Wote wanakaa nyumba za NHC siku wakitimuliwa sijui itakuwajeHili si la Uongo, nimekutana na Kijana Mzaliwa wa kariakoo mwenye Familia yake, hakuna sehemu nyingine anayoijua zaidi ya Kariakoo, Ilala, Magomeni na Posta yenyewe..Kwa sasa ndiyo ameanza angalau kutoka anaeza kwenda Maeneo mengine nje ya Mji...
Wapo wengiKuna dogo mmoja nilikutana nae katika mishe mishe anaishi mtaa wa zanaki hapo posta. Mikocheni hapajui wala ubungo au kawe hata hapo magomeni tu yeye hajawahi kufika.
Ni Posta kasoma shule za mjini, akitaka kusafiri anakula Pipa Airport basi
Kweli kabisa tembea ujioneeYaweza kua nikweli, lakin hamna faida ya kujivuna kwakukaa sehem mmoja. Nashauri tutembee kwan kuna faida sana.
Hao lazima watakua wahamiaji hawana ndg sehemu zingine za Nchi! Wanakua kama ma diplomatic maisha yao yote Masaki tu hata magomeni hawapajui!!Baadhi ya maeneo ya Kariakoo, Upanga na Posta hawa watu ni wana nchi yao ndani ya nchi
Mtu anazaliwa Posta hajawahi kufika hata Magomeni
Hudumza zote wanapata huko huko
Posta mpaka kuna vyuo vikuu vya nje vyenye matawi
Starehe zao ni huko huko
Hosptali zao ni classic zipo
Maduka yao Posta mengi ni OG
Masoko na supermaket
Mtu akitoka sana jua anaenda ofisi za uhamiaji ama airport
na huku mbagala tuna maisha yetu, huduma zote tunazipata huku kuanzia miguu ya kuku, utumbo, sukari ya sh mia n.k