Karipio la Rais Samia: Unaiba hela ya Umma ikusaidie nini? Utazikwa nayo? Utajibu nini Mbele ya Mungu?

Nchi ngumu sana hii [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kukasirika bila kuchukua hatua ni kazi bure, wezi watishwe kwa hatua kali zinazochukuliwa dhidi yao, hayo mambo ya kujibu mbele ya Mungu wala hakuna wa kuyaogopa kama wangeyaogopa kila siku wanahubiriwa makanisani na misikitini wangesha acha.
Rais atumie sheria kukemea vitendo vya ubadhirifu sio maandiko matakatifu yeye ni rais wa nchi sio Amirat wa msikiti wa Chamwino
 
Tanzania tunachoweza ni wizi wa mali za umma, sio wazee wala vijana, wabongo kuwaongoza inahitaji Rais uwe tough kama jiwe, na ukiwa hivyo watalia roho yako mbaya, wanataka kudekezwa.
 
Tena wewe
Si mlisema Magufuli anaongea kikatili,

Mama wa watu anamwachia Mungu ila bado mnataka mumuandame
Asifoke-foke kama yule kambale bali asimame kama kiongozi atoe maelekezo kama sheria inavyohitaji na sio kumsukumia Mungu mzigo huo.
 
Ndiyo aelewe wanapomwambia anaupiga mwingi
 
Kwa kweli mama kaliweka katika upande wa dhamira invyoweza kumsuta mtu.

Hili limeonyesha kuna watu hawana dhamira njema na nchi hii.
Wasakwe.
 
Hakimu wa haki ni Mungu
Sisi kama walokole tunasimama na kauli ya Mama.
Mungu atahukumu na watakufa wataziacha mali.
Mkuu tusubilie hukumu,huku Tozo ziendelea,Shule hazina madawati, Wafanyakazi wa Umma wanazidi kuwa fukara, tunaendelea kukopa na riba juu,Shule hazina vifaa vya maabara,Barabara bado ni tatizo, huduma za afya bado ni changamoto.......hata Mungu mwenyewe atatushangaa na kutuona yale maarifa aliyotupa kuyatumia hatuyatumii........
 
Wapi huko hawana madawati?
Jiwe aliposema anapigania wanyonge alidhihakiwa na watu wakadai kuwa watz siyo wanyonge,,labda kama yeye mwenyewe ndo mnyonge🤣🤣🤣

"Hukumu ni juu yangu,"Asema Bwana wa Majeshi.
Tupo nyuma ya kauli ya Mama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…