Kardinali Pengo: Ni kweli Watanzania hatuwezi kuendesha bandari yetu?

Kardinali Pengo: Ni kweli Watanzania hatuwezi kuendesha bandari yetu?

Mimi naongezea

Kama tumeongozw from independence na MCC hadi Leo na hakun jipya n Kam imeshndw kusimamia Taifa had sasa unazan itawez cmamia hao watendj kuw na Tija
 
Ni muda wa kuangalia management companies au raia wa kigeni wenye sifa sahihi na kuwapa kazi za kusimamia taasisi zote za kibiashara zinazomilikiwa na serikali sio bandari tu.

Muhimu ni kuwekeana mikataba ya performance targets.

Juzi Suma JKT imezindua kituo chao mafuta kwa hakiba ya hela zao; kwa sababu hakuna ubadhirifu kama ilivyo kwenye taasisi za serikali.

Kwanini TPDC aina vituo vya mafuta kuwa mshindani ndani ya soko. Moja ya sababu ni kwamba mteja wake mkubwa wa gas hivi sasa ni TANESCO na Dangote. TANESCO toka wameanza kupewa gas na TPDC awajawahi lipa ata centi 5, gas ambayo wanatumia kufanyia biashara na juzi hilo deni la TPDC serikali wamelifuta.

Watu ambao wameshindwa kuwalipa taasisi ambayo inauwazia malighafi wanayozalishia, hapo hapo wameenda kuingia mkataba wa kununua umeme wa jua; kipindi ambacho watakuwa na uzalishaji wa ziada bwawa la Nyerere.

Nimewatolea mfano tu hao TANESCO lakini wote TTCL, ATCL, NHC, TPDC, TRC na ikiwezekana halmashauri kama kuna uwezo wa kuajiri wageni katika nafasi ya wakurugenzi iwe hivyo.

Ifike wakati tuambizane ukweli watanzania hasa wanaoteuliwa na serikali awawezi kazi; unahitajika utaratibu mwingine ukizingatia sector zingine zina multiplier effect kubwa ya uchumi kama bandari.

Serikali isiishie na bandari tu, waende mbele wenyeji awawezi kazi.
Mkuu kuna namn nmekuelewa ILA ni kwamba s/k imeshindw kupm kiwango cha utendaji kaz kbs na kusimamia walio wapa dhamn


Tatz ata hyo MCC yenyew inatakiw isimamiwe, kuna mahali. Tumeoza sio BURE [emoji880]
 
Nakubaliana na wewe kwamba kama Viongozi wetu wanafanya maamuzi ya kubinafsisha au kuruhusu uwekezaji wa nje, kwa imani yao kuwa nchini watu wanawaongoza hawana uwezo, waanze kubinafsisha nafasi zao za uongozi. Wanawajibika kujenga uwezo wa wanaowaongoza na si vinginevyo.
Tukiwapa wageni kila kitu maana yake tumeuza uhuru wa kiuchumi tumebakisha uhuru wa kisiasa. Kitakachofuata mbeleni huko hawa wageni ndiyo watakaoamua nani awe kiongozi, tukifika hapo (na ni jirani sana kufika hapo) tutakuwa pia tumeuza uhuru wa kisiasa na sasa itakuwa ni ukoloni mpya 1000%

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Nakubaliana na wewe kwamba kama Viongozi wetu wanafanya maamuzi ya kubinafsisha au kuruhusu uwekezaji wa nje, kwa imani yao kuwa nchini watu wanawaongoza hawana uwezo, waanze kubinafsisha nafasi zao za uongozi. Wanawajibika kujenga uwezo wa wanaowaongoza na si vinginevyo.
Ukushindwa kuendesha sekta ya bandari hutoweza asilani kuendesha SGR, MGR na CGR. Tujiandae kuwapa Waarabu navyo.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Mfano Dpworld wangekuwa wanatokea Rome Italy..
Angeuliza haya maswali???
Tatizo siyo wanatokea wapi, tatizo ni MoU isiyo na kikomo, kuitisha maoni ya wadau ndani ya masaa 24, kutoa mwanya wa kumilikisha bandari zote Tanzania, kutoa mkataba kwa kampuni inayomilikiwa na nchi wakati na sisi ni nchi tunamiliki kampuni ya TPA.
 
