Kapteni Ibrahim Traore adai nchi haiwezi kuendelea ikiwa katika mfumo wa demokrasia

Kapteni Ibrahim Traore adai nchi haiwezi kuendelea ikiwa katika mfumo wa demokrasia

Haelewi kabisa, anafikiri maamuzi yake ndio ya mwisho, ajiulize akina Gadaffi kuwa walikosea nini?
Dunia ina wenyewe, hawa marais wa dunia ya 6 ni ALAMA tu za viongozi lajini RIMOTI zimeshikiliwa na wenye dunia yao
Kitendo tu cha wewe kusema dunia ina wenyewe sijui wao ndio wameshika remote tayari moja kwa moja unadhiirisha hii dunia aina hiyo demokrasia, maana tayari kuna watu wenye nguvu kuliko wengine na ndio wanaamua dunia iende vipi na wakati huo katika demokrasia tunaambiwa hakuna mtu ambaye yuko juu ya mwingine.

Sasa kama ni hivyo basi Traore yupo sahihi kwa kuipuuza kabisa hiyo demokrasia, maana hata hao unaowaita wakubwa wa dunia hawaifuati hiyo demokrasia kwa sababu wanawapangia wengine wajiongoze vipi.
 
Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso Kapteni Ibrahim Traore amedai nchi haiwezi kupata maendeleo ikiwa katika mfumo wa demokrasia.
Kapteni Traore alitoa kauli hiyo mnamo jumatatu ya tarehe 1 April 2025 wakati wa salamu za kuanza robo ya pili ya mwaka 2025.

Kapteni Traore alidai hakuna nchi yoyote duniani iliyopata maendeleo huku ikiwa katika mfumo wa kidemokrasia bali maendeleo hupatikana kupitia " mapinduzi ya kijamii" ambayo yatahusisha wananchi wote wa nchi husika.
Kapteni Traore pia alisema kuwa nchi ya Burkina Faso kwa sasa haipo katika mfumo wa kidemokrasia bali ipo katika" mapinduzi " na akadai kushangazwa na wasomi wanaopotosha umma kwa kutumia neno" demokrasia"

Je wewe una maoni gani kuhusu madai haya ya Kapteni Traore?
CHANZO: YouTube Channel ya Shirika la Habari la Burkina Faso( RTB)
Ukweli ulio komaa. Maana hili neno democracy limetuletea matatizo makubwa sana Africa, mpaka nchi za mabebelu zinaingilia mambo ya ndani ya Africa Kwa mgongo wa democracy.
 
Africa tunahitaji Hitler wetu, Mao Ze Dong wetu na Lenin Putin wetu la sivyo tutaendelea kuwekewa masharti ya kuchukua mikopo na nchi yenye vyama viwili ( Marekani) halafu nchi inayowekewa masharti ina vyama 19.
 
Malizia tena nchi ambayo wanaomchagua Rais ni watu 200 wakati Raia wako milioni 200
Africa tunahitaji Hitler wetu, Mao Ze Dong wetu na Lenin Putin wetu la sivyo tutaendelea kuwekewa masharti ya kuchukua mikopo na nchi yenye vyama viwili ( Marekani) halafu nchi inayowekewa masharti ina vyama 19.
 
🤣🤣🤣

Kuna watu mnachekesha sana aisee!

Halafu sijui shida ni nini: ni kwamba mna vichwa vizito na hamuelewi mambo mnayoyasikia na kuyasoma au labda mnapata taarifa zenu toka kwenye vyanzo vya habari visivyo vya uhakika na kuaminika?
1. Passed by Congress June 4, 1919, and ratified on August 18, 1920, the 19th amendment granted women the right to vote. The 19th amendment legally guarantees American women the right to vote. Achieving this milestone required a lengthy and difficult struggle—victory took decades of agitation and protest.

2. In 1948, three years after the end of World War II, President Harry S. Truman signed the Women's Armed Services Integration Act into law, officially allowing women to serve as full, permanent members of all branches of the Armed Forces.

3.

