It's proven beyond doubt hatuwezi. Tumeendesha zaidi ya miaka 50 bila tija yeyote, majirani wote wamehamia Mombasa na Beira. Bandari yenye potential ya kuchangia zaidi ya 70% ya bajeti ya nchi inachangia 30% tu, mnataka uthibitisho gani zaidi?
Wewe unafikiri sababu ni nini?
Je, suluhu yake ni kuzikabidhi bandari zetu ambazo ni lango kuu la usalama wa nchi yetu kwa mamlaka za nchi nyingine kwa njia na namna anayofanya Rais Samia Suluhu Hassan na kundi lake dogo huko CCM ambao wengi wakiwa ni Wazanzibar?
Wewe hii inakuingia akilini kweli?
Anyway, naweza kukusaidia kujibu swali la kwanza la "unadhani kwanini tumeshindwa kuendesha bandari kwa ufanisi Kwa miaka zaidi ya 50"
Sababu kubwa ni moja tu. Mfumo wetu wa kisiasa, kisheria + kikatiba/kisheria ambao huzaa mfumo wa kiutawala ni mbovu au dhaifu usioruhusu watu kutumia akili, maarifa na ubunifu wao kuendesha taasisi za umma kama bandari nk..
Mfumo wetu wa kiutawala ume - politicize kila kitu. Mfano katika ishu ya bandari, ambayo CEO wake huteuliwa na Rais Kwa mtazamo na utaratibu wa kisiasa, hata hivyo bado hana "power" ya kimaamuzi ya namna kusimamia, kuendesha na ku - manage bandari na badala yake power hiyo iko Kwa aliyemteua kupitia Kwa katibu au waziri wa WIZARA isimamiayo sekta hiyo....
Suluhu ni nini?
Sio kuwapa taasisi zetu wageni toka nchi. Sio kuwakodishia au kuwapa raia wa nchi za kigeni taasisi zetu muhimu kama bandari, Shirika la ndege la taifa, Reli na umeme kuzisumamia, kuzirndesha na kuzimeneji...
Tukifanya hivi, hiyo itakua ni kuuza
National Sovereignty yetu mchana kweupe kama vile sisi sote ni majuha tusiojua kitu..!!
Suluhu ni hii👇👇👇👇
Kubadilisha mfumo wa kiutawala, kisheria/kikatiba ambao utazaa mfumo mpya na imara wa kiutawala wenye focus wa kujenga taasisi imara zenye full maamuzi. Hii itawezekana tu kama wote tutakaa chini na kukubaliana nchi yetu ijitawaleje na Kisha tuweke utaratibu huo mpya ktk document inayoitwa "KATIBA MPYA" na kuachana na hii ya zamani iliyotuletea matatizo haya..!!