Hicho chama Cha siasa kitakodi wafanyakazi kutoka nje au?
Kama hawa watanganyika,hata kije chama gani ni kazi bure
Ulishawahi jaribu?Kuna siku yoyote chama tofauti na ccm kimetawala Tanzania tofauti na TANU.Mafanikio ya TANU kila mtu anayajua,madhaifu ya ccm kila mtu anayajua na tatizo kubwa ni kuendekeza sera za udini ili nchi isonge.
 
Hatari kubwa Sana ENDAPO viongozi Wetu wa Dini wakitekwa na vikundi vya itikadi za kisiasa.
BAADHI ya Viongozi Wetu wa Dini wanaonekana wamejificha kwenye SHAMBA la karanga lakini Wana agenda yao.

Tatizo hili ni kubwa zaidi katika nchi maskini na limepelekea kukosa watu waadilifu kwenye Nyanja zote. Hivi Kuna asiyefahamu MADUDU ya BANDARI zetu? Kama Container lililobeba madini linapotea bandalini unategemea IPO siku tutatoboa?
 
Nilishamtoa thamani kabisa huyo jamaa, tena afadhali akae kimya tu mnafiki huyo. Maana alichagua kutofautiana na wenzake wote kwa ajili tu kumbeba mwendazake, hata pale wenzake walipodharirishwa na kutiwa misukosuko na serikali ile yeye bado aliamua kuwa upande wake.
Pengo ana elements nyingi sana za udini, alimsumbua sana Kikwete lakini kamwe hakuwahi kuinua mdomo dhidi ya Magufuli, alibaki akimsifu huku akiwapiga vijembe Maaskofu wenzake wa Katoliki walipojaribu kusimama. Akaenda mbele zaidi na kuanza kumtabiria urais Makonda.
Zee la hovyo sana Hili.
Katika watu waliowahi kuwa viongozi wakuu Nchi hii Mzee Kikwete alikuwa na uongozi wa hovyo ever. Wizi Rushwa na kila aina ya upuuzi ulifanyika wakati wake. Mzee Pengo hana element za udini ila wewe naona unazo kwa kiwango cha juu mno. Unatetea kitu ambacho hakifai kwa namna yoyote
 
Katika watu waliowahi kuwa viongozi wakuu Nchi hii Mzee Kikwete alikuwa na uongozi wa hovyo ever. Wizi Rushwa na kila aina ya upuuzi ulifanyika wakati wake. Mzee Pengo hana element za udini ila wewe naona unazo kwa kiwango cha juu mno. Unatetea kitu ambacho hakifai kwa namna yoyote
Pengo ni hovyo, alimkalia kooni Kikwete, tukamuunga mkomo. Alipoingia Magufuli, akamkumbatia Magufuli na Makonda wake. Hakuwahi hata siku moja kumkosoa Mwenda zake kwa lolote, hata Maaskofu wenzake walipojaribu kukosoa yeye alikua kunyume nao, yeye aliendelea kumuunga mkono pamoja na madubwasha aliyoyafanya.

Leo hii anaibukia kwa Samia. Kama aliamua kukaa kimya ni heri angeendelea na ukimya wake tu na tungeuheshimu
Unaponiita mimi mdini sijui unachokimaanisha au haujui ukiongeacho.
 
