Kaptula la Marx: Unafahamu kwanini kitabu hiki kilipigwa marufuku? Waandishi wetu na Siasa zetu

Kaptula la Marx: Unafahamu kwanini kitabu hiki kilipigwa marufuku? Waandishi wetu na Siasa zetu

Tatizo umagharibi umetuharibu sana. Kwa asili yetu waafrika sanaa ni mali ya jamii nzima, hivyo msanii aliona fahari kuona kazi yake ikielimisha au kuburudisha jamii yake tofauti na sasa ambapo wasanii wanawaza pesa tu.

Naamini wasanii kama watafanya kazi nzuri, jamii itahamasika kupenda kusoma/kusikiliza au kutazama kazi za sanaa kuliko kuacha kabisa kutumia vipaji vyao.

Hivi kwa zama hizi ambazo kumkosoa mh.rais ni kosa la jinai akiibuka mwanafasihi akaweza kutumia kalamu yake vizuri kama walivyokuwa wakifanya akina Kezilahabhi, Chinua Achebe, Ngugi wa Thiongo n.k atakosa wateja?
hawezi kukosa
 
Kweli mkuu. Nilishawahi sema mahali kuwa huyo jamaa mwenye magazeti yenye kauli mbiu za kilokole single handedly ameweza "kuangamiza' kizazi kizima. Ametajirika ndiyo lakini gharama yake ni kubwa sana. Tumekuwa taifa la umbea na ushilawadu. Wenye mawazo mapya na fikra chokonozi wanaonekana maadui. Jamii isiyojali. Sad !!!
Na amefanikiwa ku corrupt mind za wabongo sana.
 
Hicho cha the dark side of nyerere tupe udodonozi
Ludovic Mwaijage anaelezea mambo yake binafsi alivyo kuwa mkimbizi wa kisiasa kutoka Tanzania, na jinsi alivyo kuwa captured Swaziland kutumia shushu la ki Mozambique. Ni true story
 
Fasihi yetu imegeuka mipasho, magazeti ya jamaa mmoja anayeweka kidokezo "IN GOD WE TRUST" lakini ndani yamejaa ugoro mtupu pamoja na vipindi vyepesi vya redio viitwavyo shila wada ndio imekuwa fasihi yetu kwa sasa , hakuna mwandishi anayeumiza kichwa kuandika mambo magumu wala hakuna msomaji anayeumiza kichwa kusoma mambo magumu. Ni udaku kwenda mbele , magazeti ya udaku saa mbili asubuhi tuu yote yameisha.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji1] [emoji23] [emoji23]
 
huyu jamaa kima kazi yupo wapi? anapoishi kwa sasa.
Shafi A Shafi, mzee wa VUTA N'KUVUTE maarufu pia kwa riway ya KULI, amefyatua riwaya nyingine inaitwa HAINI hii ni balaa.......inaswiri kabisa kauli ya "watapata taabu sana". hebu itafute uone kilichomo, waweza kumchukia yeyote aliyemo kwenye Dola.
 
namtafuta Ibrahim Hussen. ni kweli nliambiwa alipata matatizo ya akili na kuwa kuna kipindi alikuwa anauza mitumba kariakoo. ni mtu ambaye nngependa sana kuonana naye. anaishi wapi kwa sasa.

Unaongelea Ibrahim Hussein aliyeandika Mashetani? Kezilahabi ni mkimya na haongei sana. Alikuwa profesa wa fasihi mlimani mpaka alipoamua kuhamia Botswana.[/QUOTE
 
na hili ni tatizo kubwa sana. kweli watanzania wengi hawana utamaduni wa kusoma. hata threads za humu ndani hizi za maneno machache kabisa utakuta kuna mtu ambaye unategemea awe na umri wa kujielewa analalamika kuwa ni ndefu.... unajiuliza huyu ana akili kweli na ufahamu wa kutosha? hatupendi kusoma na ndo maana hatuyajui mengi.

Hata kama wangekuwepo (naamini wapo) vitabu vyao tungevisoma? Sasa waandishi wengi wa fasihi pevu wanatoka Kenya ambako usomaji wa vitabu angalau una unafuu. Hakuna kitu kinachomkatisha tamaa mwandishi kama kuandika kazi ya sanaa halafu isiwe na wasomaji. Tanzania hapa ni mpaka ubahatishe kitabu chako kiingizwe katika mitaala ya shule japo napo nasikia ni mpaka upite njia za mkato na uwe na watu wa kukupigania. Taifa lisilosoma. Taifa lisilojielewa. Taifa lisilo na fikra mpya. Na sasa tumepuuzia masomo ya sanaa na tunataka kila mtoto asome sayansi. Tutakuwa taifa la kwanza hapa duniani kuwa na wanasayansi pekee wakiongoza kila nyanja.
 
ni wazi kezihalabi alikuwa mhuni sana before... haya maneno kila nikiyasoma najaribu kujenga picha ya hako kabinti kanakojipitisha pitisha mbele za watu na tumatako twake tukavu.
Ila huyu Kezilahabi alikuwa na lugha kalikali. Kwenye Dunia uwanja wa fujo kuna kabinti kalibalehe na kakaanza ishu za wavulana vichakani. Basi dingi yake akakakamata na kuanza kukapa stiki huku akisema " vimatako vyenyewe vikavu halafu unataka kutuletea nyege"
 
shule ipo kwenye kusoma vitabu na kupata mafundisho mbalimbali yale mambo ya kupewa cheti yasikuumize sana kichwa. tunafaham usomi wa mtu kwa namna anavyochangia hoja na kupembua. namna anavyotoa masuluhisho kwenye changamoto... mimi nlishaaacha kuulizia ulizia vyetu n.k kuna watu wasomi wa vyeti lakini hawana mchango wowote kwenye jamii.

[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]mim nikijana mdogo wakati huo skuwepo na shule nimesoma lakin si hadi kwa levo za juu je sokoni kipo au kukipata unaweza tumia njia gani
 
Nilikutana na jamaa mmoja wa UDSM- IKS( Institute of Kiswahili Studies) aliniambia Kezilahabi amepata matatizo ya kwenye ubongo, ubungo wake umefuta kumbukumbu zake zote. Mbaya zaidi amepoteza mpaka uwezo wa kuongea, kwa sasa anafundishwa tena kuunda maneno.
 
ni nini kilitokea kwa nguli huyu wa fasihi? ni jambo la kusikitisha sana.

Nilikutana na jamaa mmoja wa UDSM- IKS( Institute of Kiswahili Studies) aliniambia Kezilahabi amepata matatizo ya kwenye ubongo, ubungo wake umefuta kumbukumbu zake zote. Mbaya zaidi amepoteza mpaka uwezo wa kuongea, kwa sasa anafundishwa tena kuunda maneno.
 
na hili ni tatizo kubwa sana. kweli watanzania wengi hawana utamaduni wa kusoma. hata threads za humu ndani hizi za maneno machache kabisa utakuta kuna mtu ambaye unategemea awe na umri wa kujielewa analalamika kuwa ni ndefu.... unajiuliza huyu ana akili kweli na ufahamu wa kutosha? hatupendi kusoma na ndo maana hatuyajui mengi.
Kweli kabisa tumekuwa wavivu ndio maana uwezo wa kuchanganua mambo ni mdogo sana kwa njia hii hatufiki
 
Back
Top Bottom