Kariakoo haina umuhimu kwa uchumi wa nchi kama tunavyo aminishana Bongo lala

Ujinga umetuzidi kama mtoa hoja alivyoeleza. Kariakoo ni muhimu kwa TRA kudai kodi sio kwamba ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi. Ni soko muhimu kwa uuzaji wa bidhaa za nje kwa hivyo ni mhali muhimu kwa taifa kutoza kodi na kodi kubwa kwa zile bidhaa zinaleta ushindani usio sawa kwa zile bidhaa tunazalisha nchini.
 
Nchi yako haina viwanda vya kutosha. Madini, Utalii, Kilimo bidhaa za utendaji zinatoka hapo Kariakoo. Sasa jiongeze boss.
 
Kariakiakoo ni makao makuu ya kituo uapnde wa Tanzania cha kupromote products za nje hasa kupromote viwanda vya China na kupelekea China kutoa ajira zaidi kwa wachina.
Kariakoo imekuwepo hata kabla ya large scale China-made goods importation

Kariakoo imekuwepo tangu enzi za electronic devices nyingi zikiwa ni za kutoka Japan

Kariakoo ni soko la bidhaa kutoka kokote duniani ingawa asilimia kubwa ya bidhaa ni za China. Kusema Kariakoo inapromote viwanda vya China unakosea sana.

China hawaifahamu Kariakoo kinachofamika na China ni kituo cha biashara cha pale Ubungo.

Hapo Ubungo, Mchina anaanzisha exhibition trading platform, cros-border E-commerce platform, commodity procurement platform kwa
Made in China goods only

Una hoja nzuri ya kutaka kuendeleza viwanda vya ndani ili kupunguza uingizaji wa bidhaa kutoka nje hilo pekee ndilo nakuunga mkono.
 

Sawa Mkuu, lakini tatizo ni Serikali yetu sikiveu ndiyo imetujengea uchumi wa design hiyo. Hayo unayoyasema ya uchumi wa viwanda siyo uchumi wetu labda in our dreams.
 
Uko sahihi. Pia biashara za Kariakoo hazina msaada wowote kwa vijana kuongeza maarifa yoyote kwenye fani walizosomea. Uchuuzi hauna future kabisa. Vijana wa IT, Mining, Kilimo, na fani zingine wamekuwa wachuuzi wa bidhaa zinazotengenezwa na vijana wenzao wa China.
 
Una uwezo mdogo wa kujenga hoja.

Ukisema kariakoo haina umuhimu kwa uchumi, uchumi ni nini na unajengwa na vitu gani. Kwa akili yako uchumi ni viwanda tu nani alikukaririsha uchumi ni viwanda tu.

Ilala ndio sehemu inachangia aslilimia kubwa ya makusanyo ya kodi nchi nzima hii TZ na mapato hayo ndio yanaenda kuunda pato la Taifa la ujumla. Unasemaje halina umuhimu hizi akili.

Viwanda hio ni sector nyengine kabisa initiate kujengwa kwa viwanda kama factor moja ya kiuchumi ila usi initiate factor kwa ku-undermine factor nyengine. Karikoo ni TRADING ECONOMY ni uchumi unaojitegemea na hakuna nchi isiyofanya TRADING meli haziji TZ tu daily Meli zipo baharini kupeleka bidhaa kila sehemu ya Dunia.

Kama unawaza Uchumi ni kiwanda una safari ndefu kujifunza uchumi.
 
Kariakoo kuna uhusiano gani na masuala ya kusoma, you guys inabidi mounzike kila kitu kuingiza wasomi.
 
Viwanda vinakufa kwa sababu ya kodi na wanasiasa kua wafanya biashara juzi kiwanda kinauzwa watu wajenge nyumba urafiki achana na viwanda vingine vingi vimejifia mashirika mengi pia yamejifia machache yanajikongoja km Tazara na Mengine mengi.Serikali imekaa kutafuta kodi tu hawawazi kujenge uchumi kwa mwananchi kwa kuongeza thamani ya bidhaa zetu kwa kujenga viwanda.Vijana wengi wanaisgia kua machinga hata kusimamia tu kilimo basi vijana wajiajiri huko wameshindwa ila watu wakilima na kuvuna unakuta vizuizi lipa tozo mara hiki.Tanzania hatuna viongozi .
 
Haiondoi neno Dampo, Kariakoo ni Dampo la products za kigeni, shida wana siasa wanawadanganya sana, mitaji haibadili ukweli, maada ngumu huwezi elewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…