Karibu uraiani Tundu Antiphas Mughwai Lissu, heshima iliyoje kwako DPP Mwakitalu

Karibu uraiani Tundu Antiphas Mughwai Lissu, heshima iliyoje kwako DPP Mwakitalu

Kwanza nianze na salamu ya Kwetu Kwa DPP ( mkurugenzi wa mashitaka) na kaka yangu Sylvester Mwakitalu. UGHONILE KIKOLO NDAGA UTUKUNYIKE. KYALA AKUSAJE NU KUKULINDILILA PAMUSI NA PAKILO.

Pili nimpongeze Mtanganyika mwenzangu na rais wa tatu ajaye ( Baada ya huyu kudumu Kwa muda mfupi atafata mwingine kisha utakuwa wewe) Ndugu Tundu A. Lissu kwa ustahimilivu (resilience) ulioonyesha akiwa ndani ya kuta za magereza Kwa siku zaidi ya 83 Mpaka atakapoachiwa. You are a true and tested candidate bro! Hata kitengo kina Imani nawe isiyo mithirika ( Unwavering faith). Sasa Tanzania imepata upinzani wa kweli baada ya danadana nyingi za kutimiza matakwa ya SAP na world bank huku vyama vingi Tanzania vikiwa ni vyama pandikizi vya chama tawala.

Tatu nikipongeze Chama Chángu pendwa CCM Kwa kutuletea upinzani haswa ambao utaenda kuleta mabadiliko ya kimfumo na kiutendaji na hapa niwe muwazi ( wanachopigania CHADEMA) sio Kwajili ya maslahi yao binafsi Bali ni kwajili ya kila mtanzania. Tunaenda kuwa na nchi Ambayo CHADEMA ikizingua tunaitoa inaingia CCM. CCM ikizingua tunaitoa tunaenda na ACT WAZALENDO au CHAUMMA. Mapito ya LISSU ni yale waingereza wanaita BLESSING IN DISGUISE ilibidi apitie anayopitia Ili atumike kama lango la mabadiliko Tanzania.

Mwisho tujiandae Kwa mtifuano na Siasa Kali sana kuliko wakati wowote Ule. Sema alaumiwe sana aliyeshauri TUNDU LISSU akamatwe na kuwekwa ndani. Kaihujumu nchi toka Kwa wadau wa maendeleo (Donors) na kamuongezea umaarufu LISSU.
Haya tumekusikia
 
Kwenye mabano hapo!

"Mtanganyika baada ya huyu kudumu kwa muda mfupi,halafu utakuja wewe (Lisu)!!

Elezea vizuri mkuu!!
Bado hujasoma vizuri rudi tena ule mstari hakuna aliposema baada huyu utakuja wewe Lisu
Kasema Baada ya huyu atakuja mwingine kisha Lisu
Usimulishe maneno mtoa mada😁😁
 
Kwa mtanzania halisi kabisa bila kujali itikadi ya chama chake na kama unaipinga kauli mbiu ya NO REFORM NO ELECTION basi umelaanika - ndiyo wewe unayepinga una laana.
Kauki mbiu hii haina ubaya wowote baki ni mwacho wa kuoata biongozi bora wanaotokana na wananchi wenyewe basi, sasa ubaya upo wapi?

Kaukl mbiu hii inakwenda kubalisha nchi - inakwenda kurudisha mamlaka ya utawala kwa wananchi sababu wanayemtaka tu ndiye wagamchagua na akiwazungua watakuwa na hatua za kumshughulikia kupitia sanduku la kura.
 
Kwanza nianze na salamu ya Kwetu Kwa DPP ( mkurugenzi wa mashitaka) na kaka yangu Sylvester Mwakitalu. UGHONILE KIKOLO NDAGA UTUKUNYIKE. KYALA AKUSAJE NU KUKULINDILILA PAMUSI NA PAKILO.