What is the Electoral College?​

The Electoral College is a process, not a place. The Founding Fathers established it in the Constitution, in part, as a compromise between the election of the President by a vote in Congress and election of the President by a popular vote of qualified citizens.

What is the process?​

The Electoral College process consists of the selection of the electors, the meeting of the electors where they vote for President and Vice President, and the counting of the electoral votes by Congress.

How many electors are there? How are they distributed among the States?​

The Electoral College consists of 538 electors. A majority of 270 electoral votes is required to elect the President. Your State has the same number of electors as it does Members in its Congressional delegation: one for each Member in the House of Representatives plus two Senators. Read more about the allocation of electoral votes.

The District of Columbia is allocated 3 electors and treated like a State for purposes of the Electoral College under the 23rd Amendment of the Constitution. For this reason, in the following discussion, the word “State” also refers to the District of Columbia and “Executive” to the State Governors and the Mayor of the District of Columbia.

How are my electors chosen? What are their qualifications? How do they decide who to vote for?​

Each candidate running for President in your State has their own group of electors (known as a slate). The slates are generally chosen by the candidate’s political party in your State, but State laws vary on how the electors are selected and what their responsibilities are. Read more about the qualifications of the electors and restrictions on who the electors may vote for.

What happens in the general election? Why should I vote?​

The general election is held every four years on the Tuesday after the first Monday in November. When you vote for a Presidential candidate you are actually voting for your candidate's preferred electors. Learn more about voting for the electors.

Most States have a “winner-take-all” system that awards all electors to the Presidential candidate who wins the State's popular vote. However, Maine and Nebraska each have a variation of “proportional representation.” Read more about the allocation of electors among the States.

What happens after the general election?​

After the general election, your State's Executive prepares a Certificate of Ascertainment listing the names of all the individuals on the slates for each candidate. The Certificate of Ascertainment also lists the number of votes each individual received and shows which individuals were appointed as your State's electors. Your State’s Certificate of Ascertainment is sent to NARA as part of the official records of the Presidential election.

The meeting of the electors takes place on the first Tuesday after the second Wednesday in December after the general election. The electors meet in their respective States, where they cast their votes for President and Vice President on separate ballots. Your State’s electors’ votes are recorded on a Certificate of Vote, which is prepared at the meeting by the electors. Your State’s Certificate of Vote is sent to Congress, where the votes are counted, and to NARA, as part of the official records of the Presidential election.

Each State’s electoral votes are counted in a joint session of Congress on the 6th of January in the year following the meeting of the electors. Members of the House and Senate meet in the House Chamber to conduct the official count of electoral votes. The Vice President of the United States, as President of the Senate, presides over the count in a strictly ministerial manner and announces the results of the vote. The President of the Senate then declares which persons, if any, have been elected President and Vice President of the United States.

The President-elect takes the oath of office and is sworn in as President of the United States on January 20th in the year following the general election.
 
Hata mimi nasemaga humu kila siku. Nchi haiwezi kuendelea chini ya demokrasia. Demokrasia ina walaji(machawa) wengi sana ambao usipowaridhisha huwezi baki madarakani. Wazungu walipotuletea demokrasia walikuwa wanajua wanachokifanya.
"Wazungu" hawakuleta demokrasia Afrika. Walileta ukoloni na ukoloni mamboleo.

Kuwa na demokrasia au kutokuwa na demokrasia ni uamuzi wa nchi.

Waafrika na viongozi wao wenyewe ndio walioamua kufuata mfumo wa demokrasia kisanii ili waendelee kupata misaada toka Magharibi, waweze kuhifadhi mapato yao binafsi ya kifisadi, na kwenda kula bata huko huko bila kusumbuliwa. Trump keshawapa tahadhari.

Demokrasia haitaki kabisa usanii kama ule unaofanywa nchini tangu 1992 na kuendelezwa kwenye Maridhiano na 4R.

