Karibu tushauriane juu ya nini cha kufanya na matokeo yako ya Kidato cha Sita 2020

Karibu tushauriane juu ya nini cha kufanya na matokeo yako ya Kidato cha Sita 2020

Sasa unasoma ili uende wapi wakati kila kitu kimo Youtube
 
Wakuu ushauri naombeni,mbali na bachelor ya education course gani anaweza kusoma, kidogo inayoeleweka soko.? Dogo kasoma art hkl
 
Wakuu naombeni kujua machache kuhusu hii course ya Chemical and process engineering kwa wenye utaalamu nayo mfano urahisi wake wa ajira na mengneyo na inahusika wapi zaidi
 
Nimemaliza form 6 comb PCM na matokeo yang ni div 2 point 10.

Physics. (D).

Chemistry. (D).

Adv.maths. (B).

kwa wazoefu mlioko chuoni, kwenye ajira na mliojiajili naombeni mnishauli faculty nzuri ya kusomea yenye uafadhali wa maslahi, urahisi wa kuajiliwa au kujiajili kama nikifanikiwa kumaliza chuo.

N.B mliosoma PCM na mko chuo au mmemaliza nahitaji zaidi mchango wenu

Hongera kwa ufaulu. Jambo la kwanza ni kutafakari je ungependa kuwa nani baada ya masomo? Mwalimu? Engineer? Etc kisha panga hayo machaguo yako kwa ukizingatia kipaumbele mfano
1.Mwalimu
2. Accountant
3. Engineer
Etc
Kisha kwa msaada wa Undergraduate Admission Guidebook ya 2020/21 iliyopo kwenye www.tcu.go.tz tafuta vyuo vinavyotoa programme uzipendazo na sifa za kujiunga baada ya hapo unaenda kufanya maombi..
 
Kwa matokeo haya course gani anaweza pata huyu dogo pale SUA CHEM-E BIO -D GEO-D

Ndugu kwa matokeo yako hayo unaweza kuchaguliwa kwenye programme zinazohitaji ufaulu kwenye masomo ya Bio na Geo nakushauri upate Admission Guidebook ya 2020/21 hapa www.tcu.go.tz itakuongoza vizuri ni programme gani na zipo vyuo gani kwa kuanzia angalia Ardhi University na SUA.
 
Jamani msaada

Chemistry-E
Biology -C
Geography-D

Akasome nini huyu jamani?

Je? Biotechnology anaweza soma? Nursing je?

Au ipi kozi ya mifugo.
Mawazo

Nursing hawezi kwa sababu ya E ya chemistry. Kuna programme nyingi anaweza kusoma pitia www.tcu.go.tz download 2020/21 Undergraduate Admission Guidebook kwa miongozo wa programmes na sifa za kujiunga.atweza kujiunga na kazi zinazohitaji Chem na Biology au Biology na Geo.
 
Husika na kichwa cha habari hapo juu mimi nimehitimu combination ya HGE

HISTORY -D
GEOGRAPHY -E
ECONOMIC-D

O level nilipata

Mathematics-C
BIOLOGY-C
GEOGRAPHY-C
PHYSICS-D
CHEMISTRY-D

Nimeambatanisha matokeo ya O level kwasababu kuna KOZI wanazingatia hayo
Binafsi napenda kusoma COMPUTER SCIENCE , IT & ICT AU KOZI ZINAZOENDA NA HIZO
BUT KUTOKANA NA UFAULU HUO VYUO VICHACHE NAKIZI VIGEZO

Mfano SUZA, MZUMBE, NIT ila kutokana na hofu ya competition nimekuja HUMU WAKUU kuomba ushauri WA KOZI nyengine nzuri ili nikikosa hizi nisiyumbe lakini KOZI zinazotoa ujuzi na sio certificate tupu

KAMA YUPO MUHITIMU MWENGINE UZI WETU NDIO HUU TUOMBE USHAURI

Napenda kutanguliza shukrani kwa niaba ya wanafunzi wote

AHSANTENI

Ndugu Hongera kwa ufaulu wako unaonyesha una sifa za kujiunga na programme zinahitaji ufaulu kwenye masomo ya Econ na Hist. Tafadhali tembelea tovuti hii www.tcu.go.tz kupata copy ya 2020/21 Undergraduate Admission Guidebook ambao ni mwongozo na sifa za kujiunga na programme za vyuo Vikuu vyote vinavyodahili mwaka 2020/21
 
Nina dogo langu kamaliza form six na alisoma CBG je ni course gani ya sayansi ambayo anaweza kusoma ili akimaliza atoke na ujuzi kichwani mbali na uhakika wa ajira. Ufaulu wake ni div 2 ya 11 yaani D flat.

Naomba kuwasilisha.
Education Science itamsaidia: Atembelee vyuo kama Marian University College. Website: www.maruco.ac.tz

Kwa maelezo zaidi.

Sent from my SM-J200H using JamiiForums mobile app
 
Hello wakuu
Mm nimehitimu kidato cha sita mwakahuu kwa combination ya PCB
Matokeo yangu yamenikata maini kwakwel
NINA DDE physics ndio imeniungusha kabisa
Sasa kiukweli hapa nilipo nipo njia panda
Napenda kusoma kozi za afya ila kutokana na ufaulu wangu ww kama mzoefu unaweza ukanishauri niwapi nipite ili niweze kufikia mafanikio.
Je naweza nika anza na diploma ya clinical officer au kuna njia mbadala asanteni!! Ambayo ni nuzri zaidi sitaki kurudia mtihani!!
Tembelea: www.maruco.ac.tz

Sent from my SM-J200H using JamiiForums mobile app
 
Wakuu naomba msaada wenu Mimi nimemaliza kidato Cha sita mwaka 2020 na mimebahatika kupata division 3 ya 14 kwa mchepuo wa CBG na kupata CHEMISTRY E,BIOLOGY E, GEOGRAPHY D kwa alama hizo naweza kuchaguliwa kujiunga na University

Ndugu ili uwezo kuchaguliw kujiunga na elimu ya juu kwa ngazi degree inahitajika kuwa na ufaulu utakao fikia at least point 4 kwenye masomo mawili. Kwa ufaulu wako hujafikia unashauriwa kufanya Diploma au kurudia hayo masomo uliopata chini ya D.
 
Hello wakuu
Mm nimehitimu kidato cha sita mwakahuu kwa combination ya PCB
Matokeo yangu yamenikata maini kwakwel
NINA DDE physics ndio imeniungusha kabisa
Sasa kiukweli hapa nilipo nipo njia panda
Napenda kusoma kozi za afya ila kutokana na ufaulu wangu ww kama mzoefu unaweza ukanishauri niwapi nipite ili niweze kufikia mafanikio.
Je naweza nika anza na diploma ya clinical officer au kuna njia mbadala asanteni!! Ambayo ni nuzri zaidi sitaki kurudia mtihani!!

Pole Sana kijana, lakini pia kwa ufaulu wako huo unafit baadh ya fuculty za afya Kama bacherol degree in biotechnology and labaratory science pale SUA.
 
Ndugu ili uwezo kuchaguliw kujiunga na elimu ya juu kwa ngazi degree inahitajika kuwa na ufaulu utakao fikia at least point 4 kwenye masomo mawili. Kwa ufaulu wako hujafikia unashauriwa kufanya Diploma au kurudia hayo masomo uliopata chini ya D.
Na nikiomba diploma chuo kikuu naweza kupata mkopo
 
Back
Top Bottom