Karibuni tujadli kuhusu zabuni

Karibuni tujadli kuhusu zabuni

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Habari za weekend;

Kwa wali wanaosalia najua mmewahi kumuomba Mungu awapatie Mkate wenu wa Kila siku.

Leo nataka tuzungumzie kuhusu TENDER au kwa Kiswahili TENDA.Tenda huwa zinakuja kwa lugha tofauti kama vile INVITATION TO TENDER,EXPRESSION OF INTERESTS,REQUEST FOR PROPOSAL,REQUEST FOR QUOTATION na majina mengine yanayokaribiana na hayo.Kuna tender amazo kushiriki tu lazima uchangie malipo fulani hasa za serikalini.Tenda nyingine huhitaji uthibitisho wa uwezo wa kipato kama vile Bank Guarantee,bonds etc. Tender ni Moyo wa kampuni na ni msingi wa mafanikio katika kampuni yoyote.

Unapokuwa msimamzi na mmiliki wa kampuni ni lazima uzingatia na kuelewa kwamba Tender na utaratibu mzima wa kusimamia na kutekeleza shughuli za kampuni unaendesha kwa kufuata taratibu na kanunu bora za manunuzi ambazo msingi wale ni TENDA.

Kwa nini ni muhimu kuelewa kuhusu TENDA kwa wamiliki wa kampuni?
Umuhimu wa uelewa kuhus TENDA sio tu kwa ajili ya kupata fursa za kibiashara bali pia ni muhimu katika kuhakikisha kwama kampuni nyake inapata pia huduma na bidhaa bora kutoka watoa huduma wake.Iwapo kampuni yako inafanya manunuzi bila kuzingatia kanuni za manunuzi uwezekano wa wewe kufuata kanuni za manunuzi wakati unapotoa huduma kwa wengine ni mdogo sana.

Hivyo basi kabla hujafikira kuhusu namna ya kushinda TENDA za kutoa huduma kwa watu wengine ni lazima wewe mwenyewe ufanye manunuzi kwa kufuata utaratibu wa TENDA na ukubwa/thamani ya biashara.Hata kama unataka kununua Computers au fenicha za ofisi au stationeries za ofisi au huduma ka hizo ni muhimu ukatumia utaratibu wa TENDA kutafuta mtoa huduma.Faida ya kufanya hivyo ni kwamba unapata fursa ya kutangaza kampuni yako kwani zile kampuni zitakazoitikia mwito wa kutaka kukupa huduma kuna siku pia watahitaji huduma kutoka kwako kwa hiyo ni fursa ya masoko

Unapotumia utaratibu wa kutangaza TENDA unakuwa na uwezo wa kuelezea unachohitaji kama ni bidhaa au huduma na kuweza kuwapima watoa huduma kwa kutegemea vigezo ulivoweka.

Unapotumia mfumo wa TENDA hata kama kampuni yako ni ndogo na MPYA utapata FURSA ya kujiweka kati eneo zuri na kujenga BRAND IMAGE YA KAMPUNI yako.

Mchakato wa kuandaa nyaraka za TENDA unakuwezesha pia kufahamu jinsi ya kufanya manunuzi na wewe utaweza kutumia mbinu hizi kuitikiwa na kujenda TENDA kwa makampuni mengine.

JE UNAWEZAJEKUJIBU MWALIKO WA KUSHIRIKI KATIKA ZABUNI?

Mwito wowote wa ZABUNI unalenga kuwashindanisha watoa huduma.Hivyo basi ni muhimu sana kuhakikisha kwama unapojibu zabuni unakuwa unaelewa hasa mahitaji ya MTEJA wako.Ukishahakikisha kuwa umeelewa mahitaji ya mteja basi utaweza kumuonesha mteja kwamba wewe unao uwezo wa kutatua au kumpatia huduma anayohitaji.

Mada ya ZABUNI ni mada ambayo inahitaji mjadal mpana hasa kwa kuzingatia kwamba katika eneo hili huwa kuna masuala mengi kama vile mikataba,rushwa na kujuana ambayo wakati mwingine huathiri mwenendo mzima wa ZABUNI.

Karibuni tujadli kuhusu ZABUNI na namna ambavyo biashara au kampuni yako inaweza kunufaika na mfumo mzima wa ZABUNI.


Karibuni
 
Shusha nondo zaidi kuhusu zabuni za serikali na namna ya kuzipata kwa uhakika
 
Back
Top Bottom