Karibuni kwenye Kazi ya ualimu, lakini usiwe na matarajio makubwa

Sure bro kidogo niwe mwalimu wa mambo ya afya nikatoroka😅😅😅 karibu pombe hapa mkuu
Asante mkuu, najua utakua na simu yako unapiga mdogo mdogo huku unaburudika Jf 😊

Mimi mida mida ntapiga kidogo kutakatisha akili...wanaume lazima tutakatishe AKILI kwa mvinyo maana AKILI IKITAKATA..LAZIMA MWILI UNAWILI NA KUSTAWI.
 
Umeongea kweli, kila mtu duniani yupo na malengo yake kwa mfano Mimi sipendi kua chini ya mtu, na hii kazi lazima uwe chini ya watu, madharau n.k mpaka diwani, au mwenyekiti wa mtaa anaweza kukutukana na kukupelekesha.
Mwenyekiti wa mtaa wa wapi anayeweza kumpelekesha mwalimu? Labda huko Dar
 
Kufanikiwa na akili ya mtu lakin pia kw utafit wangu mdogo wengi waliofanikiwa japo sio wote waliamua kuoa au kuolewa na wenza ambao sio walimu so kukawa na balance ya kupata muda wa kusimamia miradi waliyoanzisha
unamaanisha walioa mama wa nyumban si ndio?
 
Naongea kutokana na uzoefu kidogo, nineona kwenye interview vijana wakipanga mistari mirefu kupambania ugali wao, wengine wamekaa mtaani zaidi ya miaka 10, na bado wapo wanapambana kwenye usahili,

Utakapo pata nafasi ya kuingia kwenye ajira, Moja Kwa Moja na utakutana na watu uko kazini wakiwa wanawaza kuacha kazi, yaani wewe unapambana uingie utakutana na watu ambao wanataka waondoke, wakiwa na depression na mawazo tele, utakuta watu senior, wenye miaka 10 kazini wakiwa hawana nyumba, stress zikiwa nyingi mnooo, utashangaa kuona watu wakishinda na cadet mpauko, bado utakua uelewi elewi, utakaa miaka mitano bila ya kufanya jambo lolote la maana, hapo ndio utaanza kupata depression.

Nimeona vijana wengi wakisema tukishaingia tutafanya biashara au tutafanya kilimo, niamini Mimi kati ya walimu 10 waliofanya hivyo mmoja tu ndio alifanikiwa, kwasababu biashara au kilimo lazima uwepo wewe utajichanganya ufungue biashara alafu umuache mtu hapo ndio utakua Mwisho wako.

Huwezi Fanya jambo lolote la maendeo bila kukopa, mfano ukiingia na degree utakopesheka million 18, na mshahara utabaki na laki mbili au tatu, sasa inategemea hiyo million 18 umeipeleka wapi, kama umeenda kujenga chumba na sebule basi ndio mwanzo wa kuishi maisha ya kifukara maisha yako yoote. Ukiiweka kwenye biashara na umemuweka mtu basi ndio mwisho wako huo.

Kukosa matumaini ya uliowakuta kazini, na miaka yako mitano uliyofanya kazi bila kumiliki chochote, ndio kitakufanya uanze kuwaza kuacha kazi, kuvumilia mateso tena unajikuta umepangwa vijijini uko, au kigoma, sumbawanga, Rukwa n.k hapo ndio utatamani urudi tu uache kazi urudi mjini.

Ubaya wa hii kazi hakuna marupurupu au pesa za kuiba, alafu unyonge wa walimu wa miaka iliyopita ndio itasababisha Kila mtu akuchukulie poa tu, ukijitambulisha wewe ni mwalimu hakuna heshima Wala recognition ambayo utaipata kwa mtu yoyote yule.

Karibuni kwenye ualimu, lakini kama una ndoto miaka Yako 15 ya ualimu utazidiwa na mtu aliyeko TRA, TPA mwenye miaka miwili kazini.

Believe me, nioneshe mtu mwenye status yoyote Tanzania hii ambaye kasomesha mtoto wake ualimu.

Asante.
Kama umekosa matumaini wewe... na kanuni ya maisha hujaitunga wewe.. hivyo usikatishe watu tamaa na ukae kwa kutulia... wewe kama una amini hivyo sawa... ila usilazimishe mawazo au maoni yako yawe uhalisia
 
CCM hawathamini waalimu hata kidogo

Wewe ni mwalimu? Umeajiriwa? Au na wewe ni mmoja wao ambao hata nauli za kurudi nyumbani ni shida?
 
unamaanisha walioa mama wa nyumban si ndio?
Tafutaa anayejituma na mwenye maono hata kma mwanzo atakuwa mama wa nyumbani muongoze afanye nn na msimamie ukiweka hata bomba atakusaidia kuuza maji kuangalia bustani hata mashamba pia
Muhimu uwe na vision Mpe kazi na muongozo nn unataka. Wwotee mkiwa walimu kasheshe ujuaji mwingi muda hakuna hat biashara ya mtaji wa milioni 1 mtahitaji mfanyakzi
 
Mimi ndio nafanya hivi, sitaki mfanyakazi Bora nifungue biashara niwe nasupervise nikiwa na mke wangu, ni ngumu kutafuna mtaji woote wakati familia inateketea,
 
Wewe ni mwalimu? Umeajiriwa? Au na wewe ni mmoja wao ambao hata nauli za kurudi nyumbani ni shida?
Nilishawahi kukuomba nauli? Kama umekata tamaa ni wewe... pia mimi si mwalimu... lakini nawafahami waalimu wengi tu maisha yao mazuri
 
Back
Top Bottom