Waafrika wengi ndipo walipokwama na kukimbilia kusingizia kwamba kukosa maendeleo tatizo ni demokrasia! Ni kama muathirika wa HIV kurukaruka kwenye umezaji wa ARV halafu mashambulizi yakianza kujitokeza unakimbilia kusingizia ARV ndio tatizo.
 
Waliam

Waliamua kufata demokrasia au walilazimishwa? Kataa kufata demokrasia upigwe vikwazo uone kama mwenyewe hautarudi kwenye hiyo demokrasia. Lakini mwarabu hafati demokrasia na hawekewi vikwazo. Hapo ndo ujue tuko kwenye ukoloni uliokubuhu. Uhuru wa bendera tunadanganywa
 
Demokrasia ili ifanikiwe inahitaji watu walionyooka kuanzia ngazi ya familia.sasa uku kona kona na vichochoro vingi Demokrasia hawez fanya kitu
Sahihi kabisa mkuu, demokrasia ina thrive kwa watu ambao tayari wameandaliwa kuishi kidemokrasia tangu udogoni.

Familia zetu nyingi za kiafrika baba ndio msemaji na muamuzi mkuu wa karibu kila jambo akitoka yeye anakuja mama, mtoto ni mtu wa kufuata tu kile kilichoamuliwa na baba kama kiongozi wa familia... yaani huwa tunalelewa kwenye aina fulani ya autocratic leadership culture, halafu eti leo hii mtu huyo ashike madaraka aje aongoze watu kidemokrasia? Hata kama atajaribu basi itakuwa ni kiini macho tu...!!

Na pia kitu kingine lazima pawepo na uchumi imara kwa jamii husika kiasi kwamba mahitaji yote ya msingi yapo na sio mazingira ya njaa njaa yanayoruhusu corruption ku exist..!! Palipo na corruption hiyo demokrasia haiwezi kufanya chochote.
 
India waliingia kwenye mkumbo wa demokrasia ndio sababu mojawapo wameshindwa kuifikia China kwenye maendeleo. Wakati wako busy na siasa, wenzao China wanachapa kazi viwandani.
Kuendekeza demokrasia kwa taifa linaloendelea ni kurudisha nyuma maendeleo, wakati nyie mnabishana sera za nani ni sahihi na za nani zina mapungufu tena huku mkitukanana majukwaani... wenzenu wako bize na kufanya vumbuzi mbali mbali zinazolipeleka mbele taifa.

Leo hii Russia licha ya vikwazo walivyowekewa kila kona ya dunia, lakini bado ni taifa imara kijeshi na kiuchumi... sababu moja wapo ni pamoja na hiyo ya kuendekeza masuala ya demokrasia
 
Demokrasia ni nini ? People's Power ni jambo jema sana lakini sababu hakuna direct democracy na kuna representation ambapo average voter hata hajui anataka nini hivyo kunakuwa na demagogues ambao wanapindisha mambo au kutumia watu kupitisha ajenda zao... (Case in Point ingawa Trump analikoroga in the long run kwa nchi yake ila watu wanamsifia sababu ni Populist na anajua kucheza na akili zao kama alivyokuwa Hitler)

Hivyo basi really democracy can only occur iwapo tutaweza kutumia teknolojia ambayo watu wenyewe watakuwa na say directly (lakini hili sio jema sana sababu huenda watu wanachotaka sio chema kwao kutokana na kutokuona the bigger picture) hivyo itakuwa bora kwa yoyote kuweza to have their say iwapo they are involved and know what they are talking about..., Shida ni kwamba watu tunahusisha demokrasia na kuchagua watu wa kutufanyia mambo na sio kushiriki katika kufanya mambo...

By the way ana point a Benevolent Dictator will make things done more than a wishy washy democrats
Una mantiki kubwa sana kwenye hili bandiko lako, japo umetumia lugha ya mzunguko sana
 
Yuko sahihi!

Hata nchi zilizoendelea zilileta democrasia baadae baada ya maendeleo kupatikana chini ya udikteta.

