Kariakoo inakuwaje duka Moja la simu Kuna wauzaji zaidi ya 20

Kariakoo inakuwaje duka Moja la simu Kuna wauzaji zaidi ya 20

Hiyo ni Kwa sababu Kodi ya pango kariakoo ni kubwa sana.kumudu peke Yako Kwa wanaoanza biashara ni ngumu ndiyo maana umeona duka Moja watu watano au zaidi ili kuchangia kulipa Kodi ya nyumba.siyo kama ngara ambako Kodi ni laki Moja Tena palipo na mzunguko mkubwa wa pesa.
Nyumba NHC fremu sio bei Kali ila shida ndio Kwa hao watu wa kati yeye amechukua fremu analipia NHC Kodi laki Moja alafu ana ipangasha Kwa laki 6

Watanzania Wana roho mbaya sana
 
Dar inashangaza
Tunatoka mbali kuchukua mizigo kariakoo ambapo tunaamini ndo kitovu cha biashara na bei zitakuwa nafuu
Ukifika inatakiwa bei kubwa sawa na hapa Ngara
Kumbe wenye maduka wameruhusu udalali wa kijinga hadi Kwa mteja aliyejileta dukani unamwekea watu wa kumpandilia bei, sio fair kabisa
Kariakoo acheni uhuni
Ka frem kadogo wamejaa madalali zaidi ya 20 wanazidi hadi wateja
BIASHARA NI KUUZA NA KUNUNUA,BIASHARA NI KUJUA WASICHOJUA WENZIO,MAANA NYINGINE NI SIRI,WEWE KUJA DAR LAZIMA MWANZO UPIGWE,KKO KUNA MADUKA YA JUMLA NA REJAREJA SASA WEWE KAMA ULIINGIA DUKA LA REJAREJA UKATAKA BEI RAHISI HAIWEZEKANI,
 
Ahaa! Kumbe ipo hivyo. Nilishangaa bei ya electronics Kariakoo inataka kufanana na ya mikoani. Labda Kariakoo brands ni nyingi kuliko maduka ya mikoani. Pia, nilienda Karume kutafuta kiatu cha mpira cha mtumba almaarufu Six, bei ya chini walikomaa elfu 90. Nikaja mkoani nikapata kwa elfu 45 tena kikali kuliko vya Karume
😁😁😁😁 Dahh
 
Back
Top Bottom