Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Wasinisumbue sasa nikiwa natafuta bidhaa Kariakoo, wakae mbali na mimi.Sio jukumu lako kuwapangia cha kufanya.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wasinisumbue sasa nikiwa natafuta bidhaa Kariakoo, wakae mbali na mimi.Sio jukumu lako kuwapangia cha kufanya.
Watu wanakuja funga mzigo kariakoo hapo hapo, shida moja ya kariakoo lazima uwe na mwenyeji....🐒Hivi hapo Katoro bidhaa wanaagiza wapi mkuu
Nipe chimbo la hiyo bei ya kutupa kwa hivyo vifaa, maana km ni kuzunguka nilizunguka sana tu, kwenda mlimani nikakuta bei hazipishani kihivyo na vingine bei zinalinganaSio kweli inategemea umekutana na nani ila nakuhakikishia kariakoo kuna bei za kutupa
Wewe bado huwajui matajiriKiatu kimoja unabargain hakuna tajir anafanya huo ujinga ukimuambia buku atakuambia nakupa 800 nipe vinne au ukienda duka lolote kubwa bei iko pale sio kubargain. Kama ni biashara ya kati mnabargain. Tajir gan ana muda wa kukaa chini nusu saa anaomba kupunguziwa huyo sio tajir jombaa. Ingekuwa biashara za uzalishaji au za kati sawa sio biashara ya mlaji wa mwisho unakuta mtu anakaa dakika 20 apunguziwe buku huku ananunua kiatu kimoja huyo sio tajir mzee. Tajiri ni muda hawanaga muda.
Soko la Ubungo la Mchina litakuwa la jumla sio rejarejaMawinga wajinga aisee watakuja na hapo na watapaharibu kabisa!
Si unakumbuka kkoo ya zamani?
Haya majinga ni kama mainzi ya chooni, yatakuja tu na mchina si unamjua alivyo, atawapokea tu
Hii sasa ni mimi mwenyewe.Wala sio uongo, niliuliza nyundo ya kg 10 dukani kariakoo nikaambiwa bei ni 100k, nikapita mtaani jamaa ameweka chini hiyo hiyo nyundo na makolokolo mengine, nikauziwa kwa tsh 35k
Kwa hiyo waendelee kutanua mjini kwa athari ya mfumko wa bei.Sio jukumu lako kuwapangia cha kufanya.
🤣🤣🤣🤣 Yanakera au sioMawinga yataenda na huko, kwani Kariakoo yalitokea wapi?
Pesa hz n balaaaNa wanatumia miti shamba, wanaongea na mteja huku mkono mmoja uko mfukoni. Huko mfukoni wanaminya kihirizi flani hiv kinaitwa Kiminyio! Mteja hakatai bei
kinachozungumzwa hapa ni kwamba kitu fulani bei ya kuuza rejareja ni wastani wa elfu sitini (60, 000) lakini unaingia dukani unauliza bei kwakua ni mgeni unaambiwa laki 1 (100, 000). huu ni wizi haijalishi laki naimudu ama lahUmasikin ni mbaya sana aisee. Nyie ndio mkiona mtu kanunua range rover mnamlaumu kwa kununua gari inayotumia mafuta. Mzee ukiona unanunua kitu kwa kubagain ujue hali yako ni mbaya pambana mkuu.
Okkinachozungumzwa hapa ni kwamba kitu fulani bei ya kuuza rejareja ni wastani wa elfu sitini (60, 000) lakini unaingia dukani unauliza bei kwakua ni mgeni unaambiwa laki 1 (100, 000). huu ni wizi haijalishi laki naimudu ama lah
Matajir wa bongo mzee. Hao sio matajiri ni watu wenye vipato vya kati boss. Tajir hana muda nakuhakikishia. Ni sawa na mwanaume uende dukan na mkeo. Kitu hicho hicho atazunguka maduka yote ili apunguziwe bei wakat mwanaume huna mudaWewe bado huwajui matajiri
Uko wapiVipodozi hasa vya wanawake... Na uchache kwa wanaume
Ni ya mtumba hayo mashuka? Itabidi niende siku mojaKuna siku nilikuta mashuka tandika bei kitonga,niliyakusanya kama yote,kufika home nilipomuambia Wife bei niliyonunulia,siku ya pili tulirudi wote kuyakusanya tena,tandika ipewe maua yake,kikubwa wangese mawinga wasiende kupaharibu,soko la ilala lilikua zuri sana kwa jeans za mtumba ila now ni ghari mno,jeans za bei rahisi ukiiotea kwa wale wanaotembeza mkononi
Ndo maana mzigo unatoka bandari yetu unaenda nje ila huko nje unaupata kwa bei nafuu kuliko hapa sababu ndo hii.Mi niko kkoo huu ni mwaka 25 mkuu na kwasasa soko linaendeshwa na mawinga. Usipokubali mabadiliko ni kwamba umejiandalia kifo. Na kwa taarifa yako kkoo inategemea zaid wateja wa nje ya nchi sio ndani. So wewe endelea kuishi kwa kukariri maisha wakat wenzio wanavuka ukija kustuka uanze kuilaumu serikali. Maisha lazima ule na watu babu kama unataka kwenda mbali. Kama unataka kwenda karibu kula mwenyewe. Mi nawatumia winga tangu naanza biashara kkoo na wao wanakula na mimi natembea. Winga wananipa idea mipango na sote tunapata maisha yanaenda. We jifanye boss ubaki kuitwa mwenye duka milele. Ctaki huo upuuzi
"We leta mteja wako bei nauza laki 4 ila hata ukija na wa milioni cha juu chako" Alisikika mkinga akimpa maelekezo winga wa kimachame.Me nataka winga wako umlipe mshahara atafute wateja walioko majumbani
Yaani mtu kajileta dukani kwako kununua simu ambayo unauza labda laki 4 wewe unamweka mteja wako midomoni mwa winga wanampiga laki 7 Bado unaona ni raha
Wafanyabiashara wakimataifa watawahama wawe wanachukua mizigo miji mingine