Karma Haipo, Karma ni dhana ya kimaskini kuwafariji maskini

Karma Haipo, Karma ni dhana ya kimaskini kuwafariji maskini

Hata waafrika bado tunapigana vita na kuuana wenyewe kwa wenyewe.

Rejea mauaji ya kimbari Rwanda, Vita vya kagera, Biafran war Nigeria.

Vita mbalimbali bado zinaendelea Afrika huko Congo waasi wa ADF wanaua raia, Tigray Ethiopia watu wana uana sana, Cabo Delgado Msumbiji, Al Shabaab Somalia, Boko Haram,

Hata Tanzania tu watu wanauwawa na watu wasiojulikana.

Na vita vyote hivi si kwa sababu ya Karma, Bali ujinga wetu tu.

Watu weusi ndio wana ongoza kuuana wenyewe kwa wenyewe. Kushinda hata wazungu.

Marekani kukumbwa na vimbunga si Karma, Bali ni hali ya hewa na mabadiliko ya tabia ya nchi tu.

Hata hapa Afrika mbona tunapigwa na majanga ya asili mbalimbali.

Rejea tetemeko la ardhi la Kagera, mafuriko ya Libya, tetemeko la ardhi la Morocco. Mafuriko ya Kwa zulu Natal south Africa n.k

Hata hapa Tanzania tu, Vijana wanabwia unga. Nenda kwa wadudu Arusha chuga ukajionee, Au nenda Nairobi Kenya mitaa ya Dandora au Kibera Slums ukajionee wala ngada.

Kwa hiyo vijana wa ulaya kubwia unga si Karma ni tabia zao tu kama ilivyo kwa vijana wetu wabwia unga hapa Afrika.

Kwa hiyo matendo yote haya si Karma.

Bali ni matendo ya kibinadamu na mengine ya kijiografia kama majanga ya asili vimbunga, mafuriko n.k
ok,,umedhihirisha KARMA ipo bila wewe kujua, mauaji ya kimbari RWANDA ni jibu tosha kwamba karma ipo,kwani kutokana na kubaguana kati ya watutsi na wahutu{watutsi walijiona wao ni bora kuliko wahutu} ndo KARMA ikaingilia kati,,,huko NIGERIA yale mambo ya BIAFRA yalikuwa mauaji ya visasi kutokana na mambo ya ardhi,hapo CONGO,kutokana na serikali ya CONGO kubagua wa2 wenye asili ya RWANDA,M23 ikaibuka{KARMA} hata hapa kwe2 kutokana na wapinani kuteswan a kupotea kwa kutekwa{kwa mujibu ya vyombo vya habari},,,tunaona leo hii wanachama wa CCM wakiuawawa,,,leo hii tarehe 3/12/2024 nimesikia kwa masikio yangu kaka wa bosi mkubwa wa CCM mkoa wa kilimanjaro kauwawa kikatili bro!!!!!,,,,,KARMA-THE LAW OF NATURE ipo!!!!
 
Chawa na wafuasi wa Magufuli wanaikubali sana imani ya kuwepo kwa Karma.. Magu alifanya dhuluma na ushenzi wa kinyama baaae karma ikafanya kazi yake... Fyuu kafyekwa kwa fedheha kama hakuwepo mpaka msiba ukawa wa siri kama kafa punda
 
You don't need religion to have Morals. If you can't determine right from wrong then you lack common sense not religion.

Huhitaji dini ikufunze kutenda matendo mema, huihitaji dini ikufunze kwamba kuua au kuiba ni kosa. Haya mambo kwa mtu mwenye ufahamu na akili timamu anapaswa kuyajua automatically.

Wala huitaji dini ikwambie hivyo.
Dini ni sheria za ulimwengu, wewe unaongea hivyo kwasababu umezaliwa umeukuta huo utaratibu upo hivyo kwahiyo nawewe umejifunza kwa jamii iwe unakubaliana na mimi au unakataa ila kiukweli watu wote huwa tunazaliwa tukiwa empty kichwani then tunaanza kujifunza miongozo mbalimbali ya dunia kwa njia ya kuskia, kuona au kusoma katika vitabu mbalimbali na mambo haya yote huwa yanahifadhiwa kichwani mwa mtu.

