Kapteni Ibrahim Traore adai nchi haiwezi kuendelea ikiwa katika mfumo wa demokrasia

Kapteni Ibrahim Traore adai nchi haiwezi kuendelea ikiwa katika mfumo wa demokrasia

Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso Kapteni Ibrahim Traore amedai nchi haiwezi kupata maendeleo ikiwa katika mfumo wa demokrasia.
Kapteni Traore alitoa kauli hiyo mnamo jumatatu ya tarehe 1 April 2025 wakati wa salamu za kuanza robo ya pili ya mwaka 2025.

Kapteni Traore alidai hakuna nchi yoyote duniani iliyopata maendeleo huku ikiwa katika mfumo wa kidemokrasia bali maendeleo hupatikana kupitia " mapinduzi ya kijamii" ambayo yatahusisha wananchi wote wa nchi husika.
Kapteni Traore pia alisema kuwa nchi ya Burkina Faso kwa sasa haipo katika mfumo wa kidemokrasia bali ipo katika" mapinduzi " na akadai kushangazwa na wasomi wanaopotosha umma kwa kutumia neno" demokrasia"

Je wewe una maoni gani kuhusu madai haya ya Kapteni Traore?
CHANZO: YouTube Channel ya Shirika la Habari la Burkina Faso( RTB)
Jamaa anakubalika, hatawali Kwa mkono wa chuma au jiwe, hajui raia wanaomkosoa, hakopo na kuadaa umma tunajenga nchi Kwa pesa zetu..
 
Sasa kama hivyo ndivyo mnavyotaka, mnamshabikiaga Lisu kwa minajili ipi?

Acheni CCM itawale milele. Lisu, Heche, na wenzao wote funga jela.

Hakuna cha mikutano ya vyama vya siasa.

Piga marufuku wengine wote kufanya shughuli za kisiasa isipokuwa CCM.
 
Hakuna demokrasia ya kweli duniani
Yuko sahihi kwa hilo analosema

Ila majuzi kawaachia waliotaka kuipindua serikali wakati ule na wako huru

Hiyo pia sio demokrasia bali uungwana tu
Nchi nyingi wanauwa na kutesa huku wakisema kuna uhuru na Demokrasia
 
Wanaosema Uingereza kuna demokrasia mbona walitutawala kwa nguvu? Kwanini tusingepiga kura tuchague kama tunataka ukoloni au lah. Mbona ilimiliki watumwa waliolima mashamba kwenye vlsiwa vya Caribbean? Kwanini wasingeruhusu watu wachague kama wanataka kuwa watumwa au lah? Au wale Aborigines wa Australia mbona waliuliwa na kuchinjwa na hao hao waingereza? Hiyo ndo demokrasia? Mbona hadi leo vitu walivyoiba kwetu wamevijaza kwenye makumbusho yao? Kwanini hatupigi kura tuchague kama vitu vyetu virudishwe au viendelee kubaki kwenye makumbusho ya Uingereza? Wamegoma kurudisha hadi vinyago vilivyochongwa na mababu zetu. Hiyo ndo demokrasia?
 
Halafu muda si mrefu wenzake humo kwenye hicho kijeshi chao [more so kikundi tu cha wanamgambo wenye silaha na si jeshi proper] watamfurusha [kumpindua] au watataka kumfurusha.

Ni suala la muda tu.
 
anateuliwa na wanachi through vyama vyao

UK Parliament

Prime Minister

The Prime Minister is the leader of the Government. He or she is the leader of the party that wins the most seats at a general election. After a general election the monarch calls upon the leader of the largest party to form the Government. The Prime Minister chooses the other Members of the Government and has a residence and offices at 10 Downing Street
Kigezo cha mtu kuwa kiongozi wa chama chenye viti vingi bungeni haimaanishi kachaguliwa na wananchi kwakuwa kiongozi anachaguliwa na wanachama wa hicho chama na si kila mwingereza ni mwanachama wa chama fulani.

Tuchukulie Chadema ni moja ya vyama vya Uingereza halafu kikapata seat nyingi bungeni basi hapo Lissu atakuwa ni prime minister wananchi watake wasitake.(mfano tu)

Sasa hapo demokrasia ipo wapi?
 
