Kariakoo hakuna machimbo tena, kwa atakayepuuza sitaongea tena

Wewe bado huwajui matajiri
 
Wala sio uongo, niliuliza nyundo ya kg 10 dukani kariakoo nikaambiwa bei ni 100k, nikapita mtaani jamaa ameweka chini hiyo hiyo nyundo na makolokolo mengine, nikauziwa kwa tsh 35k
Hii sasa ni mimi mwenyewe.

Nimeenda kununua jeans naambiwa 35000.

Nimeingia mtaani jeans hiyo hiyo nimeikuta kwa 18000 nikashangaa sana.
 
Umasikin ni mbaya sana aisee. Nyie ndio mkiona mtu kanunua range rover mnamlaumu kwa kununua gari inayotumia mafuta. Mzee ukiona unanunua kitu kwa kubagain ujue hali yako ni mbaya pambana mkuu.
kinachozungumzwa hapa ni kwamba kitu fulani bei ya kuuza rejareja ni wastani wa elfu sitini (60, 000) lakini unaingia dukani unauliza bei kwakua ni mgeni unaambiwa laki 1 (100, 000). huu ni wizi haijalishi laki naimudu ama lah
 
kinachozungumzwa hapa ni kwamba kitu fulani bei ya kuuza rejareja ni wastani wa elfu sitini (60, 000) lakini unaingia dukani unauliza bei kwakua ni mgeni unaambiwa laki 1 (100, 000). huu ni wizi haijalishi laki naimudu ama lah
Ok
 
Wewe bado huwajui matajiri
Matajir wa bongo mzee. Hao sio matajiri ni watu wenye vipato vya kati boss. Tajir hana muda nakuhakikishia. Ni sawa na mwanaume uende dukan na mkeo. Kitu hicho hicho atazunguka maduka yote ili apunguziwe bei wakat mwanaume huna muda
 
Ni ya mtumba hayo mashuka? Itabidi niende siku moja
 
Ndo maana mzigo unatoka bandari yetu unaenda nje ila huko nje unaupata kwa bei nafuu kuliko hapa sababu ndo hii.

TRA ashibie hapo, Mwenye duka ashibie hapo, Bank aliyekopesha mtaji ashibie hapo, Winga ashibie hapo. Kwanini bei isiwe juu?
 
"We leta mteja wako bei nauza laki 4 ila hata ukija na wa milioni cha juu chako" Alisikika mkinga akimpa maelekezo winga wa kimachame.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…