Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Akiwa katika mahojiano yake ya kuthibitishwa kuwa Mkurugenzi mpya wa FBI, Kash Patel alipoanza kwa kuelezea historia ya familia yake alisema baba yake alikimbia Uganda ya Idi Amin, dikteta muuaji wa kimbari ambapo Wahindi laki tatu(300,000) waliuwawa kwasababu ya kuwa Wahindi kama yeye tu.
Huu ni uongo mkubwa sana, pamoja na ukweli kwamba dikteta mwendawazimu Idi Amin aliua watu wengi sana katika utawala wake lakini isingeweza kuua Wahindi laki tatu kwa sababu wakati alipopindua nchi kushika madaraka Wahindi wote nchini Uganda walikuwa hawazidi laki moja.
Kash Patel MAGA maarufu wa conspiracies za kila aina amewaingiza chaka na kuwalisha matango pori seneti ya Marekani ambayo ni chombo chenye nguvu na ushawashi mkubwa sana duniani!