KUNA MSEMO WA KIINGEREZA UNASEMA HIVI." IF MR KANTAI CAN TIE AND UNTIE A TIE, WHY CAN'T I TIE AND UNTIE A TIE". KWA KISWAHILI. " KWA KANTAI ANAWEZA KUFUNGA NA KUFUNGUA TAI, KWA NINI MIMI NISIWEZE KUFUNGA NA KUFUNGUA TAI. KANTAI AMEWEZA ANA NINI NA MIMI NASHINDWA NINA NINI. Kwa hili la bandari HAPANA, yaani wa tz 60m + hatuna uwezo wa kujiendesha. Kama ni utaalamu tukasomee hata huko uarabuni , kama ni mitambo tununue mmoja mmoja kila mwaka, mbona reli inajengwa. Baada ya miaka say 5 wataalamu tutakuwa nao na mitambo pia. Nini maana ya kujitawala? HUU MSEMO" TUMESHINDWA KUENDESHA, AJE FOREIGNER AENDESHE NI FEDHEA KWA TAIFA". VYUO VIKUU VINATOA WATAALAMU GANI SASA AMBAO "WAO WAMESOMEA, NA SISI HATUKUSOMEA". ETI WANAKUJA NA TECHNOLOGY YA TEHAMA . SI TUKAISOMEE HIYO TECHNOLOGY.HATA IKICHUKUA MIAKA 10 MPAKA TUNAFUZU. ETI WANAKUJA NA MITAMBO. SI WATUUZIE HIYO MITAMBO HATA KAMA NI MTAMBO MMOJA MMOJA TUNANUNUA KILA MWAKA. YAANI BANDARI ZOTEEEEEEE KWELI TUMESHINDWA KUJIENDESHA. HATA ILE YA BUKOBA NA KEMONDO NAPO AJE MTU TOKA NGAMBO KUPAKIA MIKUNGU YA NDIZI NA MAZAO MENGINE? HIVI KWELI KATIKA UENDESHAJI WA BANDARI HIZI KWA KUTUMIA WAWEKEZAJI, AJIRA YA WAZAWA IKOJE. MWEKEZAJI ATAKUWA NA MUDA WA KUANZA KUMFUNDISHA MZAWA ILE TECHNOLOGY NA MITAMBO ANAKUJA NAYO. JIBU NI HAPANA. ATAKUJA NA MAN POWER YAKE.SEMI NA UNSKILLED JOBS NDIZO ZITAPEWA WAZAWA.WAO WANAWEZA VIPI NA SISI TUNASHINDWA VIPI. TUJIATAHIDI KATIKA MAAMUZI ILI VIZAZI VIJAVYO VISIJE VIKAPIGA BAKORA MAKABURI YETU KWA HASIRA YA WATAKACHOKIKUTA.
 
"....huenda Serikali imeona kuna tija. Lakini najiuliza, hivi kweli sisi hatuwezi kuendesha bandari yetu wenyewe? Sielewi viongozi wetu ama wanajitafutia pesa na kuwaacha Watanzania wakididimia ama...yaani hata sielewi maana nashindwa kuelewa!

"....je, pesa ni muhimu kuliko kuwajengea uwezo Watanzania ili wao waweze kuiendesha bandari yao?! Kila mmoja wetu ajiulize hilo."

"....mwenyezi Mungu alimweka binadamu ili aweze kutawala mali na hata pesa. Hilo ndilo jawabu langu la ki maadili."

"Huwezi kumtweza mwanadamu mwenzako kwa sababu ya hela. Ni hilo tu naomba nijizuie kusema zaidi," Pengo.

Kanisa Katoliki TV.
Huyu padri mnafiki sana...anaongea hivi kwa kuwa huyu SI MWENZETU..
 
Ukiwa kiziwi utasikiaje? Wenye masikio na macho tunaukumbuka ule waraka mkali wa pasaka uliotolewa na TEC, uliomkera sana JPM kiasi cha kufikia kuamrisha makanisa yalipe kodi hata kwa vitu ambavyo ni kwaajili ya huduma.

Suluhu ilipatikana baadaye sana, ndipo misamaha ya kodi kwa vifaa vya huduma zinazotolewa na taasisi za dini, ikarudishwa tena.

Lakini pua tuulizane, JPM pamoja na ubabe wake dhidi ya demokrasia na utii wa katiba, aliwahi kuuza rasilimali gani ya nchi?
Wakatoliki walitoa Waraka wa Kwaresima na Waluteri wakatoa Waraka wa Pasaka. JPM alitaka kupata wazimu na kuanzisha vita vya kuvuruga na kukagawa makanisa kwa kutumia wanasiasa, vyombo vya dola na fedha!
 
Back
Top Bottom