I wish tungekua na rais ambaye anasema "Mwenyezi Mungu amenituma niwashughulikie wezi wa fedha za umma na walevi wa madaraka effectively"
"Umepewa fedha za mradi, umekula percent kadhaa, umepunja mradi mwisho wa siku haujakamilika. Inatakiwa CV yako ipigwe banned, kamwe usifanye tena kazi ya umma, na inatakiwa kesi yako iendeshwe haraka sana uanze kutumikia kifungo na adhabu ya makosa yako kwa mujibu wa sheria na ikiwezekana ufilisiwe" Yani kiongozi akizingua kwa makusudi hakuna second chance, ni banned for life. Mpaka watu waogope kuwa viongozi na sio kukimbilia kadi za chama ili wapate fursa za kucheza na fedha za umma.
Siku top leaders wetu wakiwa na mindset za hivi, vitu vingi vitanyooka. Ila mambo ya kumuachia Mungu na kusameheana kwa kuhamishana vitengo hayawezi kututoa tulipo. We need patriotic & responsible Leaders.
Story za wateuliwa kula hovyo kodi za watu tumezichoka. Na ni weakness kubwa sana kwenye utawala kama watu uliowakabidhi majukumu fulani wanakuchezea na huwawajibishi. Imagine mtu anakatwa kodi kwenye biashara yake au mshahara wake and then badala ya kuwaza kuwa hizi fedha zitasaidia kuleta ahueni kwenye nchi yake anaanza kuwaza kuna washenzi wanaenda kuzila kiu laini sana na hawatafanywa kitu. Ndio tumefika hapo!