Kariakoo hakuna machimbo tena, kwa atakayepuuza sitaongea tena

Kuna duka niliingia hapo mkwajuni yaani jamaa hana tamaa yeye kaamua kuuza kama super market anabandika na price tag kabisa hataki kukaushana mate na wiziwizi usio na kichwa wala miguu.Hii itapendeza hapo kariakoo watu wafanye biashara kama jamii zilizostaarabika bandikeni price tag mtu ajikadirie mwenyewe hakuna mbambamba na foleni bila sababu.
 
Kariakoo wanakupokea jinsi unavyoenda, ukitaka usisumbuke kabla ya kwenda Kariakoo jaribu kusurvwy bei mtandaoni. Ukifika huko ujue kabisa lasivyo itauziwa mara mbili yake.
Nilienda kununua sabufa tena duka famous kabisa na bei yake nilikuwa naijua, hata imstagram page yake kaweka bei, kufika pale mawinga wakanipokea sabufa ya 175k wakaniambia 300k nikawaambia straight bei yake ni 175k najua bado wanabisha mwisho 270k.
Nikataka kusepa zangu ndio mwenye duka akaniambia njoo uchukue, yaani ni kero mno
 
System hiyo ni ya nchi zilizoendelea,kwa TZ ni mlimani city tu,bei unaikuta kwa kitu unachotaka kununua
 
Yaani wewe jamaa unatetea upuuzi bila Aibu Tena kwa kujiamini kweli....
Mimi napiga vita uwinga kabisa kwa sababu ni utapeli mtupu, uwinga hauna tija yoyote kwa wafanyabiashara au wateja.
Subiri ukutane na majitu kama huyu jamaa wa kujiita Kitali yanakwambia eti yamekuza biashara zao kupitia mawinga, yaani biashara zao zimekuwa kupitia vibaraka wao wanaowatapeli na kuwaibia wateja...

Uwinga ni Moja sababu kwanini bidhaa zetu kwa asilimia kubwa huwa tunauziana sisi wabongo tu, raia wa mataifa mengine hawataki kabisa huu ujinga, ukienda hapo Zambia hata kwenye masoko tu ya kawaida Kila bidhaa imewekewa kabisa price tag, yaani huna haja ya kuuliza bei ukifika dukani... Njoo bongo Sasa yaani muuzaji Yuko tayari akamuite winga ndio aje akuuzie hata kama umemkuta yeye dukani.. ovyo sana
 
Sasa kama ni hivi basi haukuwa na aja ya kutoa maneno yaliyojaa fedhuri na dharau kwa mleta mada....

Kama wewe unaona ni sawa tu kununua kitu ambacho Kiko overpriced kwa lengo la kutaka na wengine wapate kwa sababu kipato chako kinaruhusu, basi wasikilize na waheshimu wale ambao Bado Wana bargain mpaka kwenye lowest price line, maana hapa duniani binadamu hatufanani kama tu ilivyo kwa vidole.

Kuhusu uwinga Bado nakwambia uwepo wao ni sumu na pigo kubwa sana kwa wateja, na ndio chanzo Cha kupunguza kwa customer base ya Eneo husika, mfano kama Mimi leo hii siwezi kabisa kwenda Karume kutokana huu ushenzi, yaani unaingia tu pale mlangoni unapokelewa na mawinga kama watano na Kila mtu anakuongelesha, haya unafika golini suruali moja ya mtumba wanakutajia bei eti 35,000/= kweliii??? Hapo unategemea Kuna mtu anarudi Tena Hilo Eneo.?

Hao mawinga wenu wanawaharibia biashara sana wewe endelea kuwatetea tu hapa
 
Ukitaka kuishi vizuri kariakoo tafuta winga ambaye yuko royal kwako,winga atakuumiza iwapo hamjuani wala hamjawahi kufaana kwa chochote,winga uliyewaji kumfaa jambo lake hanaga kinyongo,mimi mizigo yangu nachukua kwa mawinga wanaonipa hadi bei za kiwandani china pamoja na go dwlown zao nina access ya kuingia,ishu ni aina ya koneksheni uliyonayo.
 
Ona Sasa ndio maisha gani haya??? Kwamba hela tuitafute kwa shida na hata jinsi ya kuitumia tuanze kutafuta connection hili itumike kwa namna sahihi?? Like serious?

Nikisema hii jamii yetu ya kibongo ni jamii ya ovyo sana muwe mnaelewa, hebu ona vitu ambavyo tumevi normalize.. yaani vitu vya oovyoo
 
Kabisa jamii ya hovyo sana.

Yani mtu anatoa ushauri wa kipumbavu na anaona sawa tu.

Sasa kwa hali ya kawaida inawezekana vipi kila mtu awe na winga wake ambaye yupo royal.

Ni kitu kisichowezekana ni pia ni usumbufu kwa mteja.

Muhimu watu wakatae kwenda Kkoo.
 
Winga huwezi kumkwepa

Winga wapo dunia nzima

Hata Tajiri namba moja duniani Jeff Bezos ni winga.

Hata kampuni ya Nike yenyewe ni winga wa vifaa vya michezo. Ila haina kiwanda hata kimoja.

Kampuni ya Gucci ni winga
Mifano yako ni ya kiduwanzi sana na Haina mshabiano wowote wa kimantiki na hao vibaka wenu wa kiriakoo.. japo wewe unajiona umeandika bonge la point
 
Royal--loyal

Ova
 
Watu hununua au kuuza kitu kwako kwa sifa kuu tatu
1.Kukufahamu(Know how)
2.Kukupenda(Like)
3.Kukuamini(Trust)

Nje na hizo sababu,niamini mimi,ukiachilia mbali ubantu wa wabantu utapigwa tu kwenye bei maana utadondokea kwenye myego wa price discrimination.

Biashara ni mchezo wa supply chain na utele wa taarifa,sifa mojawapo ya mfanyabiashara ni kuficha taarifa.Tafuta kitabu cha Robert Kiyosaki kinaitwa Guide to investing kitakusaidia.

Kwenye mnyororo wa usambazaji inayegemea na;-
1.Taarifa ulizonazo
2.Nani unahusiana naye
3.Aina la soko unalotaka kulihudumia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…