Hakuna demokrasia ya kweli duniani
Yuko sahihi kwa hilo analosema

Ila majuzi kawaachia waliotaka kuipindua serikali wakati ule na wako huru

Hiyo pia sio demokrasia bali uungwana tu
Nchi nyingi wanauwa na kutesa huku wakisema kuna uhuru na Demokrasia
Walioachiliwa ni waliotaka kupindua serikali wakati Rais akiwa Blaise Compaoré nadhani sio wakati yeye akiwa Rais
 
Africa demokrasia bado wakati wake haujafika, Africa inahitaji viongozi wenye maono na dhamira ya kweli wataoleta mapinduzi ya siasa,uchumi nk, kupitia viongozi hawa mifumo ndio itawekwa na demokrasia ndio itakuwa rahisi kuiishi.
One million dollar comment.

Hii ndio comment niliyokuwa naitafuta mara tu baada ya kuona kichwa cha habari cha hii mada.

Hichi ulichokisema nimewahi kumsikia hata professor maarufu huko Kenya akikisema, kuwa afrika inahitaji zaidi uongozi imara na thabiti unaoweza kutatua changamoto zetu kwa ufanisi, na uongozi huo sio lazima uwe wa kidemokrasia.

Alijaribu kuelezea kidogo athari za demokrasia kwa afrika.. kwa mfano kama sasa hivi Samia ndani ya miaka minne aliiyokaa kuna projects za maendeleo ambazo zimeshakula pesa hajatimiza na anatarajia kuzitimiza muhura wake ujao kama atashinda, sasa ikitokea ameshindwa halafu mshindani wake ndio akawa raisi miaka mitano ijayo.....

Tusema labda nshindani wake huyo ni Tindu Lisu, sasa kama Tindu Lisu akubaliani na hizo projects ambazo Samia alizianzisha ata zi cancell na kisha ataanzisha za kwake kulingana na vipaumbele vyake, kumbuka hapo hizo projects aliazoacha Samia zimeshakula hela za wanainchi...

Haya huyo Tindu Lisu naye anaweza akatawala awamu moja ambapo ndani ya awamu hiyo moja upo uwezekano atakuwa hajamaliza projects nyingi alizoanzisha, kwq hiyo ikitokea mtawala anayefuata akaja na vipaumbele vyake ambavyo vinakinzana na projects za Tindu Lisu atazifuta na kisha ataanzisha zingine.... circle hii itaendelea hivyo hivyo

Hiyo ni moja tu ya athari za kulazimisha demokrasia afrika, kila siku nyie mtakuwa mnaanza moja kutokana utoafouti wa kiitikadi na vipaumbele vya kila awamu... hata sasa hivi tu mifano hai tuko nayo angalia sakata bandari ya bagamoyo.

Kwa hiyo mimi nakubaliana na Captain Traore kabisa, kuwa afrika haitaji demokrasia bali inahitaji uongozi imara utakaoleta mapinduzi kwenye kila nyanja ya maisha yetu.. wanaopenda hiyo demokrasia wasubiri 2080 huko angalau tayari tutakuwa tumeshakuwa na misingi imara ya maendeleo.
 
Demokrasia Marekani na ulaya imekuja Juzi TU miaka ya 40 50 na 60 usijichanganye.
Marekani wana kitu inaitwa Electro college.
Wanawake wameruhusiwa Juzi TU kupiga kura Marekani.
Hivyo ni kweli..... Democracy doesn't and won't work in Africa.
🤣🤣🤣

Kuna watu mnachekesha sana aisee!

Halafu sijui shida ni nini: ni kwamba mna vichwa vizito na hamuelewi mambo mnayoyasikia na kuyasoma au labda mnapata taarifa zenu toka kwenye vyanzo vya habari visivyo vya uhakika na kuaminika?
 
