Kariakoo hakuna machimbo tena, kwa atakayepuuza sitaongea tena

Yaani jamaa anavyoelezea Yuko very proud as if ni jambo la kijivunia sana na wakati ni ujinga tu Tena ujinga unaotia uzuni.

Yaani kwamba Sasa hivi tuanze kuumizwa kichwa jinsi ya kupata hela na pia vile vile tuumize kichwa kuwatafuta hao mawinga watakaotuuzia vitu kwa bei sahihi, kwa sababu tu hakuna usimamizi kwenye suala Zima la bei elekezi??

Kwa akili hizi wakenya wakitutukana huwa nawaona wako sahihi wakati mwingine...

Sasa hivi Mimi baada ya Karume sehemu nyingine ambayo sitoenda kununua bidhaa yoyote ni huko kariakoo, acha tu nianze kuagiza AliExpress.
 
Watu wenyewe ndiyo wanawaendekeza hao mawinga
Unaenda dukani,duka unaliona
Hakuna haja wala kupoteza muda kumsikiliza winga

Ova
Mawinga wanafosi sana kingi.

Ukifika tu dukani hata kama ulienda mwenyewe winga lazima akudandie na wenye maduka yao wanakuacha na winga uangaike nae akupige.

Yeye katulia pembeni tuli.
 
Mimi kariakoo niliacha kwenda baada ya kuona mahitaji yangu mengi nayapata maduka ya mtaani kwangu kwa gharama nafuu kuliko kkoo nikastuka nikaacha kabisa kwenda.

Labda nitafute kitu nikikose kabisa maduka ya mtaani ndo ntaenda huko kwa mawinga(wezi)wanaopandisha bei kuliko kawaida.
 
Wabongo wengi kwenye biashara uwa tunaangalia tunachopata wakati huo tu hata kama uko mbeleni kutakua na risk,hatujui biashara aisee,leo uniuzie famba unadhani kesho nitakuja!
Wabongo wengi kwenye biashara zao huwa wanapata wateja wapya Kila siku, na siku hao wateja wapya wakianza kuhadimika anafunga biashara na kurudisha fremu kisha anaanz kusingizia Kuna watu wamemuonea wivu na hivyo wameroga...

Mbongo anafanya baishara kwa kuangalia hela anayoingiza leo tu, Wala Hana muda wa kutengeneza customer base ya kudumu
 
Umechukua uamauzi sahihi kabisa mkuu.

Mimi mwenyewe Kuna siku nimenunua jeans zangu mbili nzuri kabisa kwa @16,00/= kwa jamaa alikuwa anatembeza mitaani, wiki Moja baadae nikaenda Kariakoo jeans za aina ile ile nikaambiwa bei ya reja reja ni 22,000/= tangia hapo sijanunua Tena nguo Kariakoo.

Acha tubaki kununua vitu mitaani, hao vibaka wa Kariakoo acha wawe wanaangaliana tu na wamiliki wa maduka kwanzia hasubui mpaka jua linazama.
 
Biashara mimi nimeingia kkoo nimeikuta hivyo japo nipnipo nimetoka nimeiacha hivyo. Unataka kupata hela usiwabanie watu biashara haiwez kufa kwaajili ya winga mzee. Biashara inakufa kwa kukosa mahtaji ya watu. Biashara ni game ya kuwin mindset za watu. Unaleta kisichopatika popote hawana jins zaid ya kukufuata na unacheza na wakati ili wasizoee aina moja ya kazi. So unatengeneza kitu kwenye akili yao kinachoamin uwezo wako basi. Miaka 5 unabadilika. Ukiona unazeeka unatengeneza management fungua branch unapeleka akili mpya front we unakaa pembeni kudhamin pambano.
 
Aisee hapo kwa bold umeongea kwa uchungu sana japo ndio uhalisia wenyewe
 
Sawa nimekuelewa winga mstaafu...
 
Mawinga wanafosi sana kingi.

Ukifika tu dukani hata kama ulienda mwenyewe winga lazima akudandie na wenye maduka yao wanakuacha na winga uangaike nae akupige.

Yeye katulia pembeni tuli.
Biashara kama hizo ni za kishz
Tu,ngoja dawa yao inachemka
Ngoja ubungo pamefunguliwe
Kuna kitu wataona tofauti huko
Walaji wote watakimbilia huko ubungo

Ova
 
Shida inaanzia hapo mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…