"....huenda Serikali imeona kuna tija. Lakini najiuliza, hivi kweli sisi hatuwezi kuendesha bandari yetu wenyewe? Sielewi viongozi wetu ama wanajitafutia pesa na kuwaacha Watanzania wakididimia ama...yaani hata sielewi maana nashindwa kuelewa!
"....je, pesa ni muhimu kuliko kuwajengea uwezo Watanzania ili wao waweze kuiendesha bandari yao?! Kila mmoja wetu ajiulize hilo."
"....mwenyezi Mungu alimweka binadamu ili aweze kutawala mali na hata pesa. Hilo ndilo jawabu langu la ki maadili."
"Huwezi kumtweza mwanadamu mwenzako kwa sababu ya hela. Ni hilo tu naomba nijizuie kusema zaidi," Pengo.
Kanisa Katoliki TV.
Tatizo la nchi yetu siyo kutokuwa na watu wenye uwezo na haiba ya kusimamia Sera, Sheria na kanuni zinazoongoza nchi, Wala hatuna shida ya wasomi wanaoweza kutunga mitaala ya elimu ya kufaa kwa maendeleo ya taifa. Tatizo nchi Ina wachache wanaotupangia Nani awe Nani, hata Kama Hana maadili kuanzia nyumbani kwake, hana "record" ya ubobevu wa kivitendo popote.
Mtu hawezi kuwa na mapenzi ya kweli kumsaidia jirani wakati watu wa nyumbani kwake Wana hitaji hilohilo. Ukiona imetokea hivyo, ujue Kuna agenda isiyojulikana.
Mimi nafikiri usimamizi Makini na wenye viwango vya uadilifu ndio hitaji kuu katika nchi yetu. Kuwajibisha wanaotumia vibaya madaraka yao kwa Uma bila huruma ni nidhamu muhimu tunayokosa.
Kama haya yangekuwa yako katika mstari wake, hakika tusingehitaji mwekezaji katika maeneo nyeti kiusalama. Naomba serikali usimpe nafasi spika mstaafu kuwa nabii wa kweli.
Hata Katiba iliyopo na udhaifu wake, ikiwa mikononi mwa waungwana ingeweza kutupeleka mbali Sana. Kiongozi yeyote asiyetosheka atatumia nafasi yake kuleta mengi yasiyofaa.
Hapa sijamhusisha raisi wangu. Binafsi siamini kinachoendelea ni Haiba ya raisi wetu, Ila ikithibitika kuwa Kuna udhaifu unaopigiwa kelele leo, atakuwa ameingizwa kimtego kuharibu sifa yake njema kwetu sisi tusiojua kuchambua Mambo kwa kina, ambao ndiyo wengi.
Haishangazi kuwa tunajiandaa kimrudisha madarakani kwa Kura zetu 2025. Lakini kwa habari ya bandari zetu na usalama wa Maisha yetu na vizazi vijavyo, tunasukumwa nyuma maili nyingi. Kubinafsisha bandari (eneo nyeti kimaslahi na kiusalama) kwa mtindo huo kumetuingiza kwenye Mashaka makubwa.
Hata hivyo, katika Hali ya kumaanisha, binafsi na kwa kuhamasisha watu wengine tunamuombea raisi na serikali yake (hasa rais) wafungue macho sawasawa ili waweze kuona hila za watu wa nje wenye Nia mbaya na taifa hili tangu zamani. Jambo hili kwa wale wenye ufahamu wa kadri, wametiwa hofu kubwa, naomba serikali isipuuze hofu hii.
Wala isijisikie vibaya wananchi wakihoji Jambo hili kwa nguvu, Wala isilazimishe hata Kama Lina maslahi - hiyo siyo njia pekee ya maendeleo.
Amani usalama na ustawi wenye uwiano vipewe vifikiriwe kwa kina na kwa nguvu zote. Hiyo itatoa ushawishi kuwa Kuna Nia njema Ila ni kasoro za kiutendaji zilizojitokeza.
Ambazo pia zinaweza kuwa kiashirio Cha uwezo duni wa washauri na watendaji waliohusika katika swala hili.