Karibuni kwenye Kazi ya ualimu, lakini usiwe na matarajio makubwa

Naongea kutokana na uzoefu kidogo, nineona kwenye interview vijana wakipanga mistari mirefu kupambania ugali wao, wengine wamekaa mtaani zaidi ya miaka 10, na bado wapo wanapambana kwenye usahili,

Utakapo pata nafasi ya kuingia kwenye ajira, Moja Kwa Moja na utakutana na watu uko kazini wakiwa wanawaza kuacha kazi, yaani wewe unapambana uingie utakutana na watu ambao wanataka waondoke, wakiwa na depression na mawazo tele, utakuta watu senior, wenye miaka 10 kazini wakiwa hawana nyumba, stress zikiwa nyingi mnooo, utashangaa kuona watu wakishinda na cadet mpauko, bado utakua uelewi elewi, utakaa miaka mitano bila ya kufanya jambo lolote la maana, hapo ndio utaanza kupata depression.

Nimeona vijana wengi wakisema tukishaingia tutafanya biashara au tutafanya kilimo, niamini Mimi kati ya walimu 10 waliofanya hivyo mmoja tu ndio alifanikiwa, kwasababu biashara au kilimo lazima uwepo wewe utajichanganya ufungue biashara alafu umuache mtu hapo ndio utakua Mwisho wako.

Huwezi Fanya jambo lolote la maendeo bila kukopa, mfano ukiingia na degree utakopesheka million 18, na mshahara utabaki na laki mbili au tatu, sasa inategemea hiyo million 18 umeipeleka wapi, kama umeenda kujenga chumba na sebule basi ndio mwanzo wa kuishi maisha ya kifukara maisha yako yoote. Ukiiweka kwenye biashara na umemuweka mtu basi ndio mwisho wako huo.

Kukosa matumaini ya uliowakuta kazini, na miaka yako mitano uliyofanya kazi bila kumiliki chochote, ndio kitakufanya uanze kuwaza kuacha kazi, kuvumilia mateso tena unajikuta umepangwa vijijini uko, au kigoma, sumbawanga, Rukwa n.k hapo ndio utatamani urudi tu uache kazi urudi mjini.

Ubaya wa hii kazi hakuna marupurupu au pesa za kuiba, alafu unyonge wa walimu wa miaka iliyopita ndio itasababisha Kila mtu akuchukulie poa tu, ukijitambulisha wewe ni mwalimu hakuna heshima Wala recognition ambayo utaipata kwa mtu yoyote yule.

Karibuni kwenye ualimu, lakini kama una ndoto miaka Yako 15 ya ualimu utazidiwa na mtu aliyeko TRA, TPA mwenye miaka miwili kazini.

Believe me, nioneshe mtu mwenye status yoyote Tanzania hii ambaye kasomesha mtoto wake ualimu.

Asante.
Asante sana, Bila kupepesa wewe ni mwalimu pasee.. na unajua maisha halisi ya walimu.

OMBI: Njoo na suluhisho namna ya kukwepa maisha hayo, Njoo na ushauri kwa waliokosea ,Tutakushukuru sana.
 
Sikia hakuna walimu wengi wenye maisha mazuri, ila ni mahangaiko tu, kama kula ni maisha mazuri basi sawa, Nina rafiki yangu ni mwalimu yupo daraja G, ana miaka 47, amekopa weee, salary slip inasoma laki Tano na sabini na nne ndio anapokea kama mshahara, vipi huyo na yeye ana maisha mazuri? Watoto wanne, wote wanasoma shule za kawaida tu, nawaambia vijana waingie bila expectation wataumia inabidi wajifunze, Nina miaka miwili kazini baada ya kuliona ilo mzee sijafurahishwa na maisha ya humu tulipo, sina mawazo kwasababu Nina project ya miaka 4 zaidi ya hekari 27, najua nitateseka kwa miaka hiyo Mungu akinibariki siwezi kubaki humu.
Mwalimu kama hajaachiwa urithi imekula kwake huo mshahara ni wa kula tu.Hauwezi kuutumia kufanya jambo lolote la maana!!!

