Kariakoo: Moto Mkubwa unawaka Msimbazi

Kariakoo: Moto Mkubwa unawaka Msimbazi

Naona BOA Bank hapo chini...Hv huu sio mpango kweli wajanja wamesha piga mpunga BOA Bank then wanalipua moto waje kusema pesa ziliungua ama watu wapemepita nazo ktk harakati za kuuzima moto?...ama walishapiga kitamboooo

Sijui nawaza Nini Mimi...kichwa maji mimi
Hivi kuna bank inayolaza pesa mingi weekend?
 
Acha uwake tu tena uwake uunguze vitu. Yaani kariakoo ni eneo la kijinga sana hakuna mpangilio wa kitu chochote, siyo maduka makubwa wala machinga, yaani siku ikitokea fujo watu watakufa sana. Nashauri serikali iwafukuze chinga wote wanaopanga barabarani waondoke kariakoo iwe safi
Wape kazi hao machinga wataondoka hapo Kariakoo.
Inaonekana umeshiba Kande za shemeji yako.
Unadharau kazi za wanaume wenzio wanahangaika kulea familia zao.
Jiheshimu aisee))
 
Kwakifupi hilo eneo ni mbele ya soko kuu la kkoo ambalo liko kwenye maboresho na matengenezo, inawezekana wameona walichome na hilo ili kusafisha mandhari ya mbele ya soko lao.Wamelichoma hili bila shaka yoyote wenye mamlaka zao
Hilo eneo la mnadani kuna umbali na soko la Kariakoo. Rusijazane ujinga, wengine tumekulia mitaa hiyo, tunaifahamu toka haijaanza kujengwa Maghorofa.
 
Mimi huwa najiuliza! Ni matukio machache ambayo jeshi la Zima moto huwa linafakiwa kuzima moto.Na changamoto ninayoiona ni kutegemea magari ya Maji ambayo kama moto umetokea katika maeneo ambayo hayawezi kupita huwa hayana msaada wo wote!
Hivi Serikali haiwezi kununua ndege za Helkopita za Kuzima moto kama wenzetu huko duniani ambazo zinaweza kufika kwenye tukio haraka kuliko kutegemea haya magari ya Maji ambayo pengine yakikutana na foleni yanaweza kushindwa kufikia kwenye tukio kwa wakati?
Kama twiga anagairisha safari Kila siku. Tunaondoka baada ya masaa mawili. Samahani kwa usumbufu. Hiyo fire [emoji602] twiga c itakuja baadaye sana
 
Back
Top Bottom