Kariakoo hakuna machimbo tena, kwa atakayepuuza sitaongea tena

Kariakoo hakuna machimbo tena, kwa atakayepuuza sitaongea tena

Kariakoo kila unaekutana nae usimuamini..

Hao wafanya biashara wenyewe hawana uhakika wa bei zao🤔

Unamuuliza bei ya bidhaa (mf. Kiatu) bei gani anakwambia 40k ukighairi ukitaka kuondoka utamsikia anashusha bei tena utaskia 'basi lipia 35k boss'😁

Ukirudi kuongea nae unachkua kwa 10k. 😂😂😂
 
Usijisumbue kwenda kariakoo kununua mzigo ukidhani Kuna bei nafuu
Kariakoo wamejaa wajanja na madalali tu
Unaweza ingia kwenye duka ukamkuta mwenye duka ukamuuliza bei akakuelekeza uongee na vijana wake wakuumize
Nyie watu situka Kariakoo hakufai kabisa, mawinga wameharibu uaminifu
Matajiri wanauchukulia wateja kama wajinga, wanajua kuwa mtaenda tu
Sasa naomba niwape machimbo mapya Kwa Dar

1. Kwa wale wa electronics nenda Tegeta pale Kibo complex utapata bei ambayo Kariakoo haipo

Pia nenda Mbagala rangi Tatu utapata electronics zote, kuanzia Tv, simu, cable

2. Nguo nenda Mwenge au Makumbusho

3. Mitumba
Usijaribu kwenda Karume au Ilala tena
Kwa mitumba ya bei nafuu, mabalo za rejareja nenda Tandika, Temeke, Tandale na Mwenge

Kanda ya ziwa, machimbo yapo Katoro

Kwa machimbo mengine, tujaribu ku share.
Ila chonde chonde kariakoo utaishia kupandiliwa na kupigwa bei ya maana
Kariakoo nilikuwepo Jana, nikahairisha kuchukua mzigo kisa mawinga
Huu uzi wako ni takataka.
 
Kwa sisi tulioko mikoani unatusaidiaje? Haujachukua mawasiliano?
 
Mi niko kkoo huu ni mwaka 25 mkuu na kwasasa soko linaendeshwa na mawinga. Usipokubali mabadiliko ni kwamba umejiandalia kifo. Na kwa taarifa yako kkoo inategemea zaid wateja wa nje ya nchi sio ndani. So wewe endelea kuishi kwa kukariri maisha wakat wenzio wanavuka ukija kustuka uanze kuilaumu serikali. Maisha lazima ule na watu babu kama unataka kwenda mbali. Kama unataka kwenda karibu kula mwenyewe. Mi nawatumia winga tangu naanza biashara kkoo na wao wanakula na mimi natembea. Winga wananipa idea mipango na sote tunapata maisha yanaenda. We jifanye boss ubaki kuitwa mwenye duka milele. Ctaki huo upuuzi
 
Me nataka winga wako umlipe mshahara atafute wateja walioko majumbani
Yaani mtu kajileta dukani kwako kununua simu ambayo unauza labda laki 4 wewe unamweka mteja wako midomoni mwa winga wanampiga laki 7 Bado unaona ni raha
Wafanyabiashara wakimataifa watawahama wawe wanachukua mizigo miji mingine
Bro hujui how things work. Biashara zote dunian zinafanyika online na wakat mwingine huwez kuwa na watu wote online so unakuta una mawinga kama 50 kila mtu ana wafuasi elfu 4 tuseme na wanakuja dukan kupiga picha kuposti so ndani ya nusu saa kila Winga anakuja huyu anataka pcs 30 huyu kumi huyu 20 na wanakuja kuchukua mizigo kupelekea wateja huko walipo so yeye anapata cha juu na wewe unapata chochote kitu. Ndivyo mfumo wa biashara ulivyo dunian lazima awepo mtu wa kati anaerahisisha kazi zako ziaende. Kwa mtu ambae amesafir anajua hasa viwandani. Biashara ni agent mzee. Na hiyo ya dukan kusubirishwa ni kawaida kkoo mi tangu naanza biashara vijana wanafanya hivyo miaka hiyo we umestuka leo na hata wagen wanajua. Kwa mfano mimi biashara yangu ni groups za whatsp za wateja wangu kutoka congo zambia Zimbabwe kenya malawi Rwanda Burundi comoro msumbiji nk. So mzigo ukitoka natoa sampo store narusha kwenye whatsp kila mtu anaweka order humo humo kutoka hizo nchi na wanaingiza mizigo kwenye account yako unawatumia mizigo yao. Simpo mzee life ishabadilika kaka. Mimi naweza kuuza mizigo nikiwa hukuhuku china ikawafuata wateja walipo na wakaniingizia mpunga wangu kwenye account tu. So usikariri maisha mzee pinduka maisha na yenyewe yanavyopinduka waache wenye kibarua cha kulaumu walaumu kila mtu apigane vita vyake. Ukiona umestuka ujue kuna mwingine ni mtaji, biashara ni mchezo wa sanaa kuna wakati unafungwa na kuna wakat unafunga.
 
Sijawahi kuona jitu jinga kama wewe
Kwamba ku bargain bei ni umasikiy?
Naweza kuwa mjinga kwako lakin mjanja kwa wengine bado haijanipunguzia kitu. Kuna tofauti ya kubagain na kunegoshieti mzee. Nakusanua sasa ukikataa shauri yako. Katika kitu muhimu kuliko vyote ukimtoa Mungu na uzima wako kitu kinachofuata ni. Muda na maamuzi. Ukikosea hapo bye bye. Usiseme sijakusanua.
 
Mi niko kkoo huu ni mwaka 25 mkuu na kwasasa soko linaendeshwa na mawinga. Usipokubali mabadiliko ni kwamba umejiandalia kifo. Na kwa taarifa yako kkoo inategemea zaid wateja wa nje ya nchi sio ndani. So wewe endelea kuishi kwa kukariri maisha wakat wenzio wanavuka ukija kustuka uanze kuilaumu serikali. Maisha lazima ule na watu babu kama unataka kwenda mbali. Kama unataka kwenda karibu kula mwenyewe. Mi nawatumia winga tangu naanza biashara kkoo na wao wanakula na mimi natembea. Winga wananipa idea mipango na sote tunapata maisha yanaenda. We jifanye boss ubaki kuitwa mwenye duka milele. Ctaki huo upuuzi
Very interesting. Ina maana wafanyabiashara halali wa Kariakoo ni mateka kwa mawinga?Hapa mpuuzi ni nani.
 
Back
Top Bottom