Kihistoria petro alizunguka duniani kuhubiri kile alicho fundishwa na yesu akuwa mrumi bali ni mwisraeli na hakuanzisha ukatoliki
Petro hakufundisha mambo yake bali ushuhuda wa yesu aliyeishi nae na kula nae na kutembea nae, petro alifundisha mafundisho kutoka kwa yesu ukitaka kuujua ukweli hebu angalia mafundisho ya yesu kwenye biblia na hata film je yanafansna na ukatoliki, wapi yesu alimuomba maria, wapi mitume walimuomba marai, wapi yesu aliabudu sanamu wapi mitume waliabudu sanamu daaah kazi kweli kweli
Niwazi hakuna aliyezifanya hizi ibada na ndivyo wanavyomzushia petro kuwa ni papa kutoka Italy, wakati petro hakuwai kuwa kiongozi nje ya israeli hakuwai kuwa mfalme wala papa
Umrundika vitu vingi ambavyo vingi inaonekana huna uelewa navyo.
Kuna mtu yeyote amewahi kukuambia kuwa Petro alikuwa Mrumi? Paulo na Paulo, wote walikuwa wayahudi kiasili. Walihusishwa na Warumi kwa sababu tu Warumi waliifanya Uyahudi kuwa koloni lao.
Ungekuwa unaujua ukristo japo kidogo, ungeelewa kuwa mafundisho yote ya Kristo yalionesha jinsi Mungu alivyoyageukia mataifa baada ya Wayahudi kumkataa masiha. Na hata alipokuwa akiondoka, aliwaambia mitume, "nendeni Duniani kote mkawafanye kuwa wanafunzi wangu".
Ungekuwa na uelewa japo kidogo, ungejua kuwa mapokeo ya ukristo yalikuwa makubwa zaidi nje ya Uyahudi kuliko ndani ya Uyahudi. Hivyo haishangazi na wala haiendi tofauti na yale aliyoyaeleza Kristo kuwa yangetokea.
Kama ni mkristo, jibidishe uunue ukristo, maana inaonekana umchanga sana, hujui hata ibada zilivyokuwa zikifanyika wakati wa karne ya kwanza, na wala huna uelewa wa kujua maana ya kuabudu, ndiyo maana unasema kuwa kuna watu wanaabudu sanamu. Sijawahi kusikia kuna wakristo wanabudu sanamu, labda kama hujui maana ya kuabudu. Ninaojua kuwa huwa wanaabudu sanamu ni dini za huko India. Na kwa agano la kale, Wayahudi pia waliwahi kumtengeneza ndama, wakamfanya kuwa mungu wao, wakamwabudu. Lakini baada ya kupewa amri 10 za Mungu, hawakuwahi kufanya hivyo tena, bali walisafiri na sanduku la Agano kwa heshima kunwa, na humo ndimo zilimowekwa amri 10 za Mungu. Na kule jangwani waliambiwa watengeneze nyoka wa shaba, na walipougua au kuumwa na wanyama/wadudu wenye sumu, walimtazama nyoka wa shaba, nao walipona. Sanamu hii ya nyoka wa shaba hawakuifanya kuwa Mungu wao, wala hawakuiabudu, japo waliiheshimu sana.
Kuhusu Mama Maria, pia inaonekana umepungukiwa tu ufahamu wa kiimani. Wa kwanza kumheshimu Mama Maria alikuwa ni malaika Gabriel. Alipomletea ujumbe, alisema:
28 Malaika Gabrieli alimtokea Mariamu, akamwambia: “Salaamu, ewe binti uliyebarikiwa, Bwana yu pamoja nawe!”
Wakatoliki wakiyarudia maneno hayo ya malaika, wamefanya kosa gani?
Lakini yasikilize maneno ya Elizabeth alipotembelewa na Maria:
Maria akaingia nyumbani kwa Zakaria akamsalimu Elizabeti. 41 Naye aliposikia salaamu za Mariamu, mtoto aliyekuwa tumboni mwake aliruka. Elizabeti akajazwa na Roho Mtakatifu, 42 akasema kwa sauti kubwa:
“Umebarikiwa wewe zaidi ya wanawake wengine wote, naye mtoto utakayemzaa amebarikiwa."
Wakatoliki wakiyarudia maneno hayo ya Elizabeth, nini watakuwa wamefanya kinyume na mafundisho ya Kristo?
Isikilize sala hii ya Maria:
46 Mariamu akasema: “Namtukuza Bwana, 47 na roho yangu inamfurahia Mungu Mwokozi wangu. 48 Kwa kuwa ameutambua unyonge wa mtumishi wake.
"Tangu sasa vizazi vyote wataniita niliyebarikiwa."
Wakatoliki wakisema Maria ni mbarikiwa mwenye nafasi ya pekee, ni nini kilicho kinyume?