Karibu tushauriane juu ya nini cha kufanya na matokeo yako ya Kidato cha Sita 2020

Karibu tushauriane juu ya nini cha kufanya na matokeo yako ya Kidato cha Sita 2020

Hvi siku hzi utaratibu ukoje!??
Hiyo si div 3 ya 14!??
Mbona miaka ya nyuma walipata nafasi vyuoni

Ndugu ili kujiunga na elimu ya juu kwa ngazi ya degree mwanafunzi anahitaji kuwa na at least na point 4 ktk masomo mawili yani
A=Point 5
B=point 4
C= Point 3
D= point 2
E= 1
S=0.5
F=0
A,B na C zikiunganishwa na E zinakupa jumla ya point 4 na zaidi. Kwa mwanafunzi asiye na A,B na C kwenye matokeo yake ya kidato cha sita anahitaji kuwa na atleast D mbili ambazo zina jumla ya point 4 ndo atakuwa na sifa za kujiunga na elimu ya juu kwa ngazi ya degree.
 
Tushauriane hapa dogo advance ana....
Physics D
Chemistry C
Biology C
Haende chuo gani?
 
Nina dogo langu kamaliza form six na alisoma CBG je ni course gani ya sayansi ambayo anaweza kusoma ili akimaliza atoke na ujuzi kichwani mbali na uhakika wa ajira. Ufaulu wake ni div 2 ya 11 yaani D flat.

Naomba kuwasilisha.

Hongera kwa ufaulu. Tafadhali tembelea tovuti www.tcu.go.tz pata copy ya 2020/21 Undergraduate Admission Guidebook itakuongoza vizuri ni programme zipi ambazo unaweza kujiunga na sifa hitajika.
 
Hello wakuu
Mm nimehitimu kidato cha sita mwakahuu kwa combination ya PCB
Matokeo yangu yamenikata maini kwakwel
NINA DDE physics ndio imeniungusha kabisa
Sasa kiukweli hapa nilipo nipo njia panda
Napenda kusoma kozi za afya ila kutokana na ufaulu wangu ww kama mzoefu unaweza ukanishauri niwapi nipite ili niweze kufikia mafanikio.
Je naweza nika anza na diploma ya clinical officer au kuna njia mbadala asanteni!! Ambayo ni nuzri zaidi sitaki kurudia mtihani!!

Kama ni lazima sana usome afya anza na Diploma ya afya then utafanya degree baadae lkn kwa ushauri mwingine pata copy ya Undergraduate Admission Guide Book 2020/21 hapa www.tcu.go.tz angalia programme zinazodahili wanafunzi wenye ufaulu kwenye hayo masomo uliyopata D mfano Education, BBA etc
 
Wakuu naombeni kujua machache kuhusu hii course ya Chemical and process engineering kwa wenye utaalamu nayo mfano urahisi wake wa ajira na mengneyo na inahusika wapi zaidi

Hawa ni engineers wa viwanja vya kemikali je tunavyo?
 
Nimemaliza form 6 comb PCM na matokeo yang ni div 2 point 10.

Physics. (D).

Chemistry. (D).

Adv.maths. (B).

kwa wazoefu mlioko chuoni, kwenye ajira na mliojiajili naombeni mnishauli faculty nzuri ya kusomea yenye uafadhali wa maslahi, urahisi wa kuajiliwa au kujiajili kama nikifanikiwa kumaliza chuo.

N.B mliosoma PCM na mko chuo au mmemaliza nahitaji zaidi mchango wenu
Biomedical engineering
 
Olevel umesoma sayansi,A level umesoma madudu mengine,history,!!!HV huwa mmelogwa au?unapokuwa kidato cha pili,unatakiwa uwe unajua,utasoma masomo gani,kidato cha tatu,na unataka uwe nani huku duniani, dakitari, Muhandisi, Mtaalamu wa kilimo, ICT, Mwanasiasa, Mwalimu, Mwanasheria, nk, sasa ukipelekwa na upepo wa matokeo,inakuwa umepoteza muda,sasa wewe unataka kusoma IT,wakati kidato cha sita hukusoma sayansi!kwahiyo inabidi ukatumie cheti cha form four,sasa miaka miwili ya A level,siimepotea bure,,baada ya kumaliza form four, ungeenda DIT, ungepiga, diploma, miaka miwili, then unaunganisha mitatu tena sasa HV, ama ungekuwa unasoma bachelor In Engineering,au ungekuwa kazini,unalipwa mshahara.

Sie Anko zenu,tumemaliza form four 99,kulikuwa hakuna mitandao ya kijamii,no mobile phones,no smart phones,lakini tulijitaidi kupata taarifa,za kutosha ni nini tunataka maishani na nini tusome,sasa Leo kila kitu kipo,information on ur fingertips,!!!mnafeli wapi?!!!inakuwa kama mnasoma kama vipofu,mkigonga ukuta ndio mnajua mmefika,
Mimi niliamua kuwa nataka kuwa engineer nikiwa kidato cha pili.

Na niliihapa lazima nisome UD nikiwa darasa la saba,nilivutiwa na matamasha,ya siku ya mtoto was afrika yaliyokuwa yakifanyika UD ukumbi wa nkuruma.
Siku hz watu wanaangialia wap kuna lipa co unataka kuwa nan
 
Kwa matokeo haya huyu mtu anaweza soma microbiology au bachelor of science in molecular biology and biotechnology pale udsm
Chem D
Bio D
Geo C
Bam S
Gs D
kuna jamaa frani alikua nasoma faculty ya microbiology hapo UD.😂😂😂
Alikua anaona wengine wote wamebugi ila yeye tu ndo yupoo on right track
 
Mdogo wangu kapata 2 ya 11 (DDC) anataka kusoma medical,is it possible?

=====

Habari wanaJF,

Leo Baraza la mitihani la Tanzania NECTA limeyatoa matokeo ya kidato cha sita, kwa uzoefu wangu nimeona ni vyema tuanzishe uzi huu maalumu ili tushauriane, tueleweshane, tuambiane nini cha kufanya na namna ya kuchagua vyuo.

Ikumbukwe TCU wana vigezo kwa ajili ya kujiunga na elimu ya juu.

Karibuni.
Kama anataka kusoma Md CUHAS Mwanza nicheki Pm
 
Back
Top Bottom