Kariakoo hakuna machimbo tena, kwa atakayepuuza sitaongea tena

Kariakoo hakuna machimbo tena, kwa atakayepuuza sitaongea tena

Kiatu kimoja unabargain hakuna tajir anafanya huo ujinga ukimuambia buku atakuambia nakupa 800 nipe vinne au ukienda duka lolote kubwa bei iko pale sio kubargain. Kama ni biashara ya kati mnabargain. Tajir gan ana muda wa kukaa chini nusu saa anaomba kupunguziwa huyo sio tajir jombaa. Ingekuwa biashara za uzalishaji au za kati sawa sio biashara ya mlaji wa mwisho unakuta mtu anakaa dakika 20 apunguziwe buku huku ananunua kiatu kimoja huyo sio tajir mzee. Tajiri ni muda hawanaga muda.
Sisi matajiri hatuwezi kuja k/koo kununua bidhaa huwa tunaagiza direct from kiwandani hata vyakula tunanunua kwa jumla we ushawahi kuona tajiri gani amekuja k/koo kununua Tv?we endelea kuumiza masikini wenzako na hao ma Fullback wenu.
 
MAWINGA wa karume,..wanaboa Sana..Kuna siku ilibidi niache kabisa kununua nilichofata baada ya kuona shobo nyingi..ikabid nijifanye bubu tu..nawaeleza kwa kutumia ishara..mwisho wa siku nkaondoka nkaelekea mtaa mwingine kabisa
Kuliko niende Karume na yale makelele bora niingie Tandale na Manzese tu
 
Usijisumbue kwenda Kariakoo kununua mzigo ukidhani Kuna bei nafuu
Kariakoo wamejaa wajanja na madalali tu
Unaweza ingia kwenye duka ukamkuta mwenye duka ukamuuliza bei akakuelekeza uongee na vijana wake wakuumize
Nyie watu situka Kariakoo hakufai kabisa, mawinga wameharibu uaminifu.

Matajiri wanauchukulia wateja kama wajinga, wanajua kuwa mtaenda tu.

Sasa naomba niwape machimbo mapya Kwa Dar

1. Kwa wale wa electronics nenda Tegeta pale Kibo complex utapata bei ambayo Kariakoo haipo

Pia nenda Mbagala rangi Tatu utapata electronics zote, kuanzia Tv, simu, cable

2. Nguo nenda Mwenge au Makumbusho

3. Mitumba
Usijaribu kwenda Karume au Ilala tena
Kwa mitumba ya bei nafuu, mabalo za rejareja nenda Tandika, Temeke, Tandale na Mwenge

Kanda ya ziwa, machimbo yapo Katoro

Kwa machimbo mengine, tujaribu ku share.

Ila chonde chonde Kariakoo utaishia kupandiliwa na kupigwa bei ya maana.

Kariakoo nilikuwepo Jana, nikahairisha kuchukua mzigo kisa mawinga
Kweli kabisa, kuna siku nimeenda kariakoo kununua vifaa vya finishing kwenye furniture garama niliyotumia siku hio kwa vifaa hivyo ilikua imezidi 50000 siku niliponunua pale tegeta, kariakoo sipotezi muda tena kwenda huko.
 
Wala sio uongo, niliuliza nyundo ya kg 10 dukani kariakoo nikaambiwa bei ni 100k, nikapita mtaani jamaa ameweka chini hiyo hiyo nyundo na makolokolo mengine, nikauziwa kwa tsh 35k
Kmamamake 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Mnataka graduates majobless tule wapi ninyi watu ?
Kutuajiri hamtaki , tukiwa mawinga na madalali mnatuita vibaka na matapeli , tukiwa marioo kwa mishangazi yenu mnatuwinda kitaa , tukiwa panya road na kupiga roba na nondo mitaani mnaita wasiojulikana squad kuja kutupeleka mkuranga kutumaliza , tukiamua kukaa majumbani mnatuita wazembe na hatutaki kazi ,tukiamua kutembeza bahasha kusaka kazi mnatuambia hatuna experience na tujiajiiri tu na hapo mitaji hatuna mitaji .

Hebu mtuache bana
 
Wasiojulikana mnaanza kujitokeza.
Erick Kabendera alielekezwa - Kibo complex ilitajwa.
Ally Kibao Kibo, complex ilitajwa

Wewe pia unawaelekeza members wa JF waende Kibo complex. Hamuwapati watu kizembe humu.
🤔😳
 
Mawinga na madalali wapo hadi huko kwenye dini na imani zenu aisee , wachungaji , mashehe na waganga wa kienyeji wanawakamua sadaka na kafara ili msamehewe dhambi ,mwende mbinguni na kupata mafanikio .
Sembuse mitaani humu na kwenye masoko ?
 
Hao wateja wa nje mtawakimbiza kwa bei kubwa za mawinga.
Wataenda nchi jirani au maeneo mengine Kama huko Mbagala, Tandika na Mikoani.
Dunia utandawazi watapata taarifa za masoko ya bei nafuu. Msije kuwalilia serikali wameharibu soko lenu kumbe tatizo wenyewe.
Bro kila mtu ana namna yake ya kutoka so mi binafs ctegemei kuitwa muuza duka milele. Na hata huko madukan huwez kunikuta. Ila nachojaribu kukuambia hicho kitu kipo popote, mi nimekikuta kkoo miaka 25 nyuma na mi kwasasa cfanyi biashara mteja wa mwisho niko kwenye uzalishaji na agent's. Kikubwa life kila mtu ana mkondo wake
 
Back
Top Bottom