maombi yake bali mipango na mikakati ya serikali kwakutumia majeshi yetu. Asimjaribu bwana Mungu wake kucheza na vyombo vinavyomlinda.Waliyomfanyia Kitima akafanyiwe balozi wa Marekani pale Oyster bay afu tuone kama hii nadhari Yako ina mashiko
Church ni chombo cha state lakini State sio chombo cha church, hiyo unafahamu?Mkuu,
Unaelewa kuwa hao waliokupa hizo habari za nchi, rais, bunge, mahakama, serikali wameweka kitu kinaitwa "Separation of Church and State"?
Ushawahi kusikia hiyo habari?
Siongelei mambo yalivyo ki Makaveli, naongelea mambo yanavyotakiwa kuwa kisheria.Church ni chombo cha state lakini State sio chombo cha church, hiyo unafahamu?
Mkoloni alipotaka kuja kuitawala tz alilitumia kanisa kama instrument ya kurahisisha kutawala. Sasa Kuna mtu anataka kuwaaminisha watu kuwa kanisa liko huru kujifanyia na kujiamulia mwelekeo wake. Kanisa lazima liendesheshwe kwa mujibu wa sera na vision ya taifa husika.
Lile eneo la kurasini ni eneo la bandari, serikali Ina haki na mamlaka kamili ya kufura matumizi ya eneo lilipo kanisa na kupanua bandari. Au hilo hulijui nalo?
Waumini ni raia pia, wanayo haki ya kuambiwa nani anagombea ili afanye maamuzi yake hakuna atakaemlazimisha kuchagua lakini anayo haki ya kuambiwa popote plale alipo ndani ya jamhuri. Kanisa ni jengo tu lilipata kibali cha serikali lijengwe hapo. Serikali Ina wajibu kwa kanisa na kanisa Lina wajibu kwa serikali. Wajibu huo uko kwenye usajili wa kanisa .Ku
Vipi kuhusu kuomba kura kwenye nyumba za Ibada?
Kaka huo uliousema ndio ukweli wenyewe. Watu wa dini wanazo orodha ndefu za watu wao ambao walikufa kwasababu za dini. Hata Bwana Yesu alikufa kwasababu hizohizo za kuchanganya dini na siasa. Watawala hawataki kukoki kukosolewa kwa kutumia dini(ndoto, maono na mapokeo) ambayo hayana ushahidi ila kwa anaeamini tu. Maana wananchi wanataka majibu, matokeo na huduma leoleo kutoka kwa watawala wao wakati waumini hawana haraka na majibu na matokeo kutoka kwa wachungaji na Mungu.Mambo yetu ya uongozi, nchi, mahakama, bunge, serikali, demokrasia, etc, tumeiga.
Na kuiga si lazima liwe jambo baya. Hatuhitaji kuanza upya kila kitu, hususan kama kimefanyika vizuri kwingine.
Na huko tulikoiga ambapo walianza haya mambo zamani kabla yetu, walipitia matatizo nengi sana, matatizo ambayo kwa sababu wao waliyapitia, sisi tunaweza kujifunza tu kutoka kwao tusiyapitie kama wao.
Mtu mjanja mara zote hujifunza kutokana na matatizo na historia ya wengine ili yeye asiyapitie, apate somo moja kwa moja.
Wale ambao tumejifunza kwao waliuana sana, walichinjana sana, walipigana vita sana, kwa sababu ya kuchanganya dini na siasa.
Mpaka wazungu wengine wakakimbia Ulaya wakaenda kuanzisha makazi Marekani kwa sababu walibaguliwa kidini Ulaya. Walikuwa wanataka kuishi kwa uhuru wao.
Mpaka Ulaya wakapigana kitu kinaitwa "The Thirty Years War" kwa Kiswahili "Vita Vya Miaka Thelathini" ya mwaka 1618 mpaka 1648. Sababu moja kubwa ya vita hizi ilikuwa ni kuchanganya siasa na dini.
Baada ya "The Thirty Years War" walikubaliana kimkataba kutopigana vita, kila mtu akae kwake, na wajitawale kiserikali, na watweganishe dini na siasa. Hapa ndipo dhana ya nchi kama tunavyoijua leo ikaanza, kwenye mkataba ulioitwa "The Peace of Westphalia" wa mwaka 1648. Takriban miaka 377 iliyopita wenzetu walijifunza kwamba kuchanganya dini na siasa kunatengeneza sumu mbaya inayosababisha vita kubwa sana. Wakatenganisha dini na siasa.
Sasa na sisi kimsingi tumejifunza hilo. Ndiyo maana tuna katiba inayosema nchi yetu haina dini. Lakini dini ina nguvu sana tunashindwa kutekeleza Separation of State and Religion. Ni viongozi wanafalsafa tu kama Nyerere waliosoma, kuelewa na ku internalize hii historia ndio waliweza kujizuia wao wenyewe kusimama makanisani kutoa hotuba za kisiasa.
Juzi Samia kaenda kufungua kanisa la Mwamposa, kuna Babu wa Kizanzibari alikuwa analia anasema Samia kaombewa na Mwamposa kwa jina la Yesu kaondolewa kwenye Uislamu kawa Mkristo.
Hata kabla ya hapo Samia alivyokuwa anagawa sana hela makanisani, Wazanzibari kwenye misikiti walikuwa wanamsema anawapendelea sana Wakristo anawapa hela sana Wakristo, Waislamu hawamuoni. Tayari rais kujiingiza makanisani inaleta mgawanyiko kwa wananchi.
Wasio na dini naowanaona vibaya pesa zao za kodi zinatumika kwenye nyumba za dini.
Ndiyo maana wenzetu waliona matatizo haya mapema wakaweka hii Separation of State and Religion.
Nyerere alikuwa anasali pale St. Peters Oysterbay kila siku akiwa Dar. Si kila Jumapili, kila siku. Lakini hakwenda mbele pale kusema neno hata siku moja. Ilikuwa mwiko. Mkapa naye vilevile alikiwa anasali St. Immaculata hapa Upanga karibu na Selander Bridge. Hakuenda mbele kutoa neno hata siku moja.
Huu ujinga kwa Wakristo umeanza na Magufuli tu. I am not sure about Mwinyi and Kikwete.