📌Tatizo hii mitoto ya skuizi mibishi sana.
 
Asante sana, Bila kupepesa wewe ni mwalimu pasee.. na unajua maisha halisi ya walimu.

OMBI: Njoo na suluhisho namna ya kukwepa maisha hayo, Njoo na ushauri kwa waliokosea ,Tutakushukuru sana.
📌Usiingie huko HUO NDO USHAURI WA MWISHO!!!
 
📌muache huyo ni Sr wako kakuzidi kila kitu.

Jinsi alivyodadavua mambo nyie watoto wadongo hamna mahali wala haki ya kuhoji kayatolea wapi hayo.

📌📌Dogo kaa kwa kutulia,pata mwanga njaa isikufanye ubongo wako uwe na UKUNGU ukakosa kufikiri vyema!
Hamna kitu pale kaandika andika tu kisa mke wake kamkera halafu anatafuta faraja kwa wana JF.
 
Walimu wa Tanzania tatizo lenu ni upumbavu ndiyo maana mnaona kazi ya ualimu ni ngumu au mbaya ...mnashindwa kutumia akili zenu vizuri... labda kwa sababu akili zenyewe mlizo nazo ni finyu ...hakuna kazi nyepesi na nzuri kama ualimu ila inategemea namna mnavyo endesha shule ...kwa kukosa kwenu akili badala ya kuitaka serikali ingalie maslai ya walimu kwa kuangalia ufanisi wa shule na masomo nyinyi mnataka serikali iwapatie mishahara mikubwa kwa kuangalia karatasi alizopata mtu chuoni wakati anasoma hata kama ufanisi wake kwenye ualimu shuleni ni 0
Ulianza vzri lkn huku mwishoni ukanivuruga mkuu😄😄
 
Yote wanayofanya waalimu kwa serikali ya ccm lakini wanawachukulia poa
Wakina dotto magari,mwijaku babalevel nk wanathaminiwa na ccm kuliko hata hao waalimu

Ova
 
Mnatutisha sisi vikongwe wa kitaa miaka 6+ tunalamba jiwe tunakaribia kujifariji tena tuendako mnatuambia ni chuma alooooo
 
Kama ushaingia ushauri wako wa mwisho ni upi
1.PUNGUZA MATARAJIO MAKUBWA

2.FANYA YALE YA MSINGI TU KAMA
KUJENGA NYUMBA NZURI YA KIISHI (ANGALAU ITAKUFARIJI) TOFAUTI NA UKIWA UNATOKEA KWENYE PAGALA, USIPELEKE WATOTO EMS UTAPATA STRESS NA UTANUKA MADENI WATAFUTIE SHULE ZA KAWAIDA ILA ZENYE UFAULU MZURI.WASIMAMIE NA WAASE WASOMEE FANI NYINGINE ZENYE AJIRA KWENYE MATAASISI SIO HIZO ZA SANDAKALAWE🤝.

📌📌WAPELEKE VETA WAPATE UJUZI HUWENDA ITAWASAIDIA KUSURVIVE BILA KUTEGEMEA AJIRA ZA SANDAKALAWE.

3.KAMA UPO NJE YA MAJIJI JIKITE NA KILIMO.UNAWEZA UKABAHATISHA UKATOBOLEA HUKO ILA KUMBUKA KUFUMBA MDOMO UKIFANIKIWA HATA UKIYUMBA HUKO SHAMBANI FUNGA MDOMO!!!

4KAMA UPO NDANI YA JIJI FANYA BIASHARA ZENYE KUHITAJI MTAJI KIDOGO NA MUDA KIDOGO WA USIMAMIZI.FUNGA MDOMO KWA MATOKEO YOYOTE YALE YA BIASHARA YAKO.TAMISEMI PANAHITAJI KABA KOOO!!!