Kwahiyo hoja yako yakusema kwamba mtu yeyote mwenye akili timamu haitaji dini ili ajue jema na baya ni kweli kwa maana mambo yote ya kwenye dini tayari yapo katika jamii tulizozaliwa kwahiyo tulishajifunza hayo indirectly.

Watu huishi kwa kufuata utaratibu wa ulimwengu na utaratibu wa ulimwengu ulitengenezwa na dini kwa maana dini ndio sheria za ulimwengu.

Sijali kama unaamini Mungu au huamini au unaamini Dini au huamini ila utaratibu wa maisha ya kila mwanadamu hapa duniani ni matokeo ya dini, directly au indirectly.
 
Wahadzabe na Watindiga kule maporini mbona hawana dini na wanaishi vizuri tu, kwa kufuata taratibu zao.

Sasa utasemaje kwamba dini ndio sheria za ulimwengu, ilhali kuna watu hawana hata hizo dini na wanaishi kulingana na sheria zao za jamii yao?
 
Nakuhakikishia jamii yoyote ambayo haijawahi kuchangamana na watu wengine na wala haijawahi kuskia taarifa tofauti kutoka maeneo mengine ya dunia mtindo wao wa maisha hauwezi kuwa sawa na watu ambao wako na muunganiko wa moja kwa moja na dunia.

Sijui chochote kuhusu hayo makabila uliyoyataja ila kama hayana muunganiko na dunia kwa maana ya kwamba hakuna taarifa mpya zinazowafikia kutoka katika maeneo mbalimbali ya dunia basi mfumo wa maisha yao hauna tofauti na wanyama wengine wa porini.
 
Sawa lakini, kumbuka hii dunia, kunasiri nyingi sana katika maisha yetu sisi binadamu, hatuwezi kufahamu zote, nakupa mfano mdogo tu, uchawi, unafaida na hasara, uko kwajiri, ya kusapoti watu, ambayo wanadhul
Neno "uchawi" maana yake ni nini?
 
Mimi ninachosema hapa ni kwamba,

Hakuna kitu chochote kile kinachotoa majibu ya mambo yetu hapa duniani.

Majibu ya mambo yetu ni sisi wenyewe.

Hata hiyo karma ni dhana ya kutungwa tu na sisi wenyewe.

Ila in reality hai apply na haipo.
Lakini uchawi upo na watu wanalogwa na wanadhulika, mambo mengine huwa, nakukubali sana mkuu lakini uchawi, huwa unakataa haupo, haaa" hapo nakupinga?
 
Karma Doesn't exist.

Karma ni dhana ya kimaskini inayowapa matumaini uchwara watu maskini kujifariji na matatizo yao dhidi ya watesi wao.

Mababu zetu waliteswa sana na kusulubishwa ipasavyo wakati wa utumwa na ukoloni, Lakini hiyo karma haijawahi kufanya, haijafanya na haitakaa ifanye chochote dhidi ya wazungu.

Waafrika wamebaki maskini na wazungu wanazidi kuwa matajiri.

Unafikiri matajiri watateseka kwa sababu ya kudhulumu maskini kisa eti kuna karma?

Haitakaa itokee, Sahau na futa hii dhana kabisa akilini mwako.

Tuanze tu hapa Afrika. Watawala wengi na viongozi wa serikali wamekuwa wakiwahujumu wananchi wao kwa ufisadi, wizi wa fedha za umma, ubadhirifu wa mali za umma na kuwasulubu raia wao kwa kuwatwanga kodi kubwa.

Wananchi wanabaki kulia lia tu, Mara oooh! Tunamwachia Mungu, Mungu atatenda, Mungu atafanya, Mungu atatulipia, Wengine wanajifariji Karma itawafunza viongozi wao!! Na maneno mengi ya kujifariji. Lakini mwisho wa siku hakuna kinacho tokea.

Watawala na vizazi vyao wanazidi kuneemeka na kutajirika huku wananchi walala hoi na vizazi vyao wanazidi kuwa makapuku, makabwela, mafukara na maskini choka mbaya pangu pakavu tia mchuzi.

The rich goes richer, the poor goes poorer.

Kama karma ingekuwa inafanya kazi kweli, Manung'uniko yote ya wananchi maskini kudhulumiwa na wanasiasa matajiri yangefanya karma iwafikie wanasiasa wote na kuwafanya wabadilike.

Lakini hakuna kinachotokea na karma haionekani kusaidia chochote zaidi ya kuwapa matumaini uchwara tu, wadhulumiwa watu maskini.

Maskini wanazidi kuwa maskini na manung'uniko yao na matajiri wanazidi kuwa matajiri licha ya kuwadhulumu maskini.

Karma is an illusion.

Forget about karma, Make your own money live the best life you can live. Stop hoping that karma will catch up with your oppressors. It won't.

Never think that the rich will suffer because they oppress the poor. Never they won't.

Mababu zetu waliteswa sana na wakoloni na hiyo karma haikufanya chochote.

Watawala na viongozi wa Afrika wanazidi kuwatesa waafrika na hiyo karma haifanyi chochote.

Karma doesn't exist. In the jungle of life salvation is largely on your hands.

I'm out.
Haki ya mtu huwa haipotei, asipoipata hapa duniani utaenda kuilipa mbinguni na mbaya zaidi huko hutokua na cha kumlipa ,zaidi na zaidi uchukuliwe swahabu zako au dhambi zake upewe wewe
 
Unajuaje ni uchawi na si maarifa ambayo wewe huyaelewi?
Mtu kufanya maarifa hasionekane ni uchawi, uchawi kufanya jambo utokujulikana, kwa ukawaida yani gizani tofauti na sayansi? Vitendo unaviona tena kwa watu, wengi na LIVE??
 
Mtu kufanya maarifa hasionekane ni uchawi, uchawi kufanya jambo utokujulikana, kwa ukawaida yani gizani tofauti na sayansi? Vitendo unaviona tena kwa watu, wengi na LIVE??
Wachawi ni binadamu kama sisi.
Na wanaweza kufanya vitu ambavyo hata wewe wakikufundisha, utaweza kufanya kitu hichohicho kama wao unachodai ni uchawi.

Sasa kama mchawi anaweza kukufundisha wewe uchawi, Huoni kwamba hicho unacho kiita "uchawi" ni maarifa tu ambayo wewe huyaelewi kwa vile bado hujafundishwa na ndio umeamua kuyaita uchawi?

Ila kwao sio uchawi. Ni utaalamu tu ambao wewe bado huujui.

Utathibitisha vipi ni uchawi na si maarifa mengine ambayo wewe huyaelewi na bado hujafundishwa?
 
Hiyo ni nguvu ya kufanya kwa siri bila uthibitisho, au kutambulika, jina litabaki "UCHAWI" maarifa hayajulikani na mfanyanyaji, lakini mfanyaji unamuona anafanya? mfano: sisi tulipokua skuli kunajamaa alikuja alitambulika wa mazingaobwe anauwezo wa kukata kichwa na kukirudishia tena na kawa mzima, alikuja kutoa burudani, ila kwa viingilio pesa, mwafunzi, yani alifanya maajabu mengi karatasi alivigeuza kuwa pesa, cc kujua haya maarifa ndo u
 
Mkuu,
Hujaona uzao wa akina Tip Tip wanavyoteseka pale Mashariki ya Kati?!

Ule ukatili wa kubebesha watumwa mizigo mizito, ikiwemo ya pembe za ndovu, nk, huku wamefungwa minyororo na kutembea umbali mrefu sana, kutoka Kigoma, Tabora.. hadi Pwani usingepita hivi hivi
Huo uzao uko mkoa gani!
 
Back
Top Bottom