Karibu tushauriane na kupeana uzoefu wa manunuzi ya chakula kwa ajili ya mwezi mzima

Karibu tushauriane na kupeana uzoefu wa manunuzi ya chakula kwa ajili ya mwezi mzima

Habari za jioni wakuu,

Binafsi nimekuwa nikipitia changamoto sana nifanyaje au ninunue vyakula gani ambayo vitaweza kunifikisha mwezi mzima.

Naombeni uzoefu wenu katika hili, ni nini unazingatia, utaratibu upi unautumia kwenye kufanya manunuzi ya chakula.

Ukiweza kusema ni vyakula gani huwa unapendelea kununua na kuweka ndani itakuwa vyema zaidi. Asanteni, Uzi tayari.
Kwa upande wangu na familia yangu, Maharage kilo 10,Unga kilo 20, mchele kilo 40, mafuta ya kula Lita 10 hapo naua mwezi vizuri, na ubaoni inaachwa kumi na Tano matumizi mboga na mengineyo. Japo weekend Hali huwa tofauti.
 
Hali ikiwa nzuri
Mchele 15kgs
Unga kg 15
Maharagwe sado 1
Sukari kg 3
Chumvi 1kg
Ngano 5kg
Mafuta kula 5litres
Gas tank ndogo
Mkaa kiroba kidogo
Maziwa fresh ¾ litre daily

Mboga mboga
nyama
Ndizi/viazi
manunuzi mara 2 kwa wiki, familia ndogo hiyo lakini baba, mama na mtoto
 
Unaweza kuelezea, let say nyanya, hoho,vitunguu unanunua za shilingi ngapi? Na huwa unaizitunza vipi?

Nyanya nanunua sado moja naweka kwenye friji

Carrot nanunua 2kg naweka kwenye mfuko natia kijiko naweka hata chini

Vitunguu 2kg naweka kwenye kitenga

Hoho mixer 3kg

Brocoli 2kg

Fresh beans 1kg

Zucchin 2kg nafunga kwenye mfuko kisha frijini

Tangawizi 1/2 nasaga naweka kwenye kopo natia kwenye friji

Viazi debe moja naweka sakafuni
 
Kwa upande wangu na familia yangu, Maharage kilo 10,Unga kilo 20, mchele kilo 40, mafuta ya kula Lita 10 hapo naua mwezi vizuri, na ubaoni inaachwa kumi na Tano matumizi mboga na mengineyo. Japo weekend Hali huwa tofauti.
Asante Mkuu, familia inawatu wangapi?
 
Nyanya nanunua sado moja naweka kwenye friji

Carrot nanunua 2kg naweka kwenye mfuko natia kijiko naweka hata chini

Vitunguu 2kg naweka kwenye kitenga

Hoho mixer 3kg

Brocoli 2kg

Fresh beans 1kg

Zucchin 2kg nafunga kwenye mfuko kisha frijini

Tangawizi 1/2 nasaga naweka kwenye kopo natia kwenye friji

Viazi debe moja naweka sakafuni
Ukiweka kijiko kwenye Carrot inasaidia nini ?
 
Mahitaji ya mwezi kwa familia ya watu wa 4.
Nyama kilo 7.5
Samaki kilo 7.5
Nyanya kilo 10 hizi natengeza paste
Haharibiki kata miezi 6
Vitungu kilo 2 natengeza paste ya miezi 2
Maharage kilo 2
Mchele kilo 5
Unga kilo 10
Mboga za majani ninazo Kama maua
Unga wa Uji kilo 5
Tangawizi giligilani kitunguu swaumu kilo moja moja navyo vinatengezwa paste miezi 2
 
Mchele,unga wa ugali ,ngano ,mafuta ,sukari ,maharagwe ,samaki ,dagaa ,njegele,karoti ,hoho,nyanya maji,vitunguu saumu,vitunguu maji,matunda,viazi mviringo,tambi,mayai,viungo vya mboga,pilau na chai e.t.c
Nyama na maini huwa nanunua fresh
 
Mahitaji ya mwezi kwa familia ya watu wa 4.
Nyama kilo 7.5
Samaki kilo 7.5
Nyanya kilo 10 hizi natengeza paste
Haharibiki kata miezi 6
Vitungu kilo 2 natengeza paste ya miezi 2
Maharage kilo 2
Mchele kilo 5
Unga kilo 10
Mboga za majani ninazo Kama maua
Unga wa Uji kilo 5
Mbona kama Unga na mchele ni kidogo sana kwa familia ya watu 4. Unaweza kuelezea unavyoitengeneza tomato paste, kama hutojali?
 
Mahitaji ya mwezi kwa familia ya watu wa 4.
Nyama kilo 7.5
Samaki kilo 7.5
Nyanya kilo 10 hizi natengeza paste
Haharibiki kata miezi 6
Vitungu kilo 2 natengeza paste ya miezi 2
Maharage kilo 2
Mchele kilo 5
Unga kilo 10
Mboga za majani ninazo Kama maua
Unga wa Uji kilo 5
Unatengenezaje hizo paste

#MaendeleoHayanaChama
 
Unga kg 25, Mchele 10 kg, Dagaa Kg kadhaa( huwa naongeza baada ya muda), vitunguu kg 2, Mafuta lt 5, Sukari Kg 5, Gesi full, Luku 10k, maharage kg 5, Siagi nusu Kg, maziwa. ya unga kg 2. vitu kama nyanya na mboga huwa nabadili mara njegere mara dagaa mchele na mambo yanakuwa fresh

hapo mwezi natoboa japo ni jeshi la mtu mmoja ila wanangu huwa wananiibukia weekend so tunatoa kitu kama kawa.
 
Back
Top Bottom