5.USIWAAMBIE WATU( WA MTAANI AU UNAPOFANYIA KAZI) SHIDA ZAKO,USIWAAMBIE MIPANGO YAKO,KUWA MYSTERIOUS USIPENDEZE SANA(MAKAZINI HASA TAMISEMI USIONE WATU WANAVAA MIPAUKO/MARONYARONYA😄😄😄 KADET NA MATISHETI HIYO NI CAMOUFLAGE ILA WENGINE NI MSOTO MKALI WA MAISHA😣) KAMA UTANUNUA GARI NUNUA YA KAWAIDA IKIWEZEKANA NUNUA USED 3RD HAND 🤗.HUKO WACHAWI NI WENGI NA WENGI HAWANA MATUNGURI ILA ROHO ZA CHUKI NA HUSDA.

6.JIFANYE FALA UKIWA KAZINI BE HUMBLE CHEKA NA KILA MTU( SALAAM NA KILA MTU) ILA USIJE WAKARIBISHA NYUMBANI NA IKIWEZEKANA WACHANGANYE BAADHI WAAMBIE UNAKAA MTAA X WENGINE WAAMBIE UNAKAA B ILIMRADI USISOMEKE.

📌📌📌SALAM TU STORY UNAWEZA KUCHANGIA ILA DONT SIMULIA MAMBO YAKO WEWE ONGEA STORI ZOTE AU TUNGATUNGA STORI ZA UONGO NA KWELI.AU FANYA KAMA WANA JF WEWE UKIWA UNAELEZA STORI MUHUSIKA WA STORI SEMA NI NDUGU,RAFIKI AU JIRANI YAKO KUMBE NI WEWE🤗🤗🤗

📌📌HUKO TAMISEMI/ HALMASHAURI NI VITANI KUNA MAJUNGU,WIVU,HUSDA UMASIKINI,MIKOPO ISIYO NA TIJA,MADENI LUKUKI,NJAAA KALI🔥🔥🔥NA KILA MTU ANAPAMBANA ATOKE/APANDE ILA KWA KUWAKANDAMIZA WENGINE!!!!
 
Mnatutisha sisi vikongwe wa kitaa miaka 6+ tunalamba jiwe tunakaribia kujifariji tena tuendako mnatuambia ni chuma alooooo
KAMA BADO HUJACHANGANYIKIWA ULIPOKUWA MTAANI SUBIRI UINGIE HUKO TAMISEMI HUTAAMINI.UTACHANGANYIKIWA MARA KWA MARA🤗🤗🤗

WENGI WANAJIFARIJI KWA KUHAMA ILA BADO SHIDA IPO PALEPALE HATA UKIHAMA UNAPOHAMIA BADO UTAKUTA MATARAJIO YAKO HAYATIMII AU YANAKWAMA TENA🙌🙌🙌

📌📌KWA AJIRA HIZI ZA SANDAKALAWE NASHAURI VIJANA YAFUATAYO;
1. ZAA MTOTO MMOJA UKISHINDWA SANA WAWILI.

📌📌📌AJIRA ZA SANDAKALAWE INFACT ZILITAKIWA ZIFANYWE NA WANAWAKE ILA MWANAUME ILI UWE NA NGUVU ZA KIUME( PESA) NA UJIAMINI NI EITHER UFANYE BIASHARA AU UAJIRIWE KWENYE TAASISI.HUKO SANDAKALAWE HAKUHITAJI STRESS PANATAKA WATU WASIO NA MAJUKUMU MENGI!!!

