Strong ladg
JF-Expert Member
- Jul 15, 2021
- 1,357
- 3,114
- Thread starter
- #161
Hujakosea. Binafsi nikisikia hawa wakoloni wanahubiri sijui demokrasia sijui haki za binadamu napata kichefuchefu. Hao waingereza ndo walituma silaha zikawaua mamilioni ya watu wa kabila la Igbo waliokuwa wanapigania uhuru wao kutokana na kutengwa na serikali ya Nigeria. Kama kweli Uingereza ina demokrasia kwanini hawakuheshimu maamuzi ya jamii ya kabila la Igbo? Badala yake wakashiriki mauaji ya kimbari yaliyowatekeza watu milioni 3 wa kabila la Igbo. Kuna wafanyakazi wa bandarini pale Uingereza waligoma kupakia silaha zilizokuwa zinapelekwa Nigeria lakini walilazimishwa na viongozi wapakie silaha kwa lazima. Watoto wa Igboland walikonda kwa njaa kali baada ya serikali ya Nigeria kutumia mbinu ya " starve to death" ambayo hata vitani haikubaliki lakini serikali ya Uingereza ndo kwanza ilishirikiana bega kwa bega na waliokuwa wanaua watoto kwa njaa. Halafu leo hii kiongozi wa Uingereza unakuta anahubiri demokrasia na watu hapa Afrika wanasikiliza. Bora Traore anakataa huu ujinga wa demokrasia ya kuhubiriwa na wakoloni waziwazi .Kaka hili bandiko lako hakuna hata mmoja miongoni mwa hawa washadadia demokrasia walio comment hapa wanaweza kukupa majibu...
Mimi binafsi huwa naamini muafrika aliyekariri elimu ya kimagharibi ni mjinga kuliko hata yule ambaye hajasoma kabisa.
Waafrika wengi wanaojifanya kusifia nchi za magharibi kwa ukomavu wao wa demokrasia, hawana ufahamu wa kuweza kutambua kuwa demokrasia yao inanuka damu na dhuluma walizofanya kwa watu wengine..!! Na hivyo inawaondolea uhalali wa wao kujifanya ni mababa wa demokrasia hapa duniani.
Kuna nchi kama Uingereza kipindi inatawala nusu ya dunia ilipora mali nyingi sana, kupitia utawala wake wa kimabavu watu wengi sana walikufa..... ni baada ya wao kuwa tayari wameshajiimarisha kiuchumi kupitia dhuluma walizofanya ndio sasa wakaanza kuhuburi demokrasia wakizilazimisha na nchi zingine nazo pia zifuate hiyo demokrasia.
Pamoja na maovu yote waliyoyafanya hapa duniani kwa jamii zingine, lakini hata siku moja hao waingereza hawajawahi kuomba msamaha au hata kulipa fidia ya dhuluma walizofanya kwenye mataifa ambayo ni wahanga wa utawala wao wa kimabavu walioufanya miaka ile.
Sasa kama hao waingereza ni wana demokrasia kweli na wanajuitia kile walichokifanya ni kwanini mpaka leo hatujaona wakiomba radhi au kurudisha vile vitu walivyodhulumu kwa jamii zingine?