Kansa ya matiti inammaliza mke wangu nikiwa nashuhudia, sina la kufanya. Sijui kama naweza kusahau hili

Mkuu hiyo kitu inayoitwa cancer ni hatari sana, mwezi may nimeishuhudia ikimuondoa dada yangu. Ilikuwa cancer ya titi yaani unaoza polepole huku unaongea Hadi dk ya mwisho
 
Mkuu fata huu ushauri huyu ni mtu wa tatu nasikia akizungumzia issue ya majani ya mstafeli kutibu cancer usipuuze please. Pole sana Mungu awasimamie.
 
Comments nyingine za ajabu aise. Huyo Mungu amemsahau mja wake? Kwamba walikuwa hawaombi? Hata kama,baada ya maumivu makali hakuomba? Mungu gani wa kumuacha mtu ateseke kiasi hicho? Mungu wako hana msaada wowote kwa hilo,mleta mada angekuwa na shida hiyo,makanisa anajua yalipo. Hapa si pa kuleta hizo abc
 
Aisee hii Dunia ina viumbe vya hovyo kama BICHWA KOMWE
 
Ungemfariji tu jamaa yupo kwnye hali ngumu sana.
Hayo mamimea unayoyasifu ndio chanzo cha magonjwa ya figo sbbu watu wanakunywa bila kipimo.
Trend ya wagonjwa wa Figo kuongezeka vijijiñi sio nzuri
 
Apumzike kwa amani brother, alikumbwa na kansa ya eneo gani?
Ukikubali kudanganywa na hao MAROBOTI wanaoamini kwamba MAKEMIKALI YANAPONYA au MIONZI INAPONYA, utampoteza mkeo mapema sana.

Kama MIONZI inaponya, mkeo angepona. PAMBANA na Hizi TIBA umeelekezwa na watu pale juu. Usiwachukulie poa, hao ndo MALAIKA wanamuokoa mkeo.
 
Ungemfariji tu jamaa yupo kwnye hali ngumu sana.
Hayo mamimea unayoyasifu ndio chanzo cha magonjwa ya figo sbbu watu wanakunywa bila kipimo.
Trend ya wagonjwa wa Figo kuongezeka vijijiñi sio nzuri
Huna lolote we DALALI WA MACHANJO.

Tangu lini mchicha ukaharibu FIGO bwana wewe!? 🤣

MAKEMIKALI yale mnayowalisha watu ndo yanawamaliza. Na MIONZI mtu anabanikwa kwenye TANURU LA MIONZI kama ndafu.

Wauaji wakubwa!
 
Pia nilikua nawaza kurudi hospital kwaajili ya mionzi. Pia nikawa nawza ambavyo wengine wanasema mionzi ndo inaumiza zaidi daah, angalau kwa uzoefu wako unashaurije ndugu
 
Sawa umepasua ukweli ila mbona hujasema ni mmea upi huo atumie ila aimarike?, badala ya kusema leta kwanza ufumbuzi wa tatizo, akipona ndiyo tutarudi kupasua huo ukweli mkuu
 
Ahsante sana mkuu, ila kutoonyesha huzun ni ngumu sana mkuu, kuna wakati mpaka nalia kwakweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…