2.ZAA AU ANZISHA FAMILIA NA MTUMISHI MWENZAKO HASA KADA TOFAUTI ITAKUBOOST KIMTINDO IKIWEZEKANA MTASAIDIANA JAPO WANAWAKE AKILI ZAO WENGI WANAZIJUA WENYEWE

3.KAMA UTAZAA AU KUANZISHA FAMILIA NA MWANAMKE ASIYE NA KAZI BASI AWE MCHAKARIKAJI ILI ASIMAMIE MIRADI YA FAMILIA.

UKIOA AU KUZAA NA MATAKO MENGI/MAKUBWA AKILI KISODA,SURA NZURI SHAPE YA MAMA,UMEISHA!!! HUKO TAMISEMI HAMNA HIYO PRIVILAGE😁😁😁😁HUKO NI MCHAKAMCHAKA MPAKA SIKU UNASTAAFU.

📌📌EPUKA MIGOGORO YA NDOA MAANA MADAWATI YA JINSIA WATAWINDA HIYO SALARY YAKO WAKUVURUGE ZAIDI.

🚨🚨🚨🚨🚨KAMWE USICHUKUE MKOPO KUNUNUA GARI,USICHUKUE MKOPO UJENGE,USICHUKUE MKOPO KWAKUA ULIOWAKUTA NDO WANAISHI HIVYO, UTAJUTRAAAAAAAAAAAAAAAAAAA.CHUKUA MKOPO KAMA TAYARI UNABIASHATA UNATAKA KUBOOST SIO KUANZISHA BIASHARA.MWANZO WA STRESS NI KUPOKEA LAKI MBILI HUKU MKOPO ULIOCHUKUA UKIWA UMEPOTEA AU HAULETI MATUNDA TARAJIWA😵‍💫😇.

📌UKIONA UNASHINNDWA HAYO HAPO JUU AU BADO HUELEWIELEWI VUTA SUBIRA USIFANYE JAMBO LOLOTE KWA MKUMBO MAANA KILA MTU ATABEBA SHIDA NA MAUMIVU YAKE MWENYEWE.

📌UKISHINDWA KABISA KATAA NDOA🤝🤝🤝
 
1.PUNGUZA MATARAJIO MAKUBWA

2.FANYA YALE YA MSINGI TU KAMA
KUJENGA NYUMBA NZURI YA KIISHI (ANGALAU ITAKUFARIJI) TOFAUTI NA UKIWA UNATOKEA KWENYE PAGALA, USIPELEKE WATOTO EMS UTAPATA STRESS NA UTANUKA MADENI WATAFUTIE SHULE ZA KAWAIDA ILA ZENYE UFAULU MZURI.WASIMAMIE NA WAASE WASOMEE FANI NYINGINE ZENYE AJIRA KWENYE MATAASISI SIO HIZO ZA SANDAKALAWE🤝.

📌📌WAPELEKE VETA WAPATE UJUZI HUWENDA ITAWASAIDIA KUSURVIVE BILA KUTEGEMEA AJIRA ZA SANDAKALAWE.

3.KAMA UPO NJE YA MAJIJI JIKITE NA KILIMO.UNAWEZA UKABAHATISHA UKATOBOLEA HUKO ILA KUMBUKA KUFUMBA MDOMO UKIFANIKIWA HATA UKIYUMBA HUKO SHAMBANI FUNGA MDOMO!!!

4KAMA UPO NDANI YA JIJI FANYA BIASHARA ZENYE KUHITAJI MTAJI KIDOGO NA MUDA KIDOGO WA USIMAMIZI.FUNGA MDOMO KWA MATOKEO YOYOTE YALE YA BIASHARA YAKO.TAMISEMI PANAHITAJI KABA KOOO!!!

