Kanisa Takatifu Katoliki la Mitume

Mkuu nakushukuru kwa kunipa shule, ijapokuwa imejaa simulizi za mapokeo ya kibinadamu na mantiki zake. Naomba ukumbuke Neno la Mungu halihitaji kutetewa na falsafa za kibinadamu, kwa kuwa ni kamilifu sana na tena linajitetea lenyewe.

Naomba uitafakali nukuu kutoka katika aya ya Neno hilo hilo,

MATHAYO 23
9 Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni.
10 Wala msiitwe viongozi; maana kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo.

WAKOLOSAI 1:18
Yeye ni kichwa cha mwili wake, yaani kanisa; yeye ni chanzo cha uhai wa huo mwili. Yeye ndiye mwanzo, mzaliwa wa kwanza aliyefufuliwa kutoka kwa wafu, ili awe na nafasi ya kwanza katika vitu vyote.

Lazima tujifinze siri iliyopo nyuma ya kifo na kufufuka kwake Bwana Yesu Kristo. Kwa kufanya Agano Jipya amekuwa ndiye Kuhani Mkuu, na ndiye kichwa cha kanisa lake la kweli. Kanisa hili ni jumuiya ya waongofu wanaolitii Neno lake la kweli.

Kristo kupitia kauli kutoka katika kinywa chake mwenyewe kama alikataza mtu ndani ya mwili wa kanisa lake kutambulika kwa cheo cha "ubaba" ama "upapa" ama kiongozi mkuu, sasa inakuwaje cheo hiki kinakuja kuibukia kanisani kule Rumi badala ya Yerusalemu, na pia tunaona cheo hiki hakipo katika kitabu cha Matendo ya Mitume!?

Kanisa Katoliki la Rumi ndilo mama wa dini ya Kikristo na utitiri wa madhehebu ndani yake. Kwa kufanya hivyo ndiyo ili "cement" rasmi matendo ya Unikolai.

“Nikolai” ni neno la kigiriki lenye maana ya “Kuteka madhabahu”.

Ijapo kuwa Unikolai ulianza toka siku za awali za uwepo wa Kanisa.. Lakini mfumo rasmi ulisimamishwa na upapa wa Rumi ambapo uliondoa nafasi ya uongozi wa Roho Mtakatifu ndani ya kanisa, na badala yake kusimamisha uongozi wa wanadamu.
 
Hakuna mtume amewahi kuwa mkatoliki
Kama unamfaham mtaje mmoja
Petro hakuanzisha kanisa katoliku wala kukanyaga rumi maisha yake yote
Aliendeleza kanisa la mitume Jerusalem

Kanisa la kwanza sio katoliki
Kanisa kwanza ni la mitume la Jerusalem
Na halijawahi kuwa na oadri wala sister wala sala za bikira maria, na kubusu masanamu.

Katoliki ni dhehebu la kwanza (sio kanisa la kwanza)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…