Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,835
- 23,776
Mwaka 2011 nikiwa diwani wa kawaida tu, tulipokea ugeni kutoka nchini Kenya, madiwani na watumishi wa jiji la NairobiWalikuja kujifunza kuhusu huduma za kukabiliana na majanga Dar es Salaam, tukiwatembeza katika vituo vyetu vya zimamoto na mabomba ya maji ya dharuraWalitusifia sana wakasema Dar es Salaam ipo vizuri kuliko Nairobi.Habari za awali: Moto mkubwa ambao bado chanzo chake hakijajulikana, unaunguza maduka ya wafanyabiashara Kariakoo karibu na kituo cha mafuta cha Bigbon Msimbazi, jijini Dar es Salaam.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linaendelea jitihada kudhibiti moto huo, huku wafanyabiashara wakiendelea kuokoa baadhi ya bidhaa zao.
View attachment 2768279
View attachment 2768304
View attachment 2768357
Mwaka 2013 Jiji la Nairobi walianza kufanya maboresho na mabadiliko kuhusu muundo, mfumo, huduma na vifaa vya kuzima moto na kukabiliana na majanga.Wenzetu waliweka maslahi yao, tofauti zao za kiitikadi, kikabila na vyama vyao pembeni.
Wakati Tanzania tumeweka msimamo wa kutopokea magari yaliyotumika kutoka Ulaya wao waliyapokea kutoka BELGIUM gari 12, TURKEY 10, na SWEDEN gari 10 Wakajenga chuo cha kufundisha kukabiliana na majanga ya asili na moto Wakachimba visima vya maji na kujenga matanki ya maji ya kuzimia moto .
Wakajenga vituo vya zimamoto kila Jimbo (kwa mfano Dar es Salaam tuna majimbo 10, kila Jimbo liwe na kituo cha zimamoto)Wenzetu leo wamejipanga kuliko sisi, tumekwama wala hatujaliMwaka 2018 serikali ya CCM ikazuia yjenzi wa kituo cha kuzimia moto wilaya ya Ubungo, sehemu ya Kwembe - Luguruni tena kwa pesa za wafadhili kutoka Germany, jiji la Hamburg CCM haijali wala haina muda wa kujali Watanzania wanaopoteza mali na mitaji yao.