Pili nimpongeze Mtanganyika mwenzangu na rais wa tatu ajaye ( Baada ya huyu kudumu Kwa muda mfupi atafata mwingine kisha utakuwa wewe) Ndugu Tundu A. Lissu kwa ustahimilivu (resilience) ulioonyesha akiwa ndani ya kuta za magereza Kwa siku zaidi ya 83 Mpaka atakapoachiwa. You are a true and tested candidate bro! Hata kitengo kina Imani nawe isiyo mithirika ( Unwavering faith). Sasa Tanzania imepata upinzani wa kweli baada ya danadana nyingi za kutimiza matakwa ya SAP na world bank huku vyama vingi Tanzania vikiwa ni vyama pandikizi vya chama tawala.

Tatu nikipongeze Chama Chángu pendwa CCM Kwa kutuletea upinzani haswa ambao utaenda kuleta mabadiliko ya kimfumo na kiutendaji na hapa niwe muwazi ( wanachopigania CHADEMA) sio Kwajili ya maslahi yao binafsi Bali ni kwajili ya kila mtanzania. Tunaenda kuwa na nchi Ambayo CHADEMA ikizingua tunaitoa inaingia CCM. CCM ikizingua tunaitoa tunaenda na ACT WAZALENDO au CHAUMMA. Mapito ya LISSU ni yale waingereza wanaita BLESSING IN DISGUISE ilibidi apitie anayopitia Ili atumike kama lango la mabadiliko Tanzania.

Mwisho tujiandae Kwa mtifuano na Siasa Kali sana kuliko wakati wowote Ule. Sema alaumiwe sana aliyeshauri TUNDU LISSU akamatwe na kuwekwa ndani. Kaihujumu nchi toka Kwa wadau wa maendeleo (Donors) na kamuongezea umaarufu LISSU.
We jamaa kama kweli unatupa matumaini Hewa tu basi utalaaniwa milele na milele utakuwa umeumiza nafsi zetu.

Lakini kama usemacho ni haki na kweli basi Limebarikiwa Tumbo lililokuzaa.
 
Kuhusu Tundu Lissu, there are undisputed dialogue about him.

He is Tested, Varified and Trusted
Jana nilifanikiwa kupata muda fulani wa kusoma comments za FB, twita, na Youtube kuhusu ule uwasilishaji wa TAL mahakamani.

Aiseee! Itoshe tu kusema watu wametoa yote ya moyoni. Unaweza kutoa chozi zito!

Comment nne hizi hapa:
1. ^Watu kama hawa, nchi zingine zinawalinda kwa wivu mkubwa, lakini sisi hapa tuko mstari wa mbele kujaribu kuwafuta.^

2. ^TAL siyo mbinafsi. Amewatetea hadi wafungwa wengine gerezani. Hajizungumzii yeye peke yake - japo yeye si mfungwa! Yule afisa wa Farao alimsahau Yusufu aliyekuwa naye gerezani pamoja na kwamba ndoto yake ilipotiki alimsisitiza akamtetee kwa Farao. Lakini TAL hakurudia kosa la huyo afisa wa Farao.^

3. ^Tulioko nje, kila mmoja kwa nafasi yake, tuna wajibu wa kuhakikisha kwamba haki inapatikana haraka kwa TAL. Tuache ubinafsi. Tuache kujisahau. Kila mmoja afanye kitu, hata kwa kusali au kuandika tu, sauti zetu zisikike. Tuna mengi sana ya kumfanyia, na dunia inatutazama!^

4. ^We're so blessed with renown, coveted individuals, but for some sad, selfish reasons we have chosen not to see. LORD have mercy!^

5. Funga mwaka ni hii comment: ^Tukizungumzia rasilimali za taifa, TAL naye ni tunu mojawapo!^

Nilifikia hitimisho langu mwenyewe kwamba sisi Watanzania ni wabinafsi wakubwa sana, na ubinafsi huo tumeuficha kwenye hoja na dhana fulani fulani ambazo kwa nje ni nzuri tena sana tu.
 
Back
Top Bottom