Wajinga watampinga
 
Hizo nchi zote ulizotaja hazina Marais zote zinaongozwa na wafalume ambao hawatoki madarakani !!! Chaguzi zinazofanywa ni Kwa nafasi ya mawaziri wakuu TU !!! Hapo kunademokrasia ??? Nchi chache saana ulaya zenye mkuu wa inchi ambaye ni president nyingi zinaongozwa na falume zao
Acha uongo
Mawaziri wakuu ndo wanaaandaa budget na kuratibu maendeo bila hata kuhusisha wafalme

Wafalme wapo kama ceremoniously tu nchi za ulaya zinafuata mfumo wa rule of law na sio one man show huko walishavukaga mda sana
 
Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso Kapteni Ibrahim Traore amedai nchi haiwezi kupata maendeleo ikiwa katika mfumo wa demokrasia.
Kapteni Traore alitoa kauli hiyo mnamo jumatatu ya tarehe 1 April 2025 wakati wa salamu za kuanza robo ya pili ya mwaka 2025.

Kapteni Traore alidai hakuna nchi yoyote duniani iliyopata maendeleo huku ikiwa katika mfumo wa kidemokrasia bali maendeleo hupatikana kupitia " mapinduzi ya kijamii" ambayo yatahusisha wananchi wote wa nchi husika.
Kapteni Traore pia alisema kuwa nchi ya Burkina Faso kwa sasa haipo katika mfumo wa kidemokrasia bali ipo katika" mapinduzi " na akadai kushangazwa na wasomi wanaopotosha umma kwa kutumia neno" demokrasia"

Je wewe una maoni gani kuhusu madai haya ya Kapteni Traore?
CHANZO: YouTube Channel ya Shirika la Habari la Burkina Faso( RTB)
Kauli chungu sana kwa sisi wapenda demokrasia lkn kwa hiki kizazi Cha sasa Cha mtu mweusi ni ngumu sana mtu kutimiza wajibu wake bila kubuluzwa buluzwa.

Hii watanielewa watu ambao wameajiri/ ama kufanya kazi na Hawa vijana wetu wa 2000.
 
Lakini hizo one man show ndo ziliwavusha kutoka kwenye umaskini hadi kuwa hapo walipo leo.
 
Kauli chungu sana kwa sisi wapenda demokrasia lkn kwa hiki kizazi Cha sasa Cha mtu mweusi ni ngumu sana mtu kutimiza wajibu wake bila kubuluzwa buluzwa.

Hii watanielewa watu ambao wameajiri/ ama kufanya kazi na Hawa vijana wetu wa 2000.
Kwani lini watu walitimiza wajibu wao bila kubuluzwa? Hao wezi wa mali za umma nao ni vijana wa 2000?
 
Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso Kapteni Ibrahim Traore amedai nchi haiwezi kupata maendeleo ikiwa katika mfumo wa demokrasia.
Kapteni Traore alitoa kauli hiyo mnamo jumatatu ya tarehe 1 April 2025 wakati wa salamu za kuanza robo ya pili ya mwaka 2025.

Kapteni Traore alidai hakuna nchi yoyote duniani iliyopata maendeleo huku ikiwa katika mfumo wa kidemokrasia bali maendeleo hupatikana kupitia " mapinduzi ya kijamii" ambayo yatahusisha wananchi wote wa nchi husika.
Kapteni Traore pia alisema kuwa nchi ya Burkina Faso kwa sasa haipo katika mfumo wa kidemokrasia bali ipo katika" mapinduzi " na akadai kushangazwa na wasomi wanaopotosha umma kwa kutumia neno" demokrasia"

Je wewe una maoni gani kuhusu madai haya ya Kapteni Traore?
CHANZO: YouTube Channel ya Shirika la Habari la Burkina Faso( RTB)
Hilo jinga litaonesha rangi halisi muda si mrefu na watajuta kumfahamu. Huyo hajui ht maana ya demokrasia. Anaifahamu Marekani?
 
stupid as africans are... mpuuzi huyu anataka kutawala milele. WHY NOT DEMOKRASI? MBONA WESTERN WORLD AMBAO WANA DEMOKRASIA BY 100% WAMEEDNDELEA? see Denmark, Norway, and Sweden Finland ni democratic by 100% but highly developed first world! JINGA KUMBE NALO! lakini, ni mitulinga mingi akili kidogo...... NA YEYE ATAPINDULIWA
Kwani Kuna wakati ulifikiri ana akili?
 
