Kariakoo inakuwaje duka Moja la simu Kuna wauzaji zaidi ya 20

Hao masalange wamejaa kila kona. Uhaba wa kazi umesababisha yote haya.

Kuna wale wanaokaa vituo vya mabasi. Yani abiria unaamka asubuhi una ratiba ya kwenda sehem flani na ofisi za kukatia ticket unafaham zilipo lakini ghafla ukifika stand unakutana na jopo la vijana wa hovyo wanakuvuta vuta na kukuuliza maswala wakitaka kujua unapoenda ili wajifanye wamekupeleka wao ofisi za basi husika wapate ganji. Miyeyusho kinoma.
 
Wale dawa yao nikuwaambia ushakata ticket.
 
Kata ticket online kupunguza usumbufu.
 
wewe utakuwa wa kanda ya ziwa kama sijakosea... Neno salange wanalitumia sana hasa maeneo ya stend ya mabas
 
Na unakuta kuna mafundi simu dukani humohumo.mi kabla sijaenda kununua kitu chochote kkoo naangalia bei yake mtandaoni kwanza.ukiingia kichwa kichwa kkoo lazima ulizwe.
 
Hiyo ni Kwa sababu Kodi ya pango kariakoo ni kubwa sana.kumudu peke Yako Kwa wanaoanza biashara ni ngumu ndiyo maana umeona duka Moja watu watano au zaidi ili kuchangia kulipa Kodi ya nyumba.siyo kama ngara ambako Kodi ni laki Moja Tena palipo na mzunguko mkubwa wa pesa.
 
Mjini akili nguvu kijijini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…