Kariakoo, Upanga na Posta wana nchi yao nyingine kabisa

Kariakoo, Upanga na Posta wana nchi yao nyingine kabisa

Kuna watu wanakaa kibaha, kiluvya hawajawahi fika katikati ya jiji wakija mjini wanaishia mbezi mwisho. Wakijitahidi sana ni kimara na ubungo fullstop. Zaidi ya hapo hata nauli ya kurudi hawana
Kweli kabisa, kuna watu wanaishi huku mpiji magoe, town yao ni mbezi mwisho
 
mi mwenyewe sijui popote zaidi ya hapa tarime, tena tarime vijijini
huduma zote zipo. tupo hapa tu boda na nchi jirani. kwenda nje ya nchi naenda tu kwa mguu, shopping na kurudi
sasa ujue kila mahali ili iweje
 
Kuna mdada anaishi Chanika akaniambia hajawahi kufika mlimani City
Dar es Salaam imetanuka sana sasa. Tofauti na miaka ya 1990s au 2000s. Ni kawaida kukuta mtu anaishi Chanika na hapajui Mlimani City. Sehemu za pembeni ya Dar zimezalisha maeneo mengi ya makazi. Mfano, Chanika imezalisha maeneo mengi kama vile Homboza, Zingiziwa, n.k, Mbezi Kuna msimu, makabe, Mpiji magohe, malamba mawili n.k halikdhalika Mbagala na maeneo yake. Na Maendeleo yapo, huduma nyingi zipo huko. Na zaidi maeneo ya mkoa wa Pwani jirani na Dar yefungua makazi mapya kama vile Kibaha, Kisarawe, Mkuranga (Kisemvule, Vikindu) n.k
 
Kuna dogo mmoja nilikutana nae katika mishe mishe anaishi mtaa wa zanaki hapo posta. Mikocheni hapajui wala ubungo au kawe hata hapo magomeni tu yeye hajawahi kufika.

Ni Posta kasoma shule za mjini, akitaka kusafiri anakula Pipa Airport basi
muulize Engineer Hersy.
 
Back
Top Bottom