Karatu: CCM yakata Tamaa, yakubali kuachia Jimbo, Chopa ya Chadema yatikisa

Hivi yale mashetani madogo yaliyokuwa yakidanganya kuwa Lissu na Mbowe hakukaliki na wala hapalaliki yako wapi!!??
Shetani ni muharibifu.
Shetani ni baba wa uongo.
 
Makubaliano ya kuachia Jimbo yamefikiwa leo baada ya Chadema kuvurumisha mikutano ya hadhara isiyo na idadi (Tunatafuta calculator isaidie kujumlisha), ambayo wananchi wameielewa kabisa, Hakika kisicho ridhiki hakiliki!
Mkuu 'Erythro', utanisamehe sana rafiki yangu, lakini nikianza kukusoma kama Lucas Mwashambwa..., sasa sijui nisemeje, kwa sababu huyu mshindani wako yupo daraja la kipekee kabisa ambalo sidhani kuwa nawe unaweza kulifikia.

Unaeleweka tu vizuri toka siku nyingi bila ya ushindani huu mpya. Lakini kama ndiyo njia sahihi ya kuelezea mambo ya chama, mimi ni nani wa kuhoji njia sahihi ya kuvutia wasomaji wako.
 
Mimi sijui kwanini nikiona hiki chama nawaona mabeberu...Mnisamehe ndugu zangu wapendwa!
Itafika mahali wajivue hiyo sura kama kweli wanataka chama kiwe cha waTanzania. Lakini nataka nikuache na ukweli huu: kwa hali ilipofikia CCM sasa hivi, ni bora mara mia hao CHADEMA wafanye kila juhudi za kuwaondoa CCM madarakani bila kujali huo "ubeberu" unaozungumzia wewe.
CCM Bado ni chama Cha watanzania, shida kubwa ni hiyo state capture iliyoikumba
CCM itabaki vipi kuwa chama cha waTanzania, iwapo shida hiyo ya 'state capture' imewanasa? Naona unajichanganya mwenyewe hapa.
 
Siasa cha kuvimba chopa imetikisa ,ndio maana sie tunataka mshinde ila hamtoboi kwa siasa nyepesi kama hizi.
Sisi wananchi ndo tunao umia mkuu. Hao Chadema washinde ama wasipo shinda..sisi wananchi ndo tunateseka na ugumu wa uovu na ukandamizaji wa CCM ,tuache kuwa na ushabiki wa ajabu.
 
Eti "makubaliano"!

Huo bila shaka ni uongo wa kichaga.
 
Viongozi wa ccm waliokubaliana na viongozi wa Chadema kuachia jimbo ni akina nani?
 
CCM Bado ni chama Cha watanzania, shida kubwa ni hiyo state capture iliyoikumba
Ni chama Cha watanzania au ni chama kilichopo Tanzania? Chama Cha watanzania kinachotegemea wizi wa kura na vyombo vya Dola kubaki madarakani, hakuna chama hapo bali genge linaloshurutisha kubaki madarakani.
 
Hatuandiki jf ili kushindana na mtu, wala hatujawahi kuwaza mashindano, lengo letu ni kusambaza habari njema kwa watu wote, ni bahati mbaya kwamba tunatafsiriwa tofauti, bali tunakubaliana na kila tafsiri inayoletwa maana ndio uhuru wa JF huo
 
Sawa Sawa Baadaye CCM Watakimbilia Kwa Msajili Wa Vyama
 
Yani wewe Mirembe Panakuhusu
 
Cheap politics!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…