Kaongea ukweli ila kueleweka itachukua muda!, kukataa demokrasia sio kwamba wewe ni dictator!.
sasa wengi na najua zitaanza kuzuka tetesi na kashifa za dictator kwenye nchi yake!, hizo ni kawaida maana properganda lazima aanzishiwe hata magufuli hapa bongo aliitwa kila aina ya jina!.

Mi nafikiri aina ya uongozi na kujiongoza nchi zinaweza kuchagua njia zake vile itaona inafaa, wapo wanaongoza nchi ki falme wanaenda vyema tu!.
Africa demokrasia ni udhaifu, huwezi kumuongoza mtu mwenye njaa kidemokrasia na asiibe, mtu alipwe laki na nusu lije zali la million ati aliaachie!. demokrasia kwetu inatakiwa ianzie kwa viongozi ngazi za juu wakituonyesha wao na huku chini watu wataanza kubadirika lkn huko juu kila siku ni ufujaji na hasara zakutosha!.. na wanajiita wasomi hehe!
Sijui ht kw ww mwenyewe unaelewa ulichoandika
 
Wanaosema Uingereza kuna demokrasia mbona walitutawala kwa nguvu? Kwanini tusingepiga kura tuchague kama tunataka ukoloni au lah. Mbona ilimiliki watumwa waliolima mashamba kwenye vlsiwa vya Caribbean? Kwanini wasingeruhusu watu wachague kama wanataka kuwa watumwa au lah? Au wale Aborigines wa Australia mbona waliuliwa na kuchinjwa na hao hao waingereza? Hiyo ndo demokrasia? Mbona hadi leo vitu walivyoiba kwetu wamevijaza kwenye makumbusho yao? Kwanini hatupigi kura tuchague kama vitu vyetu virudishwe au viendelee kubaki kwenye makumbusho ya Uingereza? Wamegoma kurudisha hadi vinyago vilivyochongwa na mababu zetu. Hiyo ndo demokrasia?
Kaka hili bandiko lako hakuna hata mmoja miongoni mwa hawa washadadia demokrasia walio comment hapa wanaweza kukupa majibu...

Mimi binafsi huwa naamini muafrika aliyekariri elimu ya kimagharibi ni mjinga kuliko hata yule ambaye hajasoma kabisa.

Waafrika wengi wanaojifanya kusifia nchi za magharibi kwa ukomavu wao wa demokrasia, hawana ufahamu wa kuweza kutambua kuwa demokrasia yao inanuka damu na dhuluma walizofanya kwa watu wengine..!! Na hivyo inawaondolea uhalali wa wao kujifanya ni mababa wa demokrasia hapa duniani.

Kuna nchi kama Uingereza kipindi inatawala nusu ya dunia ilipora mali nyingi sana, kupitia utawala wake wa kimabavu watu wengi sana walikufa..... ni baada ya wao kuwa tayari wameshajiimarisha kiuchumi kupitia dhuluma walizofanya ndio sasa wakaanza kuhuburi demokrasia wakizilazimisha na nchi zingine nazo pia zifuate hiyo demokrasia.

Pamoja na maovu yote waliyoyafanya hapa duniani kwa jamii zingine, lakini hata siku moja hao waingereza hawajawahi kuomba msamaha au hata kulipa fidia ya dhuluma walizofanya kwenye mataifa ambayo ni wahanga wa utawala wao wa kimabavu walioufanya miaka ile.

Sasa kama hao waingereza ni wana demokrasia kweli na wanajuitia kile walichokifanya ni kwanini mpaka leo hatujaona wakiomba radhi au kurudisha vile vitu walivyodhulumu kwa jamii zingine?
 
Back
Top Bottom