5.USIWAAMBIE WATU( WA MTAANI AU UNAPOFANYIA KAZI) SHIDA ZAKO,USIWAAMBIE MIPANGO YAKO,KUWA MYSTERIOUS USIPENDEZE SANA(MAKAZINI HASA TAMISEMI USIONE WATU WANAVAA MIPAUKO/MARONYARONYA😄😄😄 KADET NA MATISHETI HIYO NI CAMOUFLAGE ILA WENGINE NI MSOTO MKALI WA MAISHA😣) KAMA UTANUNUA GARI NUNUA YA KAWAIDA IKIWEZEKANA NUNUA USED 3RD HAND 🤗.HUKO WACHAWI NI WENGI NA WENGI HAWANA MATUNGURI ILA ROHO ZA CHUKI NA HUSDA.

6.JIFANYE FALA UKIWA KAZINI BE HUMBLE CHEKA NA KILA MTU( SALAAM NA KILA MTU) ILA USIJE WAKARIBISHA NYUMBANI NA IKIWEZEKANA WACHANGANYE BAADHI WAAMBIE UNAKAA MTAA X WENGINE WAAMBIE UNAKAA B ILIMRADI USISOMEKE.

📌📌📌SALAM TU STORY UNAWEZA KUCHANGIA ILA DONT SIMULIA MAMBO YAKO WEWE ONGEA STORI ZOTE AU TUNGATUNGA STORI ZA UONGO NA KWELI.AU FANYA KAMA WANA JF WEWE UKIWA UNAELEZA STORI MUHUSIKA WA STORI SEMA NI NDUGU,RAFIKI AU JIRANI YAKO KUMBE NI WEWE🤗🤗🤗

📌📌HUKO TAMISEMI/ HALMASHAURI NI VITANI KUNA MAJUNGU,WIVU,HUSDA UMASIKINI,MIKOPO ISIYO NA TIJA,MADENI LUKUKI,NJAAA KALI🔥🔥🔥NA KILA MTU ANAPAMBANA ATOKE/APANDE ILA KWA KUWAKANDAMIZA WENGINE!!!!
Mkuu umenena vema, nahii sio kwa walimu tu hata watumishi wengne wa umma, Maisha ni yaleyale kwa asilimia kubwa.
 
Pole sana mkuu,

Binafsi huwa naona kama una kazi haina kipato kizuri na haikupi muda wa kufanya vitu vingine au la wewe mwenyewe huwezi. Ni kheri ukae mikoani tena katika wilaya ndogo ndogo ambapo gharama za maisha zipo chini

Fikiria unalipwa laki nne au tano then unang'ang'ania kukaa Dar Es salaam na uishi kwa standard ya wafanyakazi wa, serikali. Lazma utakwama

Mungu awapiganie asee maana kwenye shughuli za kitaifa walimu wakishapewa posho, tshirt na ubwabwa wa kupangia foleni. Huwa mnasahau kabisa kupigania haki zenu
Naongea kutokana na uzoefu kidogo, nineona kwenye interview vijana wakipanga mistari mirefu kupambania ugali wao, wengine wamekaa mtaani zaidi ya miaka 10, na bado wapo wanapambana kwenye usahili,

Utakapo pata nafasi ya kuingia kwenye ajira, Moja Kwa Moja na utakutana na watu uko kazini wakiwa wanawaza kuacha kazi, yaani wewe unapambana uingie utakutana na watu ambao wanataka waondoke, wakiwa na depression na mawazo tele, utakuta watu senior, wenye miaka 10 kazini wakiwa hawana nyumba, stress zikiwa nyingi mnooo, utashangaa kuona watu wakishinda na cadet mpauko, bado utakua uelewi elewi, utakaa miaka mitano bila ya kufanya jambo lolote la maana, hapo ndio utaanza kupata depression.

Nimeona vijana wengi wakisema tukishaingia tutafanya biashara au tutafanya kilimo, niamini Mimi kati ya walimu 10 waliofanya hivyo mmoja tu ndio alifanikiwa, kwasababu biashara au kilimo lazima uwepo wewe utajichanganya ufungue biashara alafu umuache mtu hapo ndio utakua Mwisho wako.

