Petro alipelekwa Rumi kwa ajili ya mashtaka ya tuhuma za uongo dhidi ya yeye ku.mkiri Kristo na kuifuata imani yake ya kweli aliyofundishwa na Bwana Yesu Kristo mwenyewe. Alihukumiwa kifo na uongozi wa Rumi ya kipagani, na kusulubishwa kichwa chini miguu juu, na hatimaye akafa kama mfia imani ya kweli ya Kristo..
Tukio hilo lilitokea karne ya kwanza ambapo taifa la Rumi lilikuwa la kipagani na makaisari wake walikuwa wapagani. Petro alikamatwa Yerusalemu akiwa mtu wa kawaida , mtume, na kiongozi, wa kundi, na wala hakuwahi kuwa na cheo chenye mamlaka makubwa ya kiserikali na kiutawala ya kipapa.
Upapa ulianzishwa karne ya tatu. Muasisi wake akiwa Kaisari Comstatino baada kuanzisha dini ya Kikristo yenye muundo wa mafundisho ya Kikristo yaliyoghoshiwa na kuchanganya yale ya kipagani yaliyokuwa yakikubalika na wengi katika Rumi ya kipagani.
Umechannganya ukweli mdogo na mengi yasiyo ya kweli.
Nikupeleke shule kidogo.
1) Kristo alianzisha Kanisa na akamteua Simon (akambadilisha jina na kumwita Petera, yaani Mwamba) kuwa kiongozi mkuu wa Kanisa hilo. Math 16:18
2) Kwa njia ya maono, Yesu alimteua Paulo kuwa mtume wa mataifa.
3) Wote wawili, Petro na Paulo walifika Rumi kwa namna ambayo hawakuipanga. Japo walienda kwa sababu ya mashtaka, lakini ikawa ndiyo njia ya kuifikisha injili Rumi ambako ilikuwa ndiyo makao makuu ya dola kuu Duniani iliyoongozwa na wapagani.
4) Siku ya kuiabudu Miungu mbalimbali, Paulo alifika kwa watu waliokuwa wanasali kwa, "Unknown God", anaanza kuwahubiria ni yupi huyo wasiyemjua. Na watu wengi wanakuja kumsikikiza, wengi wanastaajabu, habari zinamfikia mfalme, naye anagiza Paulo apelekwe kwakwe akamhubirie. Mfalme baada ya kusikikiza mahubiri, anatoa kibali cha Paulo kuendelea kueneza imani hiyo mpya, lakini mfalme anabakia na upagani wake.
5) Petro ndiye alijenga kikanisa kidogo Roma. Petro na Paulo, wote waliuawa Roma lakini wakiwa wamejipatia waamini wengi wa Kristo. Baada ya vifo vyao, ukristo unapata nguvu zaidi baada ya mfalme Costantin, yeye binafsi kumkiri Kristo. Na hivyo wakristo kusali na kuhubiri kwa uhuru.
6) Kanisa lilianza kuitwa Katoliki baada ya kikao cha kwanza cha mitume, ikimaanisha kanisa lililoenea Duniani kote. Hivyo walioifuata imani hii iliyoenea Duniani kote waliitwa wakatoliki.
7) Mgawanyiko wa kwanza wa Kanisa Katoliki ulifanywa na aliyekuwa Katibu wa papa. Alipojitenga hakuwahi kusema kuwa ananzisha kanisa jingine bali alijitenga tu na mamlaka ya Papa. Imani aliyoendelea kuihubiri ilibakia ile ile ya Katoliki. Ili kutofautisha wakatoliki wanaofuata huyu aliyejitenga na wale waliobakia chini ya mamlaka ya Papa, ndipo likazaliwa neno hilo la Wakatoliki walio chini ya Rumi, walioitwa Waktoliki wa Rumi (Roman Catholics) na wakatoliki wa kanisa la mashariki walioitwa Orthodox.
Lakini ni uwongo mkubwa kudai kuwa eti mfalme Costantin alibadilisha mambo mengi ya kiimani au ndiye aliyehamisha makao makuu ya Kanisa toka Jerusalem kwenda Rumi.
Mfalme Costantin alichosaidia ni kulipa uhuru Kanisa. Na hivyo kanisa likastawi na kupata waamini wengi Rumi kuliko kwenye mataifa mengi ambayo watawala wao hawakuwa wameupokea ukristo. Hivyo kanisa la Rumi likawa taasisi imara na kubwa kuliko mahali pengine popote.