Karibu asilimia 70% ya maswali ya baadhi ya waandishi wa habari Bongo ni ya ovyo; nina wasiwasi na ubora wa vyuo vya habari

Karibu asilimia 70% ya maswali ya baadhi ya waandishi wa habari Bongo ni ya ovyo; nina wasiwasi na ubora wa vyuo vya habari

Tatizo ni kuwa fani ya habari bado haijafanywa kuwa profession kama fani nyingine.

Ukiachana na sheria zilizowekwa ambazo zinahusisha elimu ,serikali imeweka wakati, kuwa mpk kufikia mwaka 2022 angalau waandish wawe na diploma ,lkn bado suala la utrkelezaji limekuwa zito.

Tabia ya vyombo binafsi kuajiri watu wasio na elimu ,kwa kuzingatia vipaji mfn , Clouds na wasafi , unaiua fani ya habari na kuifanya kuonekana km ni ya makanjanja, online blogs na you- tube zimekuwa km kapu la taka.

Ni wazi kuwa mtu anayetegeme kipaji tu pasipo elimu ,hata reason capasity yake inakuwa chini.
 
Mkapa aliwahi kuwapa makavu kuwa hawajui kuuliza maswali akiwalinganisha jamaa mmoja wa CNN aliyeitwa Khan
 
Uandishi wa habari ni kama uanasheria, unahitaji MTU Msomi( ambaye sio Mvivu WA kusoma soma na kufuatilia Historia) sasa hawa Ndugu zetu kusoma hawataki, hawajui Kwa kina Historia ya nchi na dunia, sio mahiri kwenye Lugha iwe Kiswahili au kingereza, hapo unategemea nini?
Kwenye wachambuzi wa soka huko ndipo balaaa!! Utakuta mtu MIWANI KUBWA!! Hajui tofauti kati ya defence na defend!!" eti jamaa ameshindwa ku defence kabisa" eti jamaa anataka kuwa top score" na anazungumza kwa madahaa!!
 
Niliwahi kusema waandishi wa habari wa Kenya, Rwanda, Uganda wanauliza maswali yenye mantiki sana kuliko waandishi wetu Tanzania wako level ya waandishi na wana habari wa Burundi, Congo maana kosa waulize vitu vyenye logic wao huuliza umbea umbea tu,
Uwezo mdogo!!!
 
Hivi makanjanja waliishia wapi? Jamaa hao walipenda bahasha sana. Nusura wasababishe itungwe sheria kudhibiti jamaa hao.
 
Nimefuatilia mahojiano (interview) nyingi za waandishi wa habari Tanzania!

Wengi wao wanamaswali ya hovyo na kipuuzi kuliko mahitaji ya jamii inachohitaji kujulishwa!

Maswali yao mengi yapo kwenye mlengo wa taharuki kwamba Flani kasema vile na vile almradi tu jambo lionekane la kuishangaza jamii.

Mfano: Kesi ya Feisali na TFF wanahabari wanaonekana kuuliza upuuzi upuuzi mwingi mara ooh tumesikia mama akilalama kuwa mwanae alilishwa ugali na sukari. Je, Feitoo alipokuwa yanga alikula ugali na sukari ya mtibwa? au alilambishwa mayonaiza?

Hivi kwrli Maswali ya sampuli kama hiyo yanamsaada gani katika jamii kama siyo ubovu wa wanahabari wetu?

Huenda wanaohojiwa wanakerwa lakini wanayavumilia tu! Hayana tija kabisa!

Natamani kuona wanahabari wenye uwezo wa kuhoji kila swali lenye tija angalau 80% ya ujumbe
Waandishi wa maana, wenye weledi hapa Bongo, wako pungufu ya 100.
 
Sio kwamba wanaendana na Mahitaji ya Jamii yetu?
Nafikiri hayo ndio aina ya mambo Watanzania wengi wanapenda kusikia.
Media ndiyo inayojenga jamii, sasa hivi 90% ya vijana wanasema 'hii nyimbo'.. hili lilianza na watangazaji wa VIPINDI vya bongofleva Sasa limeenea, zamani waandishi wa habari walikuwa watu wanaojua mengi na sahihi
 
Elimu ndogo tena ya kuunga unga, utegemee kuwa na maarifa makubwa?!!Kenya tu wanatuzidi mbali sana,ndio maana hata kwenye...
Mkuu Pascal Mayalla nilimuaminia sana alipomuuliza anko magu mashi lile swali,ilikuwa ni ujasiri wa hali ya juu na kipekee sana kwa kipindi kile! Swali lilikuwa gumu na la kimantiki! Kudos kwako mkuu Pascal Mayalla
 
Media ndiyo inayojenga jamii,Sasa hivi 90% ya vijana wanasema 'hii nyimbo'..hili lilianza na watangazaji wa VIPINDI vya bongofleva Sasa limeenea,zamani waandishi wa habari walikuwa watu wanaojua mengi na sahihi
Inakera sana mtangazaji/muandishi kutokujua lugha sahihi, anakuwa anaikanganya hadhira yake sana!
 
Mimi nilidhani ni mwenyewe naliona Hilo!!
 
Kuna kitu inaitwa upeo,
Ukishakuwa na upeo mdogo Kwa kweli inasikitisha Sana.
Wenzako hapo wanaona wameuliza maswali ya Maana.

Kibongobongo ni ngumu kutofautisha Uandishi na Umbea
Anzisha chuo bora au uliza mwenyewe
 
Nimefuatilia mahojiano (interview) nyingi za waandishi wa habari Tanzania!

Wengi wao wanamaswali ya hovyo na kipuuzi kuliko mahitaji ya jamii inachohitaji kujulishwa!

Maswali yao mengi yapo kwenye mlengo wa taharuki kwamba Flani kasema vile na vile almradi tu jambo lionekane la kuishangaza jamii.

Mfano: Kesi ya Feisali na TFF wanahabari wanaonekana kuuliza upuuzi upuuzi mwingi mara ooh tumesikia mama akilalama kuwa mwanae alilishwa ugali na sukari. Je, Feitoo alipokuwa yanga alikula ugali na sukari ya mtibwa? au alilambishwa mayonaiza?

Hivi kwrli Maswali ya sampuli kama hiyo yanamsaada gani katika jamii kama siyo ubovu wa wanahabari wetu?

Huenda wanaohojiwa wanakerwa lakini wanayavumilia tu! Hayana tija kabisa!

Natamani kuona wanahabari wenye uwezo wa kuhoji kila swali lenye tija angalau 80% ya ujumbe

What counts ni qualifications zao kuingia chuoni na qualifications za Walimu wanaowafundisha, kama division 4 na 3 za mwisho, you dont look gold out of grass.
 
What counts ni qualifications zao kuingia chuoni na qualifications za Walimu wanaowafundisha, kama division 4 na 3 za mwisho, you dont look gold out of grass.
Siyo kwamba vyuo haviwaandai vyema
 
Media ndiyo inayojenga jamii, sasa hivi 90% ya vijana wanasema 'hii nyimbo'.. hili lilianza na watangazaji wa VIPINDI vya bongofleva Sasa limeenea, zamani waandishi wa habari walikuwa watu wanaojua mengi na sahihi
Kabisa kabisa lakini sahivi ni kama vijiwe vya redio kina babalevo, mpoki, mwajaku utawasikia ....wowowo,zigo , zagamua , ...nk
 
Hakuna namna ndio upande tuliochagua ndio maana hata ukiangalia kwenye Baraza unakuta watu wa hivyo hivyo, maendeleo ni process ndefu yenye hatua nyingi ngumu..
 
Back
Top Bottom