Kaptula la Marx: Unafahamu kwanini kitabu hiki kilipigwa marufuku? Waandishi wetu na Siasa zetu

hawezi kukosa
 
Na amefanikiwa ku corrupt mind za wabongo sana.
 
Hicho cha the dark side of nyerere tupe udodonozi
Ludovic Mwaijage anaelezea mambo yake binafsi alivyo kuwa mkimbizi wa kisiasa kutoka Tanzania, na jinsi alivyo kuwa captured Swaziland kutumia shushu la ki Mozambique. Ni true story
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji1] [emoji23] [emoji23]
 
huyu jamaa kima kazi yupo wapi? anapoishi kwa sasa.
Shafi A Shafi, mzee wa VUTA N'KUVUTE maarufu pia kwa riway ya KULI, amefyatua riwaya nyingine inaitwa HAINI hii ni balaa.......inaswiri kabisa kauli ya "watapata taabu sana". hebu itafute uone kilichomo, waweza kumchukia yeyote aliyemo kwenye Dola.
 
namtafuta Ibrahim Hussen. ni kweli nliambiwa alipata matatizo ya akili na kuwa kuna kipindi alikuwa anauza mitumba kariakoo. ni mtu ambaye nngependa sana kuonana naye. anaishi wapi kwa sasa.

Unaongelea Ibrahim Hussein aliyeandika Mashetani? Kezilahabi ni mkimya na haongei sana. Alikuwa profesa wa fasihi mlimani mpaka alipoamua kuhamia Botswana.[/QUOTE
 
na hili ni tatizo kubwa sana. kweli watanzania wengi hawana utamaduni wa kusoma. hata threads za humu ndani hizi za maneno machache kabisa utakuta kuna mtu ambaye unategemea awe na umri wa kujielewa analalamika kuwa ni ndefu.... unajiuliza huyu ana akili kweli na ufahamu wa kutosha? hatupendi kusoma na ndo maana hatuyajui mengi.

 
ni wazi kezihalabi alikuwa mhuni sana before... haya maneno kila nikiyasoma najaribu kujenga picha ya hako kabinti kanakojipitisha pitisha mbele za watu na tumatako twake tukavu.
 
shule ipo kwenye kusoma vitabu na kupata mafundisho mbalimbali yale mambo ya kupewa cheti yasikuumize sana kichwa. tunafaham usomi wa mtu kwa namna anavyochangia hoja na kupembua. namna anavyotoa masuluhisho kwenye changamoto... mimi nlishaaacha kuulizia ulizia vyetu n.k kuna watu wasomi wa vyeti lakini hawana mchango wowote kwenye jamii.

 
Nilikutana na jamaa mmoja wa UDSM- IKS( Institute of Kiswahili Studies) aliniambia Kezilahabi amepata matatizo ya kwenye ubongo, ubungo wake umefuta kumbukumbu zake zote. Mbaya zaidi amepoteza mpaka uwezo wa kuongea, kwa sasa anafundishwa tena kuunda maneno.
 
ni nini kilitokea kwa nguli huyu wa fasihi? ni jambo la kusikitisha sana.

 
Kweli kabisa tumekuwa wavivu ndio maana uwezo wa kuchanganua mambo ni mdogo sana kwa njia hii hatufiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…