Demokrasia ili ifanikiwe inahitaji watu walionyooka kuanzia ngazi ya familia.sasa uku kona kona na vichochoro vingi Demokrasia hawez fanya kitu
 
Demokrasia ni nini ? People's Power ni jambo jema sana lakini sababu hakuna direct democracy na kuna representation ambapo average voter hata hajui anataka nini hivyo kunakuwa na demagogues ambao wanapindisha mambo au kutumia watu kupitisha ajenda zao... (Case in Point ingawa Trump analikoroga in the long run kwa nchi yake ila watu wanamsifia sababu ni Populist na anajua kucheza na akili zao kama alivyokuwa Hitler)

Hivyo basi really democracy can only occur iwapo tutaweza kutumia teknolojia ambayo watu wenyewe watakuwa na say directly (lakini hili sio jema sana sababu huenda watu wanachotaka sio chema kwao kutokana na kutokuona the bigger picture) hivyo itakuwa bora kwa yoyote kuweza to have their say iwapo they are involved and know what they are talking about..., Shida ni kwamba watu tunahusisha demokrasia na kuchagua watu wa kutufanyia mambo na sio kushiriki katika kufanya mambo...

By the way ana point a Benevolent Dictator will make things done more than a wishy washy democrats
 
🤣🤣🤣

Kuna watu mnachekesha sana aisee!

Halafu sijui shida ni nini: ni kwamba mna vichwa vizito na hamuelewi mambo mnayoyasikia na kuyasoma au labda mnapata taarifa zenu toka kwenye vyanzo vya habari visivyo vya uhakika na kuaminika?
Kwani kuna kitu gani kadanganya hapo kwenye comment? Kiseme kama kipo.
 
Watanzania wanastahili Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi ili kuhakikisha haki na usawa

Tuwaunge mkono CHADEMA katika kampeni ya NO REFORM, NO ELECTION na tunahimiza Watanzania wote kusimama imara kudai haki yetu ya msingi ya Katiba mpya!

Katiba tuliyonayo haikuruhusu wewe kama mwananchi kuhoji viongozi na viongozi wakikutana na maswali magumu wanageuza lengo, badala ya kutoa majibu wanatoa lawama, uchochezi au hata unaweza kuitwa gaidi na ukionewa huruma unaitwa wewe sio mzalendo.

Ni muhimu kuwa na viongozi tuliowachagua kwa kura zetu ili tuwe na uwezo wa kuwawajibisha pindi wanapokiuka maagizo yetu, pia tuwe na uwezo wa kuwapokonya mshahara na posho wanazopata kupitia kodi zetu.

Naomba kuwasilisha kwako, na wewe hakikisha unawafikishia wengine watano zaidi.

#NoReformNoElection ✊🏾 #KatibaMpyaSasa 📢 #TumeHuru 🗳️
 
Wanaosema Uingereza kuna demokrasia mbona walitutawala kwa nguvu? Kwanini tusingepiga kura tuchague kama tunataka ukoloni au lah. Mbona ilimiliki watumwa waliolima mashamba kwenye vlsiwa vya Caribbean? Kwanini wasingeruhusu watu wachague kama wanataka kuwa watumwa au lah? Au wale Aborigines wa Australia mbona waliuliwa na kuchinjwa na hao hao waingereza? Hiyo ndo demokrasia? Mbona hadi leo vitu walivyoiba kwetu wamevijaza kwenye makumbusho yao? Kwanini hatupigi kura tuchague kama vitu vyetu virudishwe au viendelee kubaki kwenye makumbusho ya Uingereza? Wamegoma kurudisha hadi vinyago vilivyochongwa na mababu zetu. Hiyo ndo demokrasia?
Au Wamarekani kuwanyima watu weusi na wasio wazungu haki kama raia, ikiwemo kupiga kura hadi 1964. Ndiyo ilikuwa demokrasia?

Utawala wa kidemokrasia uliharibu uchumi wa Brazil. Jeshi likachukua nchi kutoka 1964-1985. Kipindi hicho kinaitwa "Brazil Miracle." Uchumi wao ulikuwa kwa kasi isivyo kawaida.
 
stupid as africans are... mpuuzi huyu anataka kutawala milele. WHY NOT DEMOKRASI? MBONA WESTERN WORLD AMBAO WANA DEMOKRASIA BY 100% WAMEEDNDELEA? see Denmark, Norway, and Sweden Finland ni democratic by 100% but highly developed first world! JINGA KUMBE NALO! lakini, ni mitulinga mingi akili kidogo...... NA YEYE ATAPINDULIWA
Usichokijua wewe pamoja na wajinga wenzio wenye mawazo kama haya yako ambao mmekaririshwa kuwa maendeleo lazima yapatikane kwa kile mnachokiita demokrasia, ni kwamba nchi nyingi unazoziona zina maendeleo leo hii ikiwemo hizi ulizotaja hapo juu zilipata misingi ya maendeleo yao nyakati ambazo walikuwa hawana tawala za kidemokrasia, mfano kama hao Sweeden walianza kupata maendeleo makubwa walipokuwa chini ya King Oscar II mwishoni mwa miaka ya 1890s na kipindi hicho mfalme ndio alikuwa final decision maker....