Huwezi Fanya jambo lolote la maendeo bila kukopa, mfano ukiingia na degree utakopesheka million 18, na mshahara utabaki na laki mbili au tatu, sasa inategemea hiyo million 18 umeipeleka wapi, kama umeenda kujenga chumba na sebule basi ndio mwanzo wa kuishi maisha ya kifukara maisha yako yoote. Ukiiweka kwenye biashara na umemuweka mtu basi ndio mwisho wako huo.

Kukosa matumaini ya uliowakuta kazini, na miaka yako mitano uliyofanya kazi bila kumiliki chochote, ndio kitakufanya uanze kuwaza kuacha kazi, kuvumilia mateso tena unajikuta umepangwa vijijini uko, au kigoma, sumbawanga, Rukwa n.k hapo ndio utatamani urudi tu uache kazi urudi mjini.

Ubaya wa hii kazi hakuna marupurupu au pesa za kuiba, alafu unyonge wa walimu wa miaka iliyopita ndio itasababisha Kila mtu akuchukulie poa tu, ukijitambulisha wewe ni mwalimu hakuna heshima Wala recognition ambayo utaipata kwa mtu yoyote yule.

Karibuni kwenye ualimu, lakini kama una ndoto miaka Yako 15 ya ualimu utazidiwa na mtu aliyeko TRA, TPA mwenye miaka miwili kazini.

Believe me, nioneshe mtu mwenye status yoyote Tanzania hii ambaye kasomesha mtoto wake ualimu.

Asante.
Kama wewe ndiyo ualimu haujakupa mafanikio ni wewe ila ukienda mikoani utashangaa jinsi waalimu walivyofanikiwa kama wewe ni masikini ni wewe tu
 
Wewe ndo masikini, Huna hata haya? Unakuja humu kutapeli watu... huvi kama kungekuwa kweli kunautajiri kwenye huo upuuzi wako ungekuja humu kusema? Acha uzwazwa tapeli wewe.....
Shangaa na wewe eti kisa yeye ni masikini anahisi watu wote ni masikini kama yeye
 
Mimi sio masikini, ndio maana sitapeli watu... matapeli wote masikini, kwa sababu ni wavivu... mnataka kupata pesa za watu burebure
 
Asante sana, Bila kupepesa wewe ni mwalimu pasee.. na unajua maisha halisi ya walimu.

OMBI: Njoo na suluhisho namna ya kukwepa maisha hayo, Njoo na ushauri kwa waliokosea ,Tutakushukuru sana.
Bahati mbaya ni kwamba watoto wa maskini ndio tunasoma ualimu ili tuingie kwenye system mapema, suluhisho ni moja tu serikali iangalie miundo mipya ya mishahara haswa huku local government, teaching allowance iwepo, alafu kwenye swala la uhamisho kama mtu amepata wa kubadilishana naye, mlolongo usiwe mrefu, maana unaweza kupata wa kubadilishana naye kituo ikachukua miaka miwili, kubadilishana, je watu watakaa kuwaza jambo moja ilo ilo?
 
Mwalimu kama hajaachiwa urithi imekula kwake huo mshahara ni wa kula tu.Hauwezi kuutumia kufanya jambo lolote la maana!!!

📌Tatizo hii mitoto ya skuizi mibishi sana.
Na huyo anaepokea laki tano la 47 kama basic ni mtu mzima miaka 47, bahati mbaya hakuna mtumishi wa local government ambaye anaeweza kufanya maendeleo yoyote bila kukopa, kabla ya kukopa uwezo wa kula utakua nao, ukishakopa hata kula hutoweza tena.
 
Mnatutisha sisi vikongwe wa kitaa miaka 6+ tunalamba jiwe tunakaribia kujifariji tena tuendako mnatuambia ni chuma alooooo
Njoo mkuu ni bora kuliko kutokua nayo kabisa, uzuri mtaani ukopesheki milion 18, njoo uchukue hela zako,
 
Back
Top Bottom