Pole sana ndugu ,pole mno.
Mwenyezi Mungu ampe nguvu ya kuvumilia maumivu, ampe subira na tumaini.
Kuna wakati mwanadamu anafika kikomo kwa namna ya ubinadamu na hapo ndipo Mungu hushika nafasi ,Mungu yupo na yupo kwa wote, wote wenye heri na wenye Shari.
Yupo kwa kila mwenye haja nae, hajifichi wala hayupo mbali sana kwa yoyote aliweka nia ya dhati kumhitaji.
Wakati huu mkiwa mnapitia changamoto hio na maumivu hayo makali na kukata tamaa ndio Mungu hushika nafasi yake.
Ili kukutana na Mungu kwanza kuweni na amani, msilitazame sana hilo tatizo bali muoneni Mungu katika hilo tatizo, mshuhudieni Mungu kwenye hilo tatizo.
Jitahidini sana mfanya ibada na matendo mema na kuwasaidia wengine wenye hali kama ya kwenu, wapeni moyo wenye hali mfano wa ya kwenu, waombeeni wengine walio kama nyie, toeni sadaka za shukurani kwa wenye mahitaji maalumu, tembeleeni wagonjwa, tembeleeni wafungwa tembeleeni wazee na wenye namna yoyote ya udhaifu wanahitaji faraja na tumaini.
Ikiwa mtajaliwa kufanya hivyo itawajieni amani, itawajieni furaha na tumaini, hamtayazama tena tatizo la mke wako kama hapo awali.
Amini kaka nakushuhudia mke wako atapona , kupona kusikotazamiwa wala kudhaniwa .
Binafsi nakuombeeni katika nia zangu hakika nitawaweka nanyi, mwenyezi Mungu yupo na ataonekana kweli katika maisha yenu.