Hizi demokrasia unazoona wameanza kuzipractice kwenye mirongo ya hivi karibuni baada ya kuwa tayari wameshaimarisha mifumo imara ya kiuchumi, ndio wakawaleteeni na nyie wamatumbi wa dunia ya tatu kwamba eti demokrasia ndio msingi wa maendeleo bila demokrasia huwezi kupata hayo maendeleo.

Nchi nyingi za kiafrika zipo stage ambayo hizo scandvania countries zilikuwepo karne iliyopita, kwa hiyo utakuwa ni uwendowazimu kuziongoza nchi hizi za kiafrika kama unaiongoza sweeden ambayo ilishajipata tangu karne iliyopita...

Tatizo watu wenye akili ndogo na duni kama wewe mkishafundishwa tu huko madarasani kwenye vitopic vya civics sijui demokrasia ndio msingi wa utawala bora, mnayashika kama yalivyo hamuwezi hata kuyachanganua kama hayo mliyofundishwa darasani je, ni kweli yako realistic kwenye maisha yetu..?

Fungua hiyo brain yako na ugundue uhalisia uko vipi mshamba wa demokrasia wewe.

Kwanza una habari hata Donald Trump anataka kuongeza muda wake wa kukaa ikulu ya white house, ndugu mpenda demokrasia?
 
Kule wameendelea kwa sababu kila mtu ana akili, huku Afrika bila mijeledi hatuendi as hatuna reasoning ya kutosha. Traore yupo sahihi, mwafrika haongozwi kwa demokrasia coz hawezi kuishi kidemokrasia. Watu wamefanya tafiti za kutosha, Afrika haihitaji demokrasia.
 
Usichokijua wewe pamoja na wajinga wenzio wenye mawazo kama haya yako ambao mmekaririshwa kuwa maendeleo lazima yapatikane kwa kile mnachokiita demokrasia, ni kwamba nchi nyingi unazoziona zina maendeleo leo hii ikiwemo hizi ulizotaja hapo juu zilipata misingi ya maendeleo yao nyakati ambazo walikuwa hawana tawala za kidemokrasia, mfano kama hao Sweeden walianza kupata maendeleo makubwa walipokuwa chini ya King Oscar II mwishoni mwa miaka ya 1890s na kipindi hicho mfalme ndio alikuwa final decision maker....

Hizi demokrasia unazoona wameanza kuzipractice kwenye mirongo ya hivi karibuni baada ya kuwa tayari wameshaimarisha mifumo imara ya kiuchumi, ndio wakawaleteeni na nyie wamatumbi wa dunia ya tatu kwamba eti demokrasia ndio msingi wa maendeleo bila demokrasia huwezi kupata hayo maendeleo.

Nchi nyingi za kiafrika zipo stage ambayo hizo scandvania countries zilikuwepo karne iliyopita, kwa hiyo utakuwa ni uwendowazimu kuziongoza nchi hizi za kiafrika kama unaiongoza sweeden ambayo ilishajipata tangu karne iliyopita...

Tatizo watu wenye akili ndogo na duni kama wewe mkishafundishwa tu huko madarasani kwenye vitopic vya civics sijui demokrasia ndio msingi wa utawala bora, mnayashika kama yalivyo hamuwezi hata kuyachanganua kama hayo mliyofundishwa darasani je, ni kweli yako realistic kwenye maisha yetu..?

Fungua hiyo brain yako na ugundue uhalisia uko vipi mshamba wa demokrasia wewe.

Kwanza una habari hata Donald Trump anataka kuongeza muda wake wa kukaa ikulu ya white house, ndugu mpenda demokrasia?
India waliingia kwenye mkumbo wa demokrasia ndio sababu mojawapo wameshindwa kuifikia China kwenye maendeleo. Wakati wako busy na siasa, wenzao China wanachapa kazi viwandani.
 
Back
Top Bottom