Karma is Real!, Kutumbuliwa ni Karma za Matendo Yako!. Ukitumbuliwa Kwa kosa la Kuusema Ukweli, ni Uonevu!, Rejoice!, Karma Itakufidia na Kukulipia!

Karma is Real!, Kutumbuliwa ni Karma za Matendo Yako!. Ukitumbuliwa Kwa kosa la Kuusema Ukweli, ni Uonevu!, Rejoice!, Karma Itakufidia na Kukulipia!

Kama haukujua kwanini aliteuliwa kamwe huwezi kujua kwanini katenguliwa.

Anayekupa majukumu ndiye anayekupima na kujua utendaji wako, unaweza kusena Nape mdomo umemponza kumbe mkeka ulishaprintiwa Toka mwezi WA SITA ukaachwa upoe.
 
Hivi hii karma haifanyi kazi kwa watekaji, waiba kura na waliomshambulia Tundu Lissu, waliombambikia kesi ya uhaini Mbowe?

Kama haifanyi kazi kwa hao wanaodhululumu uhai wa wengine hii karma itakuwa ni uchawi wa kisukuma
 
Wanabodi

Mimi ni mwalimu wa somo linaloitwa karma humu jukwaani.

Karma ni kuhukumiwa kwa mawazo yako, maneno yako na matendo yako, wazungu wanasema, what goes around, comes around.

Nashauri kama huijui karma, anza bandiko hili kwa kujifunza kuhusu karma "The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa Duniani!, Unahukumiwa kwa Matendo Yako!

Jana kumefanyika utenguzi na utumbuzi wa mawaziri 3. Hivyo kutumbuliwa kwao ni matokeo ya mawazo yao, maneno yao na matendo yao, kutumbuliwa huko ni haki yao na stahiki yao.

Niliwahi kushauri

Ila hata kama kuteuliwa ni just kwa pleasure ya the appointing authority, na unateuliwa by favours tuu na sio kwa kustahili na stahiki, pia kwenye kutenguliwa, unaweza kutenguliwa uki fall out of favours za the appointing authority, na ukatenguliwa bila kosa lolote, na mteuzi akawa hajafanya kosa lolote kwasababu uteuzi na utenguzi is at the pleasure tuu za mamlaka ya uteuzi.

Lakini kwenye kutumbuliwa lazima mtu ufanye kosa la kustahili kutumbuliwa, ukitumbuliwa kwa uonevu, then karma itaingilia kati kukufidia na kukulipia!.

Mfano kutumbuliwa kwa Nape, inawezekana kabisa ni accumulation ya karma za mabao ya mkono yote aliyoyasimamia, hivyo ametumbuliwa kwa haki. Lakini kama ametumbuliwa kwa kosa la kuusema ule ukweli wa kinachofanyika kwenye uchaguzi, then Nape ameponzwa na mdomo wake, ila hicho alichokisema kama ni kitu cha kweli na huwa kinafanyika, then Nape ametumbuliwa kwa kuonewa hivyo anatakiwa ku rejoices na karma itamfidia na kumlipia! .

Kwa vile Nape aliyatamka hayo kwa Byabato, jee Byabato kosa lake ni nini hadi kutumbuliwa?, inawezekana ni kauli ya Nape!, hivyo Byabato ametumbuliwa kwa kuponzwa na Nape bila yeye kufanya kosa lolote, hivyo ametumbuliwa kwa uonevu. This being the case, Byabato anatakiwa ku rejoice, atafidiwa, na kulipiwa!.

Kwa January, kiukweli sijui kama ilivyo kwa Balozi Liberata Mulamula, mpaka leo sijawahigi kujua sababu, ila tayari Balozi Liberata Mulamula karma imeisha mfidia sasa ni resident lecturer wa diplomasia chuo kikuu cha John Hopkins University nchini Marekani akila dola za kutosha tuu!.

Niliwahi kuandika humu Pongezi Rais Samia kwa Kutuhisania Openness and Transparency Kwenye Uteuzi, Mnaonaje Ifanyike Kwenye Utenguzi na UtumbuzI Iwe ni Haki na Sio Hisani?

Watanzania tufike mahali tu demand the right to information wakati wa utumbuzi, mfano mpaka leo, sijawahigi kujua, kwanini Balozi Liberata Mulamula alitumbuliwa, sasa January Makamba nae ametumbuliwa, natamani kujua sababu. Sihitaji kujua sababu ya Nape kutumbuliwa itakuwa ni mdomo umemponza kwa ile kauli ya Waswahili ya "mzaha mzaha, hutumbua usaha", lakini kwa Byabato ana kosa gani?.

Nashauri tumsaidie Rais Samia, asifanye kitu kinachoitwa " bad karma accumulation" bila kujijua, japo uteuzi na utenguzi is at the pleasure of the appointing authority, ukimtumbua mtu bila haki, kwa namna inayomdhalilisha, huyo mtumbuliwa akiumia, ana develop bad karma ya maumivu yake, hiyo bad karma inahifadhiwa katika akiba ya karma accumulation ya aliyesababisha maumivu hayo!, hivyo hii accumulation ina pile up, ikifikia kuwa the pile is big enough hadi furushi hilo la karma likawa halibebeki, then hilo zigo la karma, litamuelemea mbebaji sometimes linaweza kumponza na ... ndio maana nimewashauri viongozi wetu wateuliwa Wito Kwa Viongozi Wetu: Unapokosea, hata kwa kujikwaa tu ulimi, tujenge utamaduni wa kuwajibika ili kumuepushia Rais wetu kubeba mzigo wa karma
Paskali.
Correct I if am wrong! Utaratibu wa uteuzi na utenguzi at a pleasure of the appointing authority sio kabisa at this age of democracy. Ni mwendo wa kupiga mark time tu katika utekelezaji wa maendeleo na sera tengefu. I can't perform with confidence, ni bora hata mchezaji wa kabumbu anajua at least frist half kuwekwa bench ni hadi injury Ila sasa ukipangwa na hutarajii hata first half kumaliza na wala hujui then you can't perform
 
Yahya sinwar hataki kuachia uongozi wa Hamas licha ya kujificha chini ya ardhi akitembea kama mfu.

Adiosamigo
Huyo mwamba myahudi hatamweza kamfunga jela zaidi ya miaka 20 kule jangwani negev Israel mpaka leo anamtesa. Unaambiwa sinwar anaongea kiebrania kama anavoongea kiarabu (akili mingi) intelligence yote ya IDF anayo kiganjani wamweza huyo?
 
Wengi hawajakuelewa.

Ni kweli ameonewa kutumbuliwa kwasababu alichosema ni kweli.
Mkuu jmushi1 , kiukweli ma deep thinkers humu jf, ni wa kuhesabika, thanks, you are one of them!.

Ni watu wachache sana wanajiuliza why yule Blaza wangu had to go!, no one knows for sure, but it's karma, due to accumulation of bad karma kwa matendo yake.

Miongoni mwa bad karma ni utumbuzi wa majipu usio wa haki!, hili nililizungungumza humu Hii Tumbua Tumbua ya Rais Magufuli, Hivi Kikwete Anajisikiaje?!. Anajisikia Sifa Au Anajuta?!. kisha nikauliza Could There Be A Double Standards Kwa Viongozi Wadanganyifu?!. Wengine Fired, na Wengine Spared?!. na kumalizia na hii Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The Right Time, And Doing It Right, Or ?!

Mwisho wa siku...
P
 
Huyo mwamba myahudi hatamweza kamfunga jela zaidi ya miaka 20 kule jangwani negev Israel mpaka leo anamtesa. Unaambiwa sinwar anaongea kiebrania kama anavoongea kiarabu (akili mingi) intelligence yote ya IDF anayo kiganjani wamweza huyo?
Licha ya yote anaishi sasa hivi kama panya.
 
Nyie mnazunguka sana, lakini ukweli ni kuwa CCM haitufahi, wana bahatisha kwa kila jambo over 60 yrs. Hatuna viongozi kutokana na mfumo mbovu wa elimu, mfano Rais unaejitambua huwezi kuweka mambo ya wizara ya habari na wizara ya technology pamoja, kama huwezi kutofautisha hivyo vitu viwili tayari ni failure kwa mteuzi na kama nchi hatujui tunataka nini.

Duniani, nchi zilizoendelea karibu 30% ya GDP inatokana na kukua kwa shughuli za kitechnologia , mfano research, smart cities, innovation, satellite, digitalisation, information security, chipsets, frequency auction , aviation ,finitech etc exports ya technology ndio umeweka nchi kama USA, Europe , China na Japan on top of their economy, ni kitovu cha kitega uchumi duniani, wizara kama hii unampatia Nape Nnauye asiekuwa na uelewa wowote ule wa masuala ya technology kichwani ni dhihaka kubwa sana kwa watanzania.

Kwa kutambua ujinga huo nape alikuwa ana focus zaidi kwenye mambo ya habari tu , media, social media na kucheza na wasanii kwisha kazi, na kufunga magazeti, kazi za kijinga jinga .

Mnaweza kutuambia ndani ya miaka miwili, Tanzania technology imekuwa kiasi gan? Tumefanya innovation na kuuza technology ipi ndani na nje ya Tanzania?au sisi imetunufaisha vipi?, Zero.

Kwahiyo anae teua na kutengua wote ni zero brain ndio maana ccm haitakiwi kuwepo duniani, tunaongozwa na chama chenye uwezo mdogo sana, hivyo kupoteza muda na kuishia kufanya vitu vidogo kila miaka na wao kuita maendeleo